Uchaguzi 2020 Kagera: Yaliyojiri mkutano wa Tundu Lissu kusaka Urais wa Tanzania 2020-2025

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,499
51,092
Katika lile tulilojua toka mwaka 2017, mkoa wa Kagera una lake jambo juu ya CCM na Rais Magufuli.

Ni mkoa ambao ulipata tetemeko, watu wakahitaji faraja kutoka kwa mfariji mkuu wakaishia kuambulia maneno ya kukereketa na kejeli.

Wana Kagera walipoomba Chakula wakaambiwa serikali haina shamba.
Walipoomba msaada wakaambiwa kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko?
Kisha wakaishiwa kukejeliwa kuwa kwani huo mkoa una nini, Ukimwi kwao, Tena kuna mto ngono na kijiji kinachoitwa Katerero (yote hii kumaanisha kuwa ni watu wapowapo tu wanaopenda chini).

Sasa kaenda kule mtetezi wa Wanyonge Tundu Lissu, mapokezi aliyoyapata katika vitongoji vya huko ni makubwa ajabu.

Lissu alianzia Nyakanazi, akaja Ngara akaenda Kyerwa.
Kwa kweli mapokezi aliyoyapata huko utadhani ni Jenerali wa Kijeshi aliyeongoza mapambano ya kukomboa maeneo hayo.

Hii ni rasharasha tu bado hajaingia Bukoba mjini.

Kiufupi, kwenye mkoa wa Kagera, CCM hawana chao. Wahaya hawapendi dharau!
Hapa chini ni mapokezi ya Lissu huko Kyerwa!


Tundu Lissu akiwa Karagwe

Wakati wa Ukoloni nchi hii ilikuwa imegawanywa katika majimbo 8 na nyie wa Karagwe jimbo lilikuwa linaitwa 'Jimbo la Ziwa', hayo yalikuwa majimbo ya kikoloni na yote yalikuwa yanatawaliwa na watu wanaitwa wakuu wa majimbo"- Tundu Lissu.

Wakuu wa majimbo na wakuu wa Wilaya walikuwa wanateuliwa na Gavana wa kikoloni, kwa hiyo Gavana aliyekuwa Dar es Salaam ndiye aliyekuwa anaamua nani awe mkuu wa jimbo la Ziwa na anaamua nani awe mkuu wa Wilaya moja wapo ya wilaya za zamani kabisa

Tulipopata Uhuru mwaka 61 mwaka uliofuata, sheria ikapitishwa na bunge la Tanganyika, sheria ya Mikoa na Ya Wakuu wa Mikoa, ile sheria iliondoa yale majimbo ikayagawanya majimbo yale kuwa hiki tunachokiita leo mikoa"

Tunataka maamuzi ya Ardhi ya Karagwe, yafanywe na watu wa Karagwe, sio wageni tunataka mambo yanayotuhusu wananchi wa Karagwe, Singida, Dodoma au Chato, wafanye wananchi wenyewe, ndio maana ya utawala wa Majimbo tunaouzungumzia

Sisi pekee ndio nchi yenye mikoa ambayo wakuu wake wanateuliwa na Rais, ukienda Kenya wameacha kuita Majimbo walikuwa na majimbo wakati wa MOI, siku hizi kuna Kaunti zina Gavana, Gavana wa Kaunti ya Kenya anachaguliwa na wananchi wa hiyo kaunti na anaondolewa nao

Mamlaka ya kuendesha mambo yote katika Kaunti, Elimu, Maji, Barabara yanafanywa kwenye 'Level' hiyo na viongozi waliochaguliwa, ndivyo ilivyo Afrika Kusini, Zambia, Marekani, Uingereza, Ujerumani, ndivyo ilivyo nchi zote ambazo zinataka wananchi wawe na mamlaka

Huu utaratibu wa kukopa wakulima wa Kahawa wa Karagwe, na wa nchi nzima huu ni utaratibu ambao unafanya wanachi wanakuwa masikini

Leo ukilima Kahawa yako, unahangaika mwenyewe, mbegu mwenyewe, upalilie mwenyewe, madawa mwenyewe, uvune mwenyewe, ukishaweka kwenye magunia unaambiwa huwezi kuuza mahali popote isipokuwa AMCOS

=====
"Maelfu ya wananchi wa Karagwe wamefurika kwenye viwanja vya Kayanga kumshuhudia Mgombea Uraisi Mheshimiwaa Tundu Lissu kwenye mkutano wa kuomba kura kwa ajili uchaguzi mkuu 2020.

Mheshimiwaa Tundu Lissu akiutubia maelfu ya wananchi wa Karagwe amesema nao haya machache..

Katika siku Nimelala vizuri toka nimeanza Kampeni ni hapa, Nimefika sehemu ambayo watu wake Wanapenda haki. Nafarijika sana na mapokezi yenu hasa mapokezi Ya rafiki yangu na mlezi kiimani Askofu Ben Bagonza. ' Ahsanteni sana watu wa Karagwe.

Kabla sijaanza kuongea mambo ya Karagwe naomba niseme mambo mawili Ya Utangulizi...

1. Magufuli amesema sisi tunaotaka kutawala nchi kwa majimbo tunataka kuigawa nchi vipande vipande sasa acha nitoe Ufafanuzi. Kipindi cha Ukoloni huku Kote kulikuwa na majimbo yakikoloni na majimbo yote yalikuwa yanaongozwa Na wakuu wamajimbo na wakuu wawilaya. Lakini tulipopata uhuru ukaleta Sheria yakuleta mikoa na majimbo yakagawanywa kuwa mikoa, namikoa ikawekwa chini ya wakuu wamikoa ambao ni wateule wa raisi, Hoja sasa nikuwa wakati wa Ukoloni majimbo hayakutoa mamlaka kwa wananchi na hata mikoa pia haikutoa mamlaka kwa wananchi. Chadema inapozungumzia utawala wa majimbo kuwa inataka kuhamisha Mamlamka ya raisi kwenda kwa wananchi, Wananchi Zaidi Ya miaka 60 hawana mamlaka, sasa lazima tuyarudishe kwa wananchi. Kwa Mfano halisi ni huyu mkuu wa wilaya wenu.... ametapeli mashamba ya Kahawa, amekamatwa akichukua rushwa lakini hakuna wakumuondoa. Sasa tunaposema utawala wa majimbo, maamuzi ya watu Karagwe yaamuliwe na watu wa Karagwe wenyewe. Tujiamulie wenyewe nahii ndo maana ya Majimbo, tunataka mamlaka Yakuendesha Karagwe yaamuliwe na watu wa Karagwe. Nilitaka nifafanue hili ambalo Magufuli Aelewee.

2. Magufuli jana amesema kuwa Vitambulisho vya Machinga sio lazima, sasa Magufuli ameshalegea. Tangu tumeanza shughuli hii mimi nimesema kuwa baada ya tarehe 28 nitaondoa vitambulisho vya machinga. Sasa kwakuwa ameshalegea basi namwambia hvyo vitambulisho viliwekewa sheria iliyotungwa nA waziri wafedha, basi sasa namwambia Magufuli kesho afute ile sheria na kama hata fanya hvyo ni janja Janja.

Hoja Za Kagera..

1. Karagwe ni wakulima wa kahawa, Miaka Mitano ya Magufuli imezodoresha kukua kwa zao La Kahawa. Nashinda kubwa ni kwa KBCU ( chama cha ushirika wa kahawa). Mmekuwa mkila kahawa wenyewe lakini mkivuna tu mnakopwa, Magufuli Alisema Kuwa ataondoa kodi 27 za Kahawa lakini mpaka leo Hakuna. Serikali Ya Magufuli imekuwa ikiwakopa Wakulima kwakuwapa makaratasi. Utaratibu Huu wakuwalazimisha wakulima Kuuza Kahawa kwa vyama vya ushirika vinavyomilikiwa na MaCCM. Sasa Sisi Serikali Ya Chadema tutaleta Kanda maalum ya kiuchumi na Biashara kwa mikoa ya mpakani ili kuwawezesha wafanyabiashara Kuuza mazao yao kwa bei zinazolipa nakuwapa faida. Tutawaruhusu Kuuza Kahawa nje ya nchi kwa bei inayolipa. Hii ndomaana yakuweka Kanda maalum ya kiuchumi na Kibiashara.

Mvua kubwa saaaaana imekatisha, sasa tunaelekea Missenyi, Nkenge, Bunazi, mkutano wa pili kwa siku ya leo.

Picha za Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu uliofanyika leo Septemba 22, 2020, katika Uwanja wa Kayanga, Karagwe.

1. Mhe. Tundu Lissu akihutubia maelfu ya wananchi wa Karagwe, katika Uwanja wa Kayanga leo Jumanne, Septemba 22, 2020.

2. Mhe. Tundu Lissu akifurahia jambo na rafiki yake na mlezi wake kiimani wa muda mrefu, Baba Askofu Benson Kalikawe Bagonza, ambaye alifika kwenye mkutano huo kutoa salaam.

1600782776542.png

1600782316649.png
1600782328990.png
1600782344869.png
1600782357802.png
1600782377882.png
1600782395216.png
1600782415246.png
1600782435104.png
1600782448533.png
1600782465487.png
1600782492335.png
 
Wana Kagera walipoomba Chakula wakaambiwa serikali haina shamba

Walipoomba msaada wakaambiwa kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko?

Kisha wakaishiwa kukejeliwa kuwa kwani huo mkoa una nini, Ukimwi kwao, Tena kuna mto ngono na kijiji kinachoitwa katerero (yote hii kumaanisha kuwa ni watu wapowapo tu wanaopenda chini)
 
Kisha wakaishiwa kukejeliwa kuwa kwani huo mkoa una nini, Ukimwi kwao, Tena kuna mto ngono na kijiji kinachoitwa Katerero (yote hii kumaanisha kuwa ni watu wapowapo tu wanaopenda chini).

Ila jamani tuache masikhara, Wahaya wanapenda sana KUDINYANA aisee. Kwenye eneo hilo, Wahaya . Najua mshkaji wangu Maxence Melo anaweza kuniadhibu ila Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, nami nimechagua kuwa Mpenzi wa Mungu
 
Naona muna farijiana hapo.
Tanzania, upinzani bado haujawa na nguvu hiyo munayo aminishana.
Itachukua miaka 50 kuitoa CCM madarakani.
 
Katika lile tulilojua toka mwaka 2017, mkoa wa Kagera una lake jambo juu ya CCM na Rais Magufuli.

Ni mkoa ambao ulipata tetemeko, watu wakahitaji faraja kutoka kwa mfariji mkuu wakaishia kuambulia maneno ya kukereketa na kejeli.

Wana Kagera walipoomba Chakula wakaambiwa serikali haina shamba.

Walipoomba msaada wakaambiwa kwani serikali ndiyo iliyoleta tetemeko?

Kisha wakaishiwa kukejeliwa kuwa kwani huo mkoa una nini, Ukimwi kwao, Tena kuna mto ngono na kijiji kinachoitwa Katerero (yote hii kumaanisha kuwa ni watu wapowapo tu wanaopenda chini).

Sasa kaenda kule mtetezi wa Wanyonge Tundu Lissu, mapokezi aliyoyapata katika vitongoji vya huko ni makubwa ajabu.

Lissu alianzia Nyakanazi, akaja Ngara akaenda Kyerwa.

Kwa kweli mapokezi aliyoyapata huko utadhani ni Jenerali wa Kijeshi aliyeongoza mapambano ya kukomboa maeneo hayo.

Hii ni rasharasha tu bado hajaingia Bukoba mjini.

Kiufupi, kwenye mkoa wa Kagera, CCM hawana chao. Wahaya hawapendi dharau!

Hapa chini ni mapokezi ya Lissu huko Kyerwa!

View attachment 1576849
Wengi hapo ni wapenzi watazamaji
 
Endelea kujifariji tu.
Nadhani unajua kuwa upinzani ni kikundi cha maigizo tu kama Fukuto.
Hata mimi nilisha jitoaga ufaham 2005, kuwashabikia hao wasaka Ruzuku ya vyama vyao, lakini baada ya ufaham kunirudia, nimeona ningoje kwanza miaka 50 ijayo ndio nifikirie kuwashabikia hao wasaka tonge.
We endelea kuloga tu ndugu zako uwamwekuemwekue tu...hii ishu imekuzid kimo
 
Aiseeeeee!
Ninachokiona hapo ni "mahaba" yaliyopindukia.
Huo umati si mchezo kwa kweli.
Nimeona clip ya JPM akiwa Tabora leo asubuhi hii,amepaniki balaa.
Yule mzee napendekeza kama anapenda kuendelea kuwa hai,ajitoe tuu kwenye kampeni au asifuatilie kabisa kampeni za Mh. Lissu.
Nimemsikia akisema ilani ya CHADEMA imeandikwa kuwa madini na yatawekwa dhamana,maliasili zetu zitawekwa dhamana na mwisho wa siku hata sisi tunaweza kuwekwa dhamana.
Kweli baba wa uongo ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom