Tupiganie Katiba Mpya: Madaraka Matamu Wachonga Mzinga ni kama Wote

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,840
35,844
Amesikika Samia Suluhu Hassan akisema hatuna rais mwanamke. Akiendelea kasema rais mwanamke tutamweka 2025.

Amesema huyu tunayemwona sasa kaingia kwa kudra za Mola tu.

Ni wazi kuwa mheshimiwa huyu kesha nogewa kama mwonja asali vile. Tamaa yake iko sasa kwenye kuendelea kuwa rais 2025. Hii aliyonayo anazuga kuwa si mali kitu.

Katiba inabidi kuwa wazi: chaguzi ziwe huru, haki na zenye kuaminika. Achaguliwe mtu kwenye ushindani siyo kwenye ubakaji wa demokrasia.

Kesi ya Mbowe, makatazo kwenye mikutano ya siasa, kusimamisha uchumi kwanza, katiba si kipaumbele nk yote ni visingizio.

SSH ana nia ya kuendelea kubakia madarakani kwa namna yoyote. Mawazo yake muda wote yako kwenye post 2025 yeye kama rais huku akijua panapo ushindani wa haki hatoboi.

Ni wazi kuwa kwa miaka 4 hii kama chanjo za J&J zitatunusuru, tutaona mengi.

Anavutiwa na nia zozote za kususia chaguzi na hasa zile za 2024/25. Ni nia yake na wapambe wake kuwa chaguzi hizo zifanyike kwenye mazingira yale yale ya 2019/20. Lengo likiwa kukwiba kama mwendazake.

Kuhalalisha hayo anadai kila nchi ina demokrasia yake. Kwamba demokrasia siyo universal. Huyu bila katiba mpya, demokrasia kwa mara nyingine itabakwa!

2021 CCM tayari wana mgombea?Miaka 4 kabla?! Anaye tuhabarisha hayo ni mwali mwenyewe?!

Hiiiiii bagosha!

Kesha onja asali. Wala hofu ya Mola haipo tena. Kama mwendazake, naye anataka kuchonga mzinga.
 
🤣🤣🤣 huyu tuliyenaye ni Miss Utalii!

Huyo unayemwona miss kadhamiria kweri kweri:

1. Katiba mpya si kipaumbele
2. Mikutano ya vyama marufuku
3. Tayari 2021 kesha tangaza nia kwa ajili ya 2025
4. Status quo iliyomfanya mwendazake kubaka demokrasia huyu naye anapanga kuhakikisha ndiyo inayo endelea kuwapo
5. Mbowe yuko kizimbani kwa as long as they may decide kama tukiwapa fursa hiyo
6. Attention yetu hawataki iwe kwenye katiba mpya
7. Nk

Yapo mengi.

Tunapaswa kusimama imara. Tukio la leo kujaribu kuingilia mhimili wa mahakama na jinsi lilivyo suluhishwa na likatufumbue macho.

Bila kusimama imara we are in for it.
 
Amesikika Samia Suluhu Hassan akisema hatuna rais mwanamke. Akiendelea kasema rais mwanamke tutamweka 2025.

Amesema huyu tunayemwona sasa kaingia kwa kudra za Mola tu...
Chanjo ya j&j sii hatari Wala hatarishi,tutatoboa salama,shida ni hapa kwenye kunogewa,ukisha nogewa mawazo ni kupata zaidi,ili kunogewa kusikome.Katiba mpya ndio mwarobaini wa kweli.
 
Bi hangaya kwa jinsi anavyoonekana ni Mtu wa hasira sana.

Huyu Hadi 2025 anaweza kubwaga manyanga. Kama jiwe na ukatili wake kwenye kampeni alichemsha, huyu kazi anayo.

La sivyo ataanza kufunga watu na kutandika kila atayemkosoa.

Tusubiri muda
 
Chanjo ya j&j sii hatari Wala hatarishi,tutatoboa salama,shida ni hapa kwenye kunogewa,ukisha nogewa mawazo ni kupata zaidi,ili kunogewa kusikome.Katiba mpya ndio mwarobaini wa kweli.

Katiba mpya hatutakuwa na yeyote kama zawadi.

Bila mapambano leo mahakamani simu zisingekuwapo na watu wangezuiwa kuingia mahakamani kinyume cha katiba.

Ubakaji wa katiba wa namna yeyote hata kama unaendeshwa na mwanamke tusiukubali.
 
2025 mbali inaweza lolote kikabadilika naamini akiambiwa na msoga apumzike hawezi kukataa
 
Bi hangaya kwa jinsi anavyoonekana ni Mtu wa hasira Sana
Huyu Hadi 2025 anaweza kubwaga manyanga. Kama jiwe na ukatili wake kwenye kampeni alichemsha, huyu kazi anayo.
La sivyo ataanza kufunga watu na kutandika kila atayemkosoa
Tusubiri muda

Kubwaga manyanga? takuwa kusubiria dodo kwenye mnazi.

Katiba mpya anapanga kuileta after 2025 ili ajiachie legacy ya maana baada ya kuwa kajisimika 2025 - 2030.

Hayo ndiyo mahesabu yake.

Lion Chawene utakuwa umeshamsikia.
 
2025 mbali inaweza lolote kikabadilika naamini akiambiwa na msoga apumzike hawezi kukataa

Mbeba maono wenu huyo. Hukuona alivyong'aka na gazeti la Uhuru?

Huwaoni kina pole pole walivyo vunjika mioyo? Walikuwa na nafasi yote ya kushinikiza katiba mpya dhidi ya waonja asali.

Hawakuzitumia nafasi hizo na sasa leo wako kombania wakihanja hanja.
 
Kwa katiba kama yetu, DRC aliyetangazwa mshindi si aliyeshinda.

Hapa kwetu panapo fursa nini kinamzuia mtu kutangazwa kuwa mshindi hata kama hatokuwa ameshinda?
Kasome vizuri katiba ya DRC. Wanayo Mahakama ya katiba inayoingilia kati endapo atakuwepo mgombea ambaye hataridhika na matokeo.
 
Kasome vizuri katiba ya DRC. Wanayo Mahakama ya katiba inayoingilia kati endapo atakuwepo mgombea ambaye hataridhika na matokeo.

Fuatilia DRC:

Aliyeshinda uchaguzi si aliyetangazwa mshindi.

Ufahamu nini kilitokea kati ya Kabila na Tshisekedi dhidi Fayulu.
 
Kumbe kuendelea kuzuia kwake mikutano ya kisiasa ni mbinu mojawapo anayoitumia kujihami ili akigombea wapinzani wasiwe wamejinadi vizuri kwa wananchi.
 
Ukitaka kujua kama madaraka ni matamu muulize Mbowe. Alipopewa kijiti na Bob Makani aliikuta katiba ya chama hicho imekaa kidemokrasia demokrasia kama lilivyo jina la chama, na pia lengo la kuanzishwa kwake (chama cha "demokrasia" na maendeleo) jamaa alipoona amenogewa akaanza kubadilisha katiba ya kumfanya aendelee kutawala peke yake.

Akabandua kile kipengele cha ukomo wa madaraka ambacho kilikuwa kinamruhusu mwenyekiti wa chama hicho kukaa madarakan kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Pamoja na kufanikiwa kujiwekea umiliki wa kutawala chama hicho milele, na kuweka genge lake la kumlinda lkn bado alimtishia yoyote aliejaribu ku challenge kiti chake kama vile kina Chacha Wangwe, Zito, Sumaye nk.

Hii inaonesha hata tukibadilisha katiba leo, kesho akifanikiwa kushinda uraisi basi atakuja na mbinu nyingine ya kubadili katiba ya nchi ili aendelee kututawala watanzania, na hizi gharama tutazofanya sasa hivi za kubadili katiba zitakuwa zimekwenda na maji.

images (25).jpeg
 
Kama wewe si Kingai haiyumkiniki mkawa na undugu:

IMG_20210916_195226_185.jpg


Ushauri wa bure Mbowe mmzowee Tuna mpango wa kumpa mi 10 mingine.
 
Back
Top Bottom