Nimemcheka sana rafiki yangu kutoka Ghana kwenye kilimo cha Almond nikamkumbuka mzee wa Madungu jeshi kwenye kilimo cha Canola

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,734
29,124
Mzuka Wanajamvi,

Huyu Mghana tulikuwa tunabeba naye boksi pamoja. Akaomba mkopo benki akapewa kama/equivalent dollar za marekani elfu 40.

Hela ilivyoingia benki yani ilikuwa fujo. Kesho yake hakwenda kazini na kuacha kazi hata bila kutoa taarifa.

Akaniita tupige pombe. Nakunitambia hela na anaenda kwao kulima Zao la Almond na atakuwa billionaire.

Jamaa alinitambia akienda nakurudi ulaya ataendesha benz S class mpya.

Nilimshauri jamaa asikurupuke aendelee tu nakuajiriwa kubeba boksi. Nikampa mfano wa homu tikiti maji, ufuta na vanilla wapiii?

Nikampa mfano wa mNepal flani naye alichukuaga mkopo kuanzisha pizza kebab biashara ikafa akaingia blacklist. Lakini wapii.

Akaenda zake Ghana mambo yakawa mabaya. Karudi ulaya kimya kimya hela zote kwisha. Wanoko walinishtua jamaa karudi anabeba boksi kimya kimya kwa kujificha.

Jana ghafla tumekutana naye tukapishana akataka kunikwepa niliangua kicheko cha ajabu na hatariiii. Nakumuukiza where is the Mercedes Benz S class? Hakujibu kitu kimya akakatiza na mimi kuendelea kuzichana mbavu. Yani nilicheka hadi sasa hivi najiuliza na kushangaa msela Mbona akunipiga kwa kicheko kile?

Mwaka juzi au jana mwanzoni nafikiri mwamba mpenda sifa wa madungu jeshi alikuwa na ziara zake kama kawaida rural Britain ndani ndani huko vijijini Uingereza kusaka madungu Jeshi na Trekta.

Akafika kwenye shamba moja kubwa la zao la Canola na kumhoji mkulima.

Basi ikawa fujo huko FB. Akatamba wabongo wako nyuma hawafikiri wenyewe wamebez tu kwenye Alizeti. Wakati hili zao la canola rahisi sana kulima na kuvuna na kutajirika upesi.

Akatamba anakuja bongo na kulima na kusaidia watu wanufaike na kushusha mbegu za canola za kutosha.

Akatoa hadi mifano ya mabilionare wa Canola. Na weraaa weraaa kibao katikati ya motivational speaking yake.

Alitoa Mfano jamaa flani huko Iringa sijui njombe analima zao la Canola lakini ni mchoyo hana ushirikiano hataki kusaidia wengine connection lakini alikataa kumtaja jina.

Basi ikawa Canola ndio story mwezi mzima kwenye FB na jinsi atazalisha mafuta ya kula na kutoa mafunzo motivation speaker.

Mara ghafla jamaa kimya kuhusu Canola. Hata akija Bongo likizo halizungumii kabisa.

Wadau tukajiridhisha jamaa alianza kulima akapigwa au ilishindikana. Kwa mbwembwe zile. Itakuwa tu alipigwa kwenye Canola akaamua tu kukausha na kukomaa kwenye madungu jeshi.


Tuliona tikiti maji, ufuta, vanilla mayai ya kware. Twendeni polepole na tujifunze
 
Raha ya ngoma, uingie ucheze.

usije ukaona mpemba pale mbezi beach kwa zena anauza chipsi kuku na nyama choma mpaka usiku wa manane ukajua ni kazi rahisi. Ukakurupuka na wewe ukaanza kuuza chipsi, nakwambia utaumia.

mambo ya dunia hayaendi hivyo.
 
Back
Top Bottom