Kwani kuna ajabu gani?Ndugai tulimtibu kwa michango yetu ambazo ni kodi zetu.Tanzania inaomba misaada nje na mpaka sasa bajeti inategemea wafadhili kwa asilimia zaidi ya 45!!
Na hii wala sio kumchafua,watu walianza kumchangia toka akiwa Nairobi.Na yeye amekiri hivyo.Sina itikadi moja na Lissu,lakini nilimchangia kuanzia usafiri wa kutoka Dodoma kwenda Nairobi na mpaka matibabu.Nitaendelea kumchangia.
Kwangu,utu kwanza na itikadi baadae.Siasa na itikadi vitapita,JPM atamaliza muda wake na ataondoka,lakini utu na thamani ya uhai wa mtu vinadumu milele.Naona hapo juu watu wanamtukania mpaka mkewe,sasa mlitaka asichangiwe wakati hajapewa pesa ya matibabu?Jamani jamani hizi siasa za awamu hii,ni chuki tupuu