UZUSHI Tundu Lissu na Godbless Lema Kuhudhuria vikao vya Baraza Kuu la CHADEMA

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Kumeibuka dondoo kuwa Viongozi wa CHADEMA walio nje ya nchi Tundu Lissu na Godbless Lema wanatajwa kuwemo kwenye Vikao vya Baraza kuu la Chadema vitakavyofanyika 11/5/2022 Nchini Tanzania.

Aidha, inadaiwa pia wawili hao mpaka sasa wanazo tiketi mikononi mwao kwa ajili ya kuanza safari za kurejea nchini na kuhudhuria vikao vya chama chao.

Je kuna ukweli hapa?

1657979468103.png
 
Tunachokijua
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa yapo Madai kwamba Tundu Lissu na Godbless Lema watahudhuria kwenye Vikao vya Baraza kuu la Chadema vitakavyofanyika 11/5/2022 Nchini Tanzania.

Madai hayo pia yanawahusisha viongozi hawa kuwa na tiketi mikononi mwao kwa ajili ya kuanza safari za kurejea nchini, na kuhudhuria vikao vya chama chao.

Upi ukweli wa madai hayo?
JamiiForums imefuatilia na kubaini kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Mjumbe wa kamati Kuu ya Chama hicho, Godbless Lema wametangaza kuwa watarejea nchini hivi karibuni ili kuendeleza jitihada za kudai Katiba mpya.

Wakizungumza katika kongamano la Baraza la Vijana la CHADEMA (Bavicha) Mkoani Arusha, Mei 21, 2022 kupitia mtandao wamesema siku ya kurejea itatangazwa na watapokewa kwa uwazi.

Akizungumza kupitia mtandao, Lissu amesema:

"Lazima tutarejea nchini, tumekuwa tukiahidi kurudi lakini kuna vitu vidogo kuhusiana na masuala ya usalama wetu ila tutakuja tumechoka kukaa ugenini," amesema Lissu.

Amesema siku ya kurejea nchini itatangazwa na watakuwa na mkutano na wananchi na wakifika wataendelea na kazi ya kuimarisha chama kupitia mikutano ya hadhara na Katiba Mpya.

"Mimi na Lema tutarudi pia Wenje na wengine kwa sababu mnajua mazingira tuliyoondokea nchini,"


Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo wa Tundu Lissu ni dhahiri kwamba tarehe inayodaiwa kwamba Viongozi hapo wa CHADEMA watarejea nchini haina ukweli.

Japokuwa viongozi hao wamekiri kuwa watarejea nchini hivi karibuni lakini hawakubainisha tarehe husika.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom