Tusio na kazi tukutane hapa

Tusio na kazi tukutane hapa

Mimi pia sina kazi ila najitahidi majirani zangu wasijue ndio maana usiku kucha nakesha JF, mchana kutwa nalala nikiamka jioni naenda kwa ndugu jamaa na marafiki kudowea msosi!
 
Mimi pia Ni clinical officer nipo mtaani sipo job ndugu mkisikia nishtue jamani.
 
Nipo mtaani nna uzoefu wa mambo ya reservation.Nimrahisi kufundishika system ya aina yoyote as nafahamu system mbili ambazo ni Opera na IDS.
Sichagui iwe kaz za hotel,tour company au Airways company.
 
Kilimo chenyewe mbona mazao bei chini pia. Na jukwaa litatusaidiaje kupata ajira au kujiajiri. kama kuna mtu ana ushuhuda wa kikundi kilichofanikiwa basi tufanye.
Inategemea mkuu haiwezekani mazao yakawa bei chin mwaka mzima,pia kilimo si lazma uingie shamba unaweza kuwa mlanguz pia,fanya kilimo kama kaz na sio kama kimbilio lakukosa kaz
 
Ndugu zangu huu uzi wangu niliuandika mwaka jana, ila mpaka sasa sijapata kazi yeyote, naombeni mnisaidie
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Naomba msaada wako ndugu yangu


Habarini za muda huu mpendwa

Pole na miangaiko ya hapa na pale, ya kuhakikisha tunajenga familia zetu vyema na taifa letu la Tanzania kwa ujumla.

Kwa wale wagonjwa/wanaouguza poleni sana na mwenyezi mungu mwigi la lekhema awape nguvu mpya na kuwaponya kabisa ili mrejee kwenye majukumu yenu ya awali.

Niende kwenye maada moja kwa moja

Ndugu yangu Mimi ni mtanzania mwenzako ninapitia wakati mgumu sana nahisi kuchanganyikiwa maana umri pia unasonga sana na sina chochote.

Kwanza kabisa nikili mbele zenu napenda sana kuja kuwa "Mfanya biashara" kwanini sikufanikiwa uko

Nilipomaliza Elimu yangu ya Diploma (diploma in computer science )

Nilipenda nipate mtaji ili nifanye biashara, kwanza kabisa ilinilazimu kutafuta kazi ili nipate mtaji na pa kuanzia...

niliangaika sana na kutafuta kazi yapata mwaka mzima pasipo kuambulia chochote...

Note: aliyenisomesha diploma ni ante yangu, pesa yake alipenda kuitoa kwa kunisomesha tuu na sio vinginevyo (ndio msimamo wake ulikuwa ivyo)...

Nilisha jaribu kumshawishi kwa namna moja ama nyingine anisaidie mtaji wa kiasi fulani ili baada ya mzunguko wa biashara nitairejesha pesa yake yote, alikataa alisema "kama unataka kuendelea na shule ntakulipia ada ila sio mambo ya biashara"

Baada ya kuona mambo si shwali ilinilazimu kurudi tena chuoni kwa ngazi ya "bachelor degree "

Nilisoma na kumaliza, alijitahidi kunilipia sehemu ya ada yangu yote... (mwenyezi mungu ambariki sana)

Ndugu yangu nimeangaika sana kutafuta sehemu ya kujishikiza pasipo mafanikio yeyote yale, kila siku nimekuwa mtu wa kuamini uwenda bahati yangu yaja....ila giza kwangu naona linanizonga sasa..

Ndugu yangu poleni kwa maelezo marefu sana hapo juu

Naombeni msaada wenu wa kazi yeyote halali nipo tayari kuifanya kwa ajili ya kuhakikisha kampuni/taasisi/au mtu binafsi, usika inakuwa na kufikia kilele cha mafanikio tarajiwa

Mungu awabariki sana nyote

Napatikana Mbezi ya kimara, Dar es salaam

Phone no: 0755836347


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom