Tembea uone, ni Ubungo Interchange uzuri na ubaya wa maendeleo

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Leo nimeamua kutembea kwa miguu kushuhudia yale watu waliyokuwa wanayasema hapa JF

Nimeamua kutembea kama sehemu ya mazoezi baada ya kuona nimeongezeka zaidi kilo 10 tofauti na urefu wangu baada ya ushindi wa kishindo November 2020.

Safari yangu ilianzia Mlimani City kwa miguu nikitembea kuelekea ubungo Interchage mapaka Riverside.

Nikatoka Riverside mpaka Kibo kituoni kwa miguu, Nimepita pembeni ya kanisa la Askofu Gwajima nimeshuhudia waumini wakiangalia mahubiri ya Gwajima mchungaji kupitia television na idadi ya watu na magari hapo kanisani imepungua sana sana,Sijajua sababu lakini nikaendelea na safari zangu.

Yafuatayo ndio niliyoyaona kwa upande wa ubaya.

Hakuna kituo chochote cha mabasi kwa ajili ya raia wanaoishi kati ya ubungo interchange na kibo, Hawa watu asubuhi wakiamua kupanda magari ukiacha mwendokasi wanapanda sehemu gani, Mimi leo niliona kama sehemu ya mazoezi baada ya kilo zangu kuongezeka nimeamua kuzipunguza

Pili, Biashara za wamachinga zimeanza taratibu kushamiri hasa pale kwenye daraja kutoka ubungo interchange kuelekea Riverside hii inapelekea hatari kwa wapita kwa miguu kugongwa na magari, Leo hakuna purukushani kabisa, Je siku mji unapochanganya watu wanatembea kwa style gani eneo hilo kukwepa biashara za machinga na magari.

Mazuri niliyoyashuhudia,Ni mazuri kutokana sijafika eneo hili la ubungo kwa zaidi ya miaka kumi na moja sasa ,Hivyo kila kitu niliona kimebadilika na kinapendeza sana.

Mosi, Magari yanakwenda kwa spidi nzuri na ya haraka hakuna foleni kwa magari yanayotoka kimara kuelekea Posta na hakuna foleni kwa magari yanayotoka mwenge kuelekea Riverside kwa njia ya juu.

Pili, Mji umependeza sana sana unaweza ukahisi upo Califonia kumbe tupo mji wa wazaramo na wavuvi wa kimakonde.

Tatu, Wataalamu wanaendelea kutoka mchanga kwenye mifereji ya chini yaani ile underground drainage system baada ya mvua, Je watakapokabidhi mradi hili zoezi la watu kuingia kwenye hiyo mifereji na kutoa mchanga litaendelea au ndio itaziba na kusababisha dhahama

Naungana na Mwana JF Johnthebaptist kuwa kuna upepo mwanana na mzuri chini ya hilo daraja, Hatari iliyopo mbeleni ni mateja kugeuza vichaka vya ukabaji ni muhimu mamlaka kuangalia eneo hilo.

Nawapongeza watu mnaoishi Dar es Salaam hasa eneo la ubungo kwa kukubali kubomoa nyumba zenu ili kuimarisha miundo mbinu kwa manufaa ya uma, Dar es Salaam ya sasa sio ile ya miaka kumi na moja iliyopita.
 
Je ni kwanini kwa Gwajima Magari yamepungua? Je waumini wameamua kufanya mazoezi ili kupunguza uzito kama wewe?
Mkuu sijajua sababu, Mazoezi yataka moyo na kujituma, usipokuwa makini unaweza ukajikuta huwezi kuvaa viatu na kufunga kamba mpaka ukae chini au uchuchumae

Hao waumini labda watakuwa wamehamia kwa Mwamposa huko kawe

Chezea kitambi

Maendeleo ya kitambi siyaungi mkono hata kwa miaka miwili tena nakataa
 
Wanabodi, Leo nimeamua kutembea kwa miguu kushuhudia yale watu waliyokuwa wanayasema hapa JF

Nimeamua kutembea kama sehemu ya mazoezi baada ya kuona nimeongezeka zaidi kilo 10 tofauti na urefu wangu baada ya ushindi wa kishindo November 2020....

Haya ni madaraja ya kawaida tuache ushamba wakati mwingine. Unasema California unajua kuna madaraja mangapi kama hayo ni kwa maelfu hata south na Kenya wana madaraja sasa ni mambo ya kawaida sana
 
Haya ni madaraja ya kawaida tuache ushamba wakati mwingine. Unasema California unajua kuna madaraja mangapi kama hayo ni kwa maelfu hata south na Kenya wana madaraja sasa ni mambo ya kawaida sana
Mmha
 
Waombe Mods warekebishe kichwa cha habari neno Ubunge lisomeke Ubungo .
Naona una haraka sana kesho unarudi chatto unawahi kukata ticket.
 
Back
Top Bottom