mkuu nashukuru sana kwa kuitikia wito wa post hii.
Mimi nina elimu ya degree ya kwanza katika field ya logistics and transport management, class of 2015.
Umri wangu ni miaka 25, single. Naishi Dar kwa sasa.
naongea lugha kuu moja tu ya kigeni, yaani English. Ila nina mpango wa kujifunza na nyinginezo ambazo zitakuwa na umuhimu katika majukumu yangu.
Kwa sasa sijapata uzoefu wowote katika field niliyosomea, zaidi ya kufanya field work ya miezi miwili tu katika bandari ya mwanza south.
Karibu sana mkuu.
Napatikana kwa +255653811003 or e mail
ayotekniktz@gmail.com
Australia, Kanada na New Zealand wanaweza kukupa viza ya kuishi huko kwa elimu yako.
Kuna vitu viwili vya kuzingatia. Uzoefu wa kazi na muda gani umefanya kazi. Umesema huna uzoefu, itakuwa vigumu kukidhi vitu wanavyohitaji.
Lazima ufanye kazi katika fani yako siyo chini ya miaka mitano.
Lazima ufanye mtihani wa Kiingereza kwa kuwa ni Mtanzania.
Angalia Logistics katika tovuti zao kama wanahitaji. Kuna fani nyingi na zinabadilika kila mwaka.
Utapata police clearance katika wizara ya mambo ya ndani ( gorofa la tatu) kwa kuwapa fingerprints zako, baada ya wiki, unapewa barua yako inayosema wewe ni raia mwema.
Utafanya ukaguzi wa afya yako na daktari wao. Utaambiwa wapi ukifanikiwa.
Tayarisha Transcripts za masomo yako ya sekondari na Chuo .
Lazima pia ujipange kulipa gharama. Viza ni $1000-2000. ( permanent , baada ya miaka 4-5, unaweza kuomba uraia wao).
Lazima uwe na uwezo wa $20,000 benki. Huwezi kuomba misaada ya serikali ukifika huko mpaka uwe raia.
Google " Canada / Australia immigration" halafu soma somo wanalolihitaji katika listi yao.
Kama somo lako, halipo, unaweza kusoma masomo mengine katika listi.
Kuna wakati walikuwa wanahitaji mpaka vinyozi wa nywele huko na wapishi. Ukipenda unaweza kusoma upishi Kama ipo kwenye listi.
Dunia ya Leo ni ndogo sana. Kuna nchi nyingi unaweza kufanya kazi. Ni kujipanga tu.
Ukiwa na swali, usichoke kuuliza.
Good Luck.