Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
422
1,000
Ni muda wakusikia madini kutoka kwa Mhe. Tundu Lissu akiwa live VOA akichambua hoja na kujibu maswali mbalimbali kutoka katika chombo hiki cha kimataifa.

Karibu tumsikilize , nilitamana sana mahojiano Kama haya yangekuwa yanafanywa na televisheni na media zetu kama ilivyokuwa enzi ya JK lakini Sasa hivi wenye akili wanatakiwa wakae kimya na wasijadili chochote against current regime.

Ninachojiuliza Marekani imewahi kuacha kupiga hatua kwa ukosoaji unoendelea?

Kenya majirani zetu wamewahi kupoteza mikakati ya maendeleo kwa Uhuru wakuhoji na kujieleza?

Kwanini sisi tunataka kuwaaminisha watu maendeleo ni kunyamazisha vyombo vya habari.

Tunaona fahari gani Watanzania kuzungumza wakiwa uhamishoni? Wamekosa Nini?

Kama wanazungumza na mabeberu mbona nyinyi watawala kila siku mpo na hao hao mabeberu?

Tofauti ya ninyi kuzungumza na mabeberu na wengine kuzungumza nao ni nn?
 

Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,282
2,000
Mwigulu wizara ya fedha tumepigwa.
Jafo kumtoa TAMISEMI tumepigwa.
Kabudi kumtoa kimataifa tumepigwa.

Ondoa Gwajima weka Ummy mwalimu ingelikuwa supersub moja hatari Sana.

Ummy ni mchapa Kazi Mzuri lakini hiyo wizara aliyopewa ataonekana Kama hafanyi Kazi kutokana na uzito wa wizara ulivyo.

Inshort nauona mpasuko ukitokea ndani ya Chama Cha kijani hivi karibuni na Taifa litavurugana kwa Muda.


Lumumba vs Lissu
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
928
1,000
Habari.

Tundu Lisu alichaguliwa kwa mbwembwe kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na wafuasi wa upinzani wakawa na matumaini makubwa kuwa atakuja na mawazo mapya ya kuinua Chadema na Upinzani kwa ujumla nchini. Laa! Kama ilivyokuwa alipochaguliwa kuwa rais wa TLS badala ya kufanya kazi za taasisi iliyomchagua Lisu yuko bize kufanya kazi zake na kujiimarisha yeye binafsi!

Tundu Lisu tokea achaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema hamna clip wala mkutano wowote akiipromote Chadema lakini anaendelea kulipwa mshahara mnono kama makamu mwenyekiti wa Chadema!!

Hili halikubaliki Lisu ni mfanyakazi hewa wa Chadema na anatakiwa kutumbuliwa haraka.

Bavicha amkeni mhoji matumizi ya hela za Chadema maana Mbowe ni mwenyekiti bubu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom