Uchaguzi 2020 Ushindi wa CCM mwaka huu utakuwa mtamu sana kwa sababu Dkt. Magufuli atamshinda mpinzani wa kweli Tundu Lissu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,975
141,986
Tangu chaguzi za vyama vingi zianze tumezoea kuona wagombea urais wa upinzani ambao wamewahi kuwa wanachama wa CCM au TANU huko nyuma.

Sina hakika kama huyu Tundu Lissu aliwahi kupitia chipukizi au UVCCM wakati akiwa mwanafunzi ila siasa za " ukubwani" amezianzia NCCR mageuzi.

Ndio kusema kwa mara e kwanza CCM inakutana na mpinzani wa kweli tangu mfumo wa vyama vingi uasisiwe.

Maana yake ni kwamba ushindi wa Rais Magufuli hapo Oktoba 28 utakuwa mtamu sana kupita chaguzi zote zilizotangulia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Labda ashinde na njaa
IMG_20200929_221037.jpg
 
Ushindi mtamu sana.

Awamu ya kwanza ilikua njema,

Mitano tena itakuwa iliyojaa neema kwa Kila Mtanzania.
 
mtoto aishangaa CCM.jpg
Kuwa na huruma kijana...mhurumie hata huyu mtoto mdogo aliyebaki akishangaa asiweze kuamini anachokishuhudia kikitendeka
mbele ya macho yake

Ilinganishe hiyo hali hapo juu na hii hapa chini...!



Yaani mkombozi kama huyu ashindwe kwenye sanduku la kura...! Sema tu mtaiba kama ilivyo kawaida ya chama cha mafisadi, CCM!
 
Hii hali sio sawa kwa mgombea urais wa CCM mpya, kuna jambo lakini anajitahidi kulificha.

Hivi hawezi kujitoa katika mbio za urais ? Maana kushinda haiwezekani mwaka huu, nadhani hapa kulilia Gwajima anaombea miujiza lakini anajua haiwezi kutokea na anaonesha frustration kali za kudanganywa na kina Humphrey Polepole na Dr. Bashiru Ally Kakurwa
 
Back
Top Bottom