Ujenzi wa daraja la juu la Jangwani kuokoa muda na fedha za wakazi wa wilaya mbili za Kinondoni na Ubungo

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
UJENZI WA DARAJA LA JUU LA JANGWANI,KUOKOA MUDA NA FEDHA ZA WAKAZI WA WILAYA MBILI,KINONDONI NA UBUNGO.

Leo 11:25hrs 15/11/2020

Daraja la juu la Jangwani lisasaidia kuepuka kutembea kwa miguu toka Kariakoo hadi Buguruni au toka Kariakoo,Muhimbili hadi Morocco,kuepuka kukaa foleni masaa matano,na ukishangaa unaweza kufika nyumbani kwako saa nane usiku,sisi watu Kariakoo kutembea kwa mguu tunaita Azimio la Arusha,sijui ninyi watu wa Posta,Jangwani pakifungwa tu,kila mtu Kariakoo anajua leo moja moja Azimio la Arusha,tutatembea kwa mguu toka Kariakoo hadi Buguruni, Kariakoo Kigogo hadi Magomeni, Kariakoo hadi Mwenge ndio upate gari wakati huo foleni itakuwa imepungua,Boda boda watakwambia shilingi 15,000 hadi 20,000 ,Daraja la Flyover la Jangwani litaokoa muda na fedha,na Serikali itapata kodi na mapato yake kama watu watawahi kwenye biashara zao na wafanyakazi kuwahi makazini,

Unapomchelewa mteja,unakosa hela,unakosa kuuza bidhaa yako,mteja awe ametoka Congo,Zambia,Malawi,Rwanda,Burundi au awe Mtanzania,tayari utakuwa umempoteza mteja,mauzo hayaingii kwenye kitabu kama utamchelewa mteja aliyekusibiri dukani kwako Kariakoo kwa masaa matano wewe ukiwa njiani kutokea Kimara,Mzunguko wa masaa matano baada ya kufunga duka lako Kariakoo kurudi Kinondoni kupitia Kigogo kwa sababu Jangwani pamefungwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi gari haziendi kwenye foleni utakuongezea gharama za mafuta hata pale utapoamua upite bar ule chakula cha elfu kumi wakati nyumbani ungekula bure na kusave elfu kumi,hapa nawazungumzia watu Milioni tatu wanaotumia daraja la Jangwani kutoka au kuelekea Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Kinondoni,hizi ndizo gharama ambazo tutaokoa kama daraja la juu flyover itajengwa pale Jangwani.

Wilaya ya Kinondoni ni moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam,na kwa lugha nyingine ni manispaa ndani ya jiji la Dar es Salaam ambayo robo tatu ya wakazi wake wanapita daraja la Jangwani kila asubuhi na kila jioni,hapa nazungumzia jumla ya watu Milioni moja na nusu (1,500,000) Kinondoni ipo kaskazini ya jiji la Dar es Salaam, Kinondoni ndio yenye pwani inayoanzia Selander bridge na kuendelea kupitia rasi ya Msasani, Kunduchi hadi Mbweni, Kinondoni ndio Wilaya na Manispaa yenye hoteli nyingi za kitalii zilizopo sehemu hizo nilizozitaja.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina kilometa za eneo 260.40, kutokana na Sensa ya watu mwaka 2012 Manispaa ina jumla ya watu 845,368 ambapo wanaume ni 409,149 na wanawake 436,219 lakini kwa makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2016 Halmashauri ya Manispaa ina jumla ya watu 1,031,349 ambapo wanaume ni 499,161 na wanawake 532,188.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepakana na Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusini mashariki na Halmashuri ya wilaya ya Kisarawe upande wa magharibi. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeunganishwa na Barabara nzuri na njia zingine za mawasiliano katika Jiji la Dar es Salaam na sehemu zingine za nchi . Barabara kuu zinazounganisha Halmashauri ni Barabara ya Morogoro, Barabara ya Mandela, na Barabara ya Sam Njoma.

Ubungo inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani,Maelfu ya Wafanyabiashara kutoka kusini,kaskazini, Mashariki na Magharibi ya jiji la Dar es Salaam wanatumia kituo kikubwa cha Usafiri wa mabadi ya Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi,Kituo cha mabasi cha Mbezi kimeungana na baadhi ya vituo vikubwa vya miji mbalimbali ya Tanzania kama vile cha Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

-Wananchi ushuka kwenye Mwendokasi na kupita kwenye matope,kama greda limechelewa kuondoa matope yanayofikia magotini,

Chanzo cha Mto Msimbazi unafurika Jangwani kinapatikana katika vilima vya Pugu, upande wa kaskazini wa Kisarawe,Mvua ikinyesha Kisarawe hata isiponyesha Dar basi Jangwani panafungwa,Njia yake ni km 42.5 hadi mdomo wake kwenye daraja la Selander ambalo linaingiza mto huo baharini,Mto Msimbazi unapitia eneo lote la Dar es Salaam ikiwa ni mto mkuu wa jiji hili. Mafuriko yake yanaathiri maisha ya watu wengi mara kwa mara.

Mto huo una viwango vikubwa vya uchafu, hasa kutokana na kuwepo kwa metali nzito zinazotokana na viwanda na ambazo ni sumu; sumu nyingine zinazidi kutoka kwenye majalala ya takataka ya Vingunguti zikipelekwa na maji ya mvua mtoni,Machinjio makubwa kando ya mto yanaongeza uchafuzi. Vyanzo vingine ni vyoo vya shimo vinavyotumiwa na idadi kubwa ya wakazi,Bonde la mto ambalo ni kavu sehemu kubwa ya mwaka ni sehemu ya kumwaga takataka kwa wakazi wa karibu.

Shughuli za kilimo huongeza tatizo kwa kutumia samadi na mbolea za chumvi. Maji ya mto Msimbazi hayafai kwa matumizi ya binadamu hata hayafai kwa matumizi ya kilimo cha mazao,Mboga za majani kutoka bustani mbalimbali za bonde la Msimbazi, vile vile kupita kwa miguu wakati wa matope baada ya maji kuisha kunaweza kusababisha mtu kukatwa na chupa zinazojisaga wakati greda likitoa matope hayo,vile vile kujichoma na vyuma hata kuweza kusababisha kansa.

Nimalizie kwa kusema,Daraja la Jangwani ndilo linalotenganisha wilaya mbili kwa upande huu wa Kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam,Daraja la Jangwani linatenganisha wilaya ya Kinondoni na Ilala lilipo soko la Kariakoo na pia Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Ilala,tukumbuke Wafanyabiashara wote wanaotoka Soko la Kariakoo,katika Wilaya ya Ilala wanapita Jangwani kuja Wilaya ya Ubungo kwa ajili ya Safari zao mikoani na nje ya nchi,Ningekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,kila siku asubuhi na jioni mvua ikinyesha ningekuwa maeneo yale,kuhakikisha yale magreda yanaondoa tope kwa haraka sana ili njia ifunguliwe kuepusha usumbufu kwa Wananchi ambao wengi wanachukua hatua ya kuvua viatu na kupita kwenye matope kuepuka gharama ya kuvushwa na pikipiki kwa shilingi 10,000 kubebwa kwa shilingi 5,000 au kutumia masaa manne kuzunguka Kigogo au Salenda

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Watanzania wamekuwa kama yatima, mnapelekwa mzobemzobe tu. Poleni sana.

Wengine tumebaki watanzania kimwili tu ila kiroho na kiakili tulishahama zamani.

Pale Mwenge wanatifuatifua sijui vitu gani visivyoisha wakati kuna mpango wa kujenga flyover au sijui mdudu gani pale pale. Kwa hiyo wakimaliza haitakaa muda, ujenzi upya utarudi tena.
 
Nilisoma sehemu kuwa Dar es salaam ina wakazi million 4, wewe umesema wanaopita hapo ni million 3,so unamaanisha wanaobaki dar yote ni kiduchu tu yaani million 1 tu wengine wote ni kupita jangwani
emoji848.png
emoji848.png

Nirekebishe kama sijakupata vizuri kwenye hizo takwimu zako.
 
Nadhani hatuna vipaumbele,tunajenga daraja kuvuka bahari ambalo halina msaada ukilinganisha na barabara ya lango la jiji........
 
Watanzania wamekuwa kama yatima, mnapelekwa mzobemzobe tu. Poleni sana.

Wengine tumebaki watanzania kimwili tu ila kiroho na kiakili tulishahama zamani.

Pale Mwenge wanatifuatifua sijui vitu gani visivyoisha wakati kuna mpango wa kujenga flyover au sijui mdudu gani pale pale. Kwa hiyo wakimaliza haitakaa muda, ujenzi upya utarudi tena.
Bajeti inayopitishwa na bunge dhaifu (sasa NEC B ya CCM) sijui inaheshimiwa vipi maana kila kukicha kinachotekelezwa na miradi inayoamriwa na Mhutu. Haijapitishwa na bunge lolote. Labda Mwanamke mweupe mtoa stress anashirikishwa huko magogoni.
 
Nilisoma sehemu kuwa Dar es salaam ina wakazi million 4, wewe umesema wanaopita hapo ni million 3,so unamaanisha wanaobaki dar yote ni kiduchu tu yaani million 1 tu wengine wote ni kupita jangwani
Nirekebishe kama sijakupata vizuri kwenye hizo takwimu zako.
Dar kwa sasa ina Wakazi Milioni 7,nenda kasome tena hiyo Sehemu uliyosoma.
 
Watanzania wamekuwa kama yatima, mnapelekwa mzobemzobe tu. Poleni sana.

Wengine tumebaki watanzania kimwili tu ila kiroho na kiakili tulishahama zamani.

Pale Mwenge wanatifuatifua sijui vitu gani visivyoisha wakati kuna mpango wa kujenga flyover au sijui mdudu gani pale pale. Kwa hiyo wakimaliza haitakaa muda, ujenzi upya utarudi tena.
Mwenge na Ubungo huwa panajengwa toka mwaka 2010, sijajua mpaka sasa zilishatumika fedha kiasi gani kujenga na kubomoa hizo junction
 
Hakuna sehemu iliyojaa watu wajinga kama clserikali ya sasa pale jangwani hakukuruhusiwa watu kujenga lakini walipoiachia brt kujenga tumeona matokeo yake
 
UJENZI WA DARAJA LA JUU LA JANGWANI,KUOKOA MUDA NA FEDHA ZA WAKAZI WA WILAYA MBILI,KINONDONI NA UBUNGO.

Leo 11:25hrs 15/11/2020

Daraja la juu la Jangwani lisasaidia kuepuka kutembea kwa miguu toka Kariakoo hadi Buguruni au toka Kariakoo,Muhimbili hadi Morocco,kuepuka kukaa foleni masaa matano,na ukishangaa unaweza kufika nyumbani kwako saa nane usiku,sisi watu Kariakoo kutembea kwa mguu tunaita Azimio la Arusha,sijui ninyi watu wa Posta,Jangwani pakifungwa tu,kila mtu Kariakoo anajua leo moja moja Azimio la Arusha,tutatembea kwa mguu toka Kariakoo hadi Buguruni, Kariakoo Kigogo hadi Magomeni, Kariakoo hadi Mwenge ndio upate gari wakati huo foleni itakuwa imepungua,Boda boda watakwambia shilingi 15,000 hadi 20,000 ,Daraja la Flyover la Jangwani litaokoa muda na fedha,na Serikali itapata kodi na mapato yake kama watu watawahi kwenye biashara zao na wafanyakazi kuwahi makazini,

Unapomchelewa mteja,unakosa hela,unakosa kuuza bidhaa yako,mteja awe ametoka Congo,Zambia,Malawi,Rwanda,Burundi au awe Mtanzania,tayari utakuwa umempoteza mteja,mauzo hayaingii kwenye kitabu kama utamchelewa mteja aliyekusibiri dukani kwako Kariakoo kwa masaa matano wewe ukiwa njiani kutokea Kimara,Mzunguko wa masaa matano baada ya kufunga duka lako Kariakoo kurudi Kinondoni kupitia Kigogo kwa sababu Jangwani pamefungwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi gari haziendi kwenye foleni utakuongezea gharama za mafuta hata pale utapoamua upite bar ule chakula cha elfu kumi wakati nyumbani ungekula bure na kusave elfu kumi,hapa nawazungumzia watu Milioni tatu wanaotumia daraja la Jangwani kutoka au kuelekea Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Kinondoni,hizi ndizo gharama ambazo tutaokoa kama daraja la juu flyover itajengwa pale Jangwani.

Wilaya ya Kinondoni ni moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam,na kwa lugha nyingine ni manispaa ndani ya jiji la Dar es Salaam ambayo robo tatu ya wakazi wake wanapita daraja la Jangwani kila asubuhi na kila jioni,hapa nazungumzia jumla ya watu Milioni moja na nusu (1,500,000) Kinondoni ipo kaskazini ya jiji la Dar es Salaam, Kinondoni ndio yenye pwani inayoanzia Selander bridge na kuendelea kupitia rasi ya Msasani, Kunduchi hadi Mbweni, Kinondoni ndio Wilaya na Manispaa yenye hoteli nyingi za kitalii zilizopo sehemu hizo nilizozitaja.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ina kilometa za eneo 260.40, kutokana na Sensa ya watu mwaka 2012 Manispaa ina jumla ya watu 845,368 ambapo wanaume ni 409,149 na wanawake 436,219 lakini kwa makadirio ya idadi ya watu ya mwaka 2016 Halmashauri ya Manispaa ina jumla ya watu 1,031,349 ambapo wanaume ni 499,161 na wanawake 532,188.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepakana na Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusini mashariki na Halmashuri ya wilaya ya Kisarawe upande wa magharibi. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeunganishwa na Barabara nzuri na njia zingine za mawasiliano katika Jiji la Dar es Salaam na sehemu zingine za nchi . Barabara kuu zinazounganisha Halmashauri ni Barabara ya Morogoro, Barabara ya Mandela, na Barabara ya Sam Njoma.

Ubungo inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani,Maelfu ya Wafanyabiashara kutoka kusini,kaskazini, Mashariki na Magharibi ya jiji la Dar es Salaam wanatumia kituo kikubwa cha Usafiri wa mabadi ya Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi,Kituo cha mabasi cha Mbezi kimeungana na baadhi ya vituo vikubwa vya miji mbalimbali ya Tanzania kama vile cha Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

-Wananchi ushuka kwenye Mwendokasi na kupita kwenye matope,kama greda limechelewa kuondoa matope yanayofikia magotini,

Chanzo cha Mto Msimbazi unafurika Jangwani kinapatikana katika vilima vya Pugu, upande wa kaskazini wa Kisarawe,Mvua ikinyesha Kisarawe hata isiponyesha Dar basi Jangwani panafungwa,Njia yake ni km 42.5 hadi mdomo wake kwenye daraja la Selander ambalo linaingiza mto huo baharini,Mto Msimbazi unapitia eneo lote la Dar es Salaam ikiwa ni mto mkuu wa jiji hili. Mafuriko yake yanaathiri maisha ya watu wengi mara kwa mara.

Mto huo una viwango vikubwa vya uchafu, hasa kutokana na kuwepo kwa metali nzito zinazotokana na viwanda na ambazo ni sumu; sumu nyingine zinazidi kutoka kwenye majalala ya takataka ya Vingunguti zikipelekwa na maji ya mvua mtoni,Machinjio makubwa kando ya mto yanaongeza uchafuzi. Vyanzo vingine ni vyoo vya shimo vinavyotumiwa na idadi kubwa ya wakazi,Bonde la mto ambalo ni kavu sehemu kubwa ya mwaka ni sehemu ya kumwaga takataka kwa wakazi wa karibu.

Shughuli za kilimo huongeza tatizo kwa kutumia samadi na mbolea za chumvi. Maji ya mto Msimbazi hayafai kwa matumizi ya binadamu hata hayafai kwa matumizi ya kilimo cha mazao,Mboga za majani kutoka bustani mbalimbali za bonde la Msimbazi, vile vile kupita kwa miguu wakati wa matope baada ya maji kuisha kunaweza kusababisha mtu kukatwa na chupa zinazojisaga wakati greda likitoa matope hayo,vile vile kujichoma na vyuma hata kuweza kusababisha kansa.

Nimalizie kwa kusema,Daraja la Jangwani ndilo linalotenganisha wilaya mbili kwa upande huu wa Kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam,Daraja la Jangwani linatenganisha wilaya ya Kinondoni na Ilala lilipo soko la Kariakoo na pia Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Ilala,tukumbuke Wafanyabiashara wote wanaotoka Soko la Kariakoo,katika Wilaya ya Ilala wanapita Jangwani kuja Wilaya ya Ubungo kwa ajili ya Safari zao mikoani na nje ya nchi,Ningekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,kila siku asubuhi na jioni mvua ikinyesha ningekuwa maeneo yale,kuhakikisha yale magreda yanaondoa tope kwa haraka sana ili njia ifunguliwe kuepusha usumbufu kwa Wananchi ambao wengi wanachukua hatua ya kuvua viatu na kupita kwenye matope kuepuka gharama ya kuvushwa na pikipiki kwa shilingi 10,000 kubebwa kwa shilingi 5,000 au kutumia masaa manne kuzunguka Kigogo au Salenda

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Suala la Jangwani kama watengeneze daraja au catchment areas na water ways ni vizuri likafanyiwa assessment na wataalamu wa miundo mbinu na kuona njia ipi iliyo bora .

Hata ikiwa kuondoa kituo cha Mwendo kasi
 
Back
Top Bottom