DOKEZO Wanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Chanika wazuiliwa kuingia darasani kutokana na kutochangia 500 ya masomo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Governor of Bettors-GB

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
9,874
8,895
Ninawajulisha tuuuu,mpita njia wenu.

CC:-
  • Afisa Elim Kata (Limemshinda au kajiongeza)
  • Afisa Elim Wilaya (Hasomeki,vikaoni haendagi)
  • Afisa Elim Mkoa (anajua mambo saafi kwa wa chini yake)
  • Wizara ya Elimu
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Chanika wanaojiandaa na mitihani ya Darasa la Saba wengi wao wamezuiliwa kuingia kwenye masomo kwa kutokuchagia Tsh: 500 kila siku ili kuingia darasani, pia Tsh. 1,000 kila Jumamosi.

Watoto wengi wapo nje ya mazingira ya shule, huku wenzao waliotoa Tsh. 500 wakiwa darasani.

Nahisi hii sio sahihi, kutumia advantages za Darasa la Saba kisa kukabiliana na mtihani, muda wa masomo wa kawaida ni haki ya wanafunzi wote.

Remedios ndio iwe optional.
 
Ukiwa unaona elimu ni ghali basi,basi jaribu ujingaaaaa🎼🎼🎼🔊🔊🔊📢📢 ...R.I.P Banza
 
Pole Shule za ilala hata msemeje hawashughulikiwi ng'ooo hao wanakula na watu Wa juu magu mwenyewe alishindwa sembuse mama
 
Mbona haya mengi sana, nendeni Kilombero ndo mtashangaa. Kuna kitu kinaitwa makambi inakamua wazazi pesa acha kabisa. Hasa shule za kata ya Kidatu.
 
Back
Top Bottom