Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,014
- 9,883
Dar es Salaam, Agosti 22, 2023
Abdulrahman Omari Kinana, mwanasiasa maarufu nchini Tanzania ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki kuanzia mwaka 2001 hadi 2006, ametoa maoni yake kuhusu maendeleo ya demokrasia nchini humo. Akizungumza na katika mkutano wa wadau wa demokrasia nchini leo mjini Dar es Salaam, Kinana ameelezea jinsi demokrasia imekua na mwelekeo unaovutia.
Akiwa amegusia mabadiliko ya miaka iliyopita, Kinana amesema, 'Ukiniuliza kama demokrasia imekuwa, nitasema ukifananisha na miaka kadhaa iliyopita demokrasia imekua.' Ameangazia hasa mabadiliko katika uwakilishi wa wananchi katika bunge lao. Amekiri kuwa ingawa kuna changamoto katika sheria na usimamizi wa uchaguzi, hatua zimechukuliwa kuimarisha haki za kisiasa.
Akizungumza kuhusu uhuru wa kujieleza nchini, Kinana amesema, "Uhuru wa kusema upo lakini kila uhuru una mipaka yake. Uhuru bila nidhamu ni wendawazimu, nidhamu bila uhuru ni utumwa." Amesititiza umuhimu wa kudumisha usawa kati ya uhuru na wajibu wa kijamii.
Kuhusu mchakato wa kuunda katiba mpya, Kinana ametaja tume mbalimbali zilizoundwa ili kuandaa katiba hiyo mpya na kusema kuwa hatua kadhaa zimeshachukuliwa na nyingine bado zinaendelea. Kinana amemwelezea Rais Samia Suluhu Hassan kuwa amezungumza kwa uwazi kuhusu nia yake ya kuwa na katiba mpya. "Rais Samia ameshazungumza namna ambavyo serikali yake imejipanga kuwa na katiba," amesema Kinana. Ameeleza kuwa marekebisho ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa yatakuwa sehemu ya mchakato huo.
Katika mwaka 2024/25, Kinana anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na uchaguzi ambao utaendeshwa kwa uwazi na kuheshimu kanuni za demokrasia.