...hawa wajukuu zangu kwa nini wanakimbia nchi yao (Ethiopia)?
1. Wana mradi wa reli ya SGR mkubwa kuliko yote barani Afrika!...
2. Wana mradi mkubwa wa umeme.
3. Wana flyovers kibao zilizopo mjini Adis Ababa...
4. Wana shirika kubwa la ndege kuliko mashirika mengi barani Afrika!...
5. Haka ka 'airbus' kamoja tunakojivunia nako, wao wanazo 45, achilia mbali utitiri wa Boeing, Bombadier na ATR...
6. Wana mradi mkubwa wa umeme uitwao GRHEP ambao unazalisha karibu megawati 9,000. Mradi huo ni mkubwa karibu mara 5 ya mradi wetu tunaojisifia nao wa "Stiglers gorge" ambao utazalisha megawati 2,000 ukikamilika...
Ethiopia wa kwao ni 9,000MW.
7. Wana viwanja vya ndege vya kisasa zaidi ya 20 nchi nzima!...
Lakini kila siku watu wanatoroka nchini kwao kukimbilia ughaibuni.... Tunawapokea kila siku, hapa barani Ulaya, baada ya kuvuka bahari ya Mediterranean na wengine kupoteza maisha baharini humo!... Wengine wanazamia huko Sauzi, wanasafirishwa kwa magari ya mizigo... Wengine wanazamishwa kwenye magunia ya pumba, vichwa tu vinatokeza nje...Wengine wanasafirishwa pamoja na mifugo...
Lakini kwa nini mtu aache barabara za lami, flyover, madaraja, viwanja vizuri vya ndege, na akimbilie nje ya nchi na kukubali kusafirishwa pamoja na mifugo?...🤔
Jibu ni kwamba MAENDELEO YA VITU hayawezi kuwa muhimu kuliko MAENDELEO YA WATU!...
Ukijenga Flyover wakati mama anakufa kwa kukosa dawa hospitalini, means umethamini vitu kuliko watu... Ukijenga Terminal viwanja vya ndege hadi kijijini kwako wakati vijana hawana ajira na umezuia serikali kuajiri, means unathamini vitu kuliko watu!...
Ukijenga bwawa la umeme wakati hujapandisha mishahara ya watumishi kwa miaka mitano, means unathamini vitu kuliko watu...
Ukijenga reli wakati wakulima wa korosho na mbaazi wanahangaika kupata soko, means unathamini vitu kuliko watu na hapo utakuwa ni KIONGOZI MPUMBAVU!...
Sijasema tusijenge reli, wala flyover!... Tujenge lakini tuwe na vipaumbele... Kuna faida gani kujenga reli kama kuna mama kule Namtumbo anakufa kwa kukosa dawa ya bei rahisi tu?...🤔
Kuna faida gani kununua ndege kama kuna watu wanakunywa maji machafu kule Lindi na Kigoma, ambayo wanayatafuta kilomita 20 kutoka walipo?...🤔
Ni baba mpumbavu na MWENDAWAZIMU pekee, anayeweza kusifiwa kwa kumnunulia mkewe Iphone 11, lakini aliacha mwanae akafa kwa kukosa laki moja ya matibabu!...
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8[1](a) inasema "Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa (wananchi) WATU sio ustawi wa VITU!... Asomaye na afahamu!...
👋🏾
Nimeikopi mahali