Amb. Kijazi Interchange, Mchina arudi kufanya usafi na ulinzi? Tz tumeshindwa?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Kuna usemi wa Kijaluo kwamba "Solution to One Problem Carries the Seeds for the Next Problem" yaani "ufumbuzi wa tatizo moja hubeba mbegu za kuotesha tatizo jingine, tafsiri isiyo rasmi"

Daraja-kavu la Amb. Kijazi Interchange katika Manispaa ya Ubungo jiji Dar es Salaam ambalo mwanzoni lilibezwa na kupewa msemo wa kijaluo kuelezea mradi usiowezekana "White Elephant Project" sasa baada ya kukamilika kwake na kuzinduliwa limepamba jiji la Dsm na kuwa alama ya jiji na kivutio cha utalii wa ndani mbali na kutatua tatizo la msongamano la eneo hilo linalokutanisha njia za ndani ya jiji na za kwenda mikoani hasa katika barabara kuu ya Tanzaniaone.

Nairobi ni jjiji la nne barani Afrika kwa msongamano wa magari unaosababishia Jamhuri ya Kenya hasara ya US $ 578,000, huku jiji la Dsm likipata hasara ya 411bl kwa mwaka (kabla ya daraja-kavu hilo kujengwa).

Hosea Mpogole wa Iringa University na Samira Msangi walifanya utafiti wa msongamano wa magari Dar es Salaam na madhara yake kwenye tija ya wafanyakazi mwaka 2016 na matokeo ya utafiti huo kuchapwa kwenye Jarida la "Journal of Sustainable Development" Hiki ndicho walichogundua:

"....study assesses traffic congestion in Dar es Salaam and particularly its implications for workers’ productivity. Travel time and productivity indexes were established from a sample of 96 workers who used public transport along Morogoro and Mandela Roads. Travel time index (TTI) is the ratio of the average travel time during peak period to the travel time during off-peak period. Findings reveal that TTI was 2.19. Workers spent about 2 times of the average commuting time to work and 3 times of the same commuting from work to their various residences. About 2.5 hours were lost on traffic jam per day and that people worked 1.4 times less than the required time due to traffic congestion. It was further established that in 10 working days, almost 3 days were lost to traffic congestion...."

Taifa limetatua tatizo la msongamano kwenye eneo hilo la kimkakati, lakini utatuzi huo umeotesha mbegu ya matatizo mengine ambayo kwa mila na desturi zetu yameachwa kwanza yasubiri kalamu na shajara za waandishi kuyang'amua japo yako waziwazi kwa kila mtu. Tatizo la msongamano limetambuka na kuleta matatizo mengine matatu mbali na lile lililotatuliwa la msongamano kama ifuatavyo:

Tatizo la pili, eneo la daraja-kavu la kimkakati limeanza kidogokidogo kuwa dampo la taka ngumu zinazozalishwa na wapita njia, abiria kwenye vyombo vya usafiri na chokoraa ambao wote hutupa hapo vifungashio vya bidhaa walizotumia na kufanya eneo kupoteza umaridadi wake na kulitangaza taifa na jiji la Dar kama maeneo machafu duniani. Je, taifa linahitaji kukopa fedha kwenye masoko ya mitaji na kurudisha mkandarasi wa Kichina kuja kufanya usafi pale?

Tatizo la tatu, chokoraa wanaostahili kuwepo shule kufaidi matunda ya elimu bure wamepafanya eneo hilo kuwa ndiyo makazi yao ya kudumu kwa kuwa wanafurahia upepo mwanana, kivuli na kujikinga mvua. Ni nyumba yao, ni maliwato yao isiyokuwa na matundu, ni dampo lao, na ni salama kwao kwasababu wako ndani ya uzio mkali wa waya wa seng'enge. Je, taifa linahitaji kukopa fedha kwenye masoko ya mitaji na kurudisha mkandarasi wa Kichina kuja kuwaondoa machokoraa pale?

Tatizo la nne, juu ya daraja-kavu kwenye njia ya Port-access na Mwenge (njia ya BRT) pamekuwa ni uwanja wa wafanya mazoezi ya viungo na waporaji ambao nao pia wanafanya hayo bila kuchukuwa tahadhari ya ajali inayoweza kuwakuta huko au hata wao wenyewe kuwasababishia ajali hizo watumiaji wa njia hiyo ambayo iko rasmi kwa vyombo vya moto vya usafiri tu na wala siyo watembea kwa miguu, wanyama, guta nk. Je, taifa linahitaji kukopa fedha kwenye masoko ya mitaji na kurudisha mkandarasi wa Kichina kuja kuwaondoa wakaidi hao pale?

Maswali magumu:

1. Tanroads wapo? Wana kitengo au kikosi cha ukaguzi?
2. Polisi wapo? Wana kikosi cha patrol?
3. Sumatra kama mdau wa usafiri wapo? Wana kitengo cha ukaguzi wa njia ambazo wateja wao wanapita?
4. Jiji la Dsm lipo? Lina Mgambo wa kutunza amani na mali za Jiji?
5. Manispaa ya Ubungo ipo? Ina Mgambo wa kutunza amani na mali zilizoko ndani ya Manispaa?
6. Je, baada ya uzinduzi wa mradi huo wa kimkakati, ulinzi na usalama wake viko kwenye mikono ya serikali au bado mradi uko kwenye uangalizi wa Mkandarasi kusubiri kuona ubora wake ndipo waukabidhi serikalini? Yaani bado uko kwenye warranty?
7. Je, nani ajuaye kama ulinzi imara hauhakikishwi pale kesho na keshokutwa tukaamka na kukuta seng'enge zile zimekatwa na kuuzwa kama vyuma chakavu? Tayari kwenye kuta za daraja la juu kabisa la Mwenge Bandarini kuna maandishi ya matusi yasiyovumilika kabisa. Kweli Mwafrika asipodoe ngozi apodoe ubongo wake ili abadalikie.

Ushauri:
1. Serikali itoe ulinzi wa mradi huo wa kimkakati kama unavyotoa ulinzi kwenye madaraja-maji makubwa nchini kama Kirumi Mara, Umoja Mtwara/Msumbiji, Mkapa Rufiji, Magufuli Kilombero, Kikwete Malagarasi, Nyerere Kigamboni nk.

2. Kama serikali haina walinzi wa kutosha, Tanroads na Sumatra waombe vibali serikalini ku-recruit, kufunza na kuajiri jeshi-usu (Auxilliary Police) kulinda mradi huo kama ambavyo UDSM, Mzumbe University, SUA, Ardhi University, TPA na Muhimbili National Hospital walivyoomba vibali kwa minajili hiyo na kuwa na kitengo chao cha ulinzi.

3. Tanroads na Sumatra kama ushauri namba 1 na 2 haviwezekani basi watanue bajeti zao zijazo ili watengewe fedha za kutosha waingie mkataba na SUMA JKT kutoa ulinzi wa maeneo hayo, pia Jeshi la Magereza linaanzisha kitengo cha ulinzi kama cha SUMA JKT.

NB.
Sidhani kama tuna sababu ya kusubiri mahayati Eng. Mfugale na Rais Magufuli kuja hata kwa njia ya ndoto kutufundisha kuona umuhimu wa kulinda mradi huo.

Mradi usipolindwa, unawezakuwa target ya uhalifu siyo huo mdogomdogo bali hata mkubwa tusioufikiria.

Aidha, Mradi huo ni tegemeo kwa mataifa ya SADC, EAC na GLR.

Bila mradi huo, TPA itasuasua katika kutafuta ufanisi na tija.

Bila mradi huo, vyombo vyetu vya ulinzi vitapata shida ya access.

Bila mradi huo, JNIA itapoteza ufanisi wake.

Bila mradi huo, wanafunzi wa vyuo vikuu watapata shida kubwa.

Bila mradi huo Magufuli Bus Terminal itakuwa "White Elephant"

Bila mradi huo sekta za uzalishaji na utoaji huduma zitayumba.

Bila mradi huo, Tanesco itakuwa taabani nk nk nk....

Ninaamini hili litafanyiwa kazi hima kwasababu naumia kuona kodi yangu ikichezewa wakati jimboni kwetu tunavuka mto kwa kamba.

1639907882634.png

Taswira kwa hisani ya google.
 
Kuna watu watakuambia unatetea legacy. Wao wanakazana kusema kazi iendelee bila kutambua kuna mtu alianza kufanya kazi hiyo. Kazi iendelee maana yake kuna kazi ilikuwa imeanza ghafla ikasimama, wengine wakasema 'kwisha kazi'. Baada ya hiyo kwisha kazi akaja mtu ndo akasema kazi iendelee. Kazi kuendelea ni pamoja na kutambua mchango wa waliofanya kazi awali.
 
Back
Top Bottom