PLO Lumumba: Tundu Lissu ni muongo, nimefika Chato Hayati Magufuli hana utajiri wa kumlinganisha na Mobutu Sese Seko

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,448
Mwanasheria mkongwe na mwanaharakati maarufu Afrika kutoka nchini Kenya PLO Lumumba amesema madai ya Tundu Lissu kwamba Hayati Magufuli ni tajiri kama hayati Mobutu Sseseko wa Zaire ni ya uongo na uzandiki uliopindukia.

Lumumba alikuwa anajibu swali la mtangazaji Shaka Ssali wa VOA na kusema amefika Chato na kulikuta ni eneo la kimaskini kabisa kadhalika ameshapita Dar es Salaam na Mwanza hivyo Tundu Lissu hawezi kumdanganya chochote.

Prof Lumumba amesema Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mwenzie apunguze hasira anapomzungumzia Hayati Magufuli vinginevyo atapoteza ushawishi na heshima aliyonayo.

Chanzo: VOA

Kila zama na kitabu chake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimemsikiliza PLO Lumumba, mzee anajua Sana. Nataman Sana serikali ya JMT ingekua na mtu mwenye uwezo wa kuisemea Kama Prof. Kwa ufafanuzi wake, Sasa ni rasmi dunia nzima inajua Lissu ana chuki binafsi na JPM, na ni hakika Magufuli alikuwa Kiongozi mwema, mpenda nchi yake aliyetamani kuona nchi ikipiga hatua kimaendeleo.
#TANZANIA NI YETU SOTE, TUIPENDE NA KUITUMIKIA
 
Prof Lumumba anamuita Tindu Lisi!
 
wahenga walisema kila mwamba ngoma huvutia kwake na ndicho alichofanya Prof Lumumba huyo ni teja kwa mwendazake hasikii haoni kila hoja ya ubaya wa mwendazake huitwist vizuri na mark up.
 
Apoteze mara ngapi? Hana hata akili ya kujua anamshambulia anatoka kanda yenye nguvu sana kisiasa..ina wapiga kura wengi sana. Hata kama kuna watu walikuwa wanam support huko wamepoteza kiongozi wao yeye ni kumshambulia..Subiri arudi huko tena ndio atajua ushawishi wake umeshuka kiasi gani.
 
Lumumba hana mabadiliko yoyote aliyowahi kuchangia katika uchumi wake na uchumi wa Afrika licha Dunia, ukimsikiliza unachokiona ni maneno yakiingereza yaliyopakwa Nakshi.

Mazingira ya Chato miaka mitano Leo hii kwa msomi mzalendo anaweza kutetea kilichofanyika? Lakini najiuliza lini alifika chato? Kwa ninavyomfahamu hakuna alipokanyaga bila media kuwa nyuma yake maana si kwa mbwembwe hizo.

Mfuatilie Lumumba kwenye uchaguzi wa Kenya uliopita utajua who his Lumumba
 
Back
Top Bottom