Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Binafsi nimeumia na kujisikia vibaya sana kitendo cha serikali wanachomfanyia Tundu lissu cha kusitisha malipo na mshahara wake.

Mh. Tundu lissu ameingia katika wakati mgumu sana na inasikitisha akiomba sehemu ya kula , kulala na ada kwa ajiri ya watoto wake!

Mungu ibarika Tanzania, mungu mbariki Tundu Lissu

Haya maisha tu! Leo kwake kesho kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shithole ,video ya siri wakati anatumia kisemeo!!! Haikuwa kitu ya siri hata kidogo aliisema wazi alipokuwa na mkutano na diaspora na alieleza sababu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ndugu yenu bi tapeli mkubwa na msaliti. Anachokipitia anastahili kabisa. Kila siku kutukana watu na kujifanya yeye ndiye mjuaji wa kila jambo. Mgonjwa gani kila siku kuzunguka kuitukana serikali na nchi yetu?

Ibambasi,
Acha ushabiki wa u-homeboy hapa.
Unelikuwa unampenda homeboy wako Jiwe usingeongea haya unayoongea. Tundu Lissu kaponea tundu ya sindano kuawa....Serikali ya mjomba wako imekataa kumtibia Lissu kwa gharama za Bunge/Serikali kwa maksudi kabisa ili afe.
Mpaka leo hakuna aliyekamatwa wala uchunguzi wowote kuhusu hilo tukio.

Anachofanya Lissu huko nje ni kuwaeleza watu huko nje wajue kile kilichomtokea na hakuna alichotukana hapo..!!Hiv kuambiwa kuwa Serikali haijafanya lolote kuhusu tukio la kushambuliwa kwake ni kuitukana serikali? Kwamba Serikali ya CCM imekataa kumlipia gharama za matibabu ni kuitukana serikali? Kuhoji kwamba CCTV Camera ziling'olewa kwenye makazi aliyokuwa akikaa kabla ya shambulio ni kutukana Serikali? Kama madai hayo ni uongo mbona Serikali ya jomba haijitokezi hadharani na UTHIBITISHO kuwa anachodai Lissu ni UZUSHI au UONGO wakamaliza ubishi?

Spika Ndugai alijitututumua juzi Bungeni ati ataweka MKEKA(Bank statement whatsoever) wa malipo ya Mhe. Lissu kiasi cha 250m/= ati za matibabu kumbe ilikuwa ni stahili zake za mishahara na posho za Mbunge akiwa kwenye matibabu na wala si malipo ya Hospitali kama alivyotaka kupotosha...!!.
Tunataka Serikali wajibu hoja zile CCTV Camera ziko wapi na zili-record nini wakti wa tukio siku ile ya 7th Sept,2017.Kwa kawaida CCTV Camera hu-record matukio yote kwa siku, saa, dakika na sekunde yaani 24/7. Mje ya hapo ni longolongo na uzushi wa kuwachanganya watu akili ili kupoteza malengo na hoja.
 
Mpiganaji wa kweli hawezi kuomba msaada kitapeli namna hiyo. Lissu atambue kuwa njaa haina ukamanda

CCM na Serikali yako ya Magufuli wamewahi kuomba MISAADA mara ngapi na ikaishia kunenepesha matumbo ya KIJANI hapo mtaa wa Lumumba??? Hemu..tusidanganyane bhana..!!.
 
Hii video umewahi iona?Huoni kuna mtu alirecord kwa siri na sio wahusika wenyewe?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.

Mwenyewe anajiona yupo d
Mbona hakuna kitu cha ajabu.Tumeanza kumchangia toka akiwa Nairobi na hadi Ubelgiji.Yaani huyu bwana sisi ndio tunampa Coverage,maana tunamzungumzia sana wakati kuna mambo yetu kama Chama na serikali tunatakiwa kuyatolea majibu.

Job huo mshahara aliozuia hata yeye sio wake,ni kodi za wananchi.Ukiwa mwanasiasa,pesa unayotumia ni kodi za wananchi na sio zako.

Lissu kaanza kusaidiwa kwa watu kuzunguka kumuombea misaada...Alipopata nafuu akasema ye mwenyewe atazunguka,na ataenda kuwashukuru wote waliomchangia mpaka kafikia hapo.Account zilitolewa toka akiwa Nairobi na tulichanga.Sasa hapa kuna kipi labda kipya?

Kuna watu walitegemea wakikata mshahara huyu bwana atapiga magoti,sasa wanadhani kwa kuweka video hii wanamdhalilisha Lissu.Kitengo chetu cha mikakati na Propaganda kimefubaa sana.

Tunatakiwa kumjibu Lissu kwa namna ya matendo ambayo yeye atakosa hoja,hizi hoja za ombaomba hazina mashiko.Sisi kama Taifa tunakopa na kuomba kila siku.Hao tunaoita mabeberu,mwezi ujao bunge la bajeti Mh.Mpango atawataja kwenye hotuba kama wadau wa maendeleo na si mabeberu.

Lissu katibiwa kwa pesa za wasamalia wema toka siku amenyanyuka Dodoma na ndege ya Flight link.

Mwisho wa siku,kila mtu ataonja mauti,licha ya kutukana na kusakama watu nyuma ya keyboard.Taifa linalofikia kuona uhai wa mtu ni kama uhai wa kuku,na watu wake kufurahia,ni Taifa linaloelekea kuvurugika kwa chuki.

Halafu wewe nawe,kwani ni dhambi au vibaya wewe kuwa mfuasi wa lissu na chama chake?unaleta kujificha ficha mara sijui utu mara nini sijui?au unafikiri watu wote ni wajinga humu?
 
CCM na Serikali yako ya Magufuli wamewahi kuomba MISAADA mara ngapi na ikaishia kunenepesha matumbo ya KIJANI hapo mtaa wa Lumumba??? Hemu..tusidanganyane bhana..!!.
Ujumbe kwa Lissu...njaa haina ukamanda. Arudi tu home
 
CHADEMA mkishika 'KUNAKO' mnakimbilia kutukana,huu sio wakati wake.Msaidieni mwenzenu jamani.
T.A.L ni kiboko yenu mmemchangia kuanzia mabalozi mpaka wakuu wa idara nchi nzima na amewagaragaza wote, sasa mmepata cha kusema, hili mnadhani litamrudisha nyuma hicho ni CHUMA CHA PUA.
 
Ibambasi,
Acha ushabiki wa u-homeboy hapa.
Unelikuwa unampenda homeboy wako Jiwe usingeongea haya unayoongea. Tundu Lissu kaponea tundu ya sindano kuawa....Serikali ya mjomba wako imekataa kumtibia Lissu kwa gharama za Bunge/Serikali kwa maksudi kabisa ili afe.
Mpaka leo hakuna aliyekamatwa wala uchunguzi wowote kuhusu hilo tukio.

Anachofanya Lissu huko nje ni kuwaeleza watu huko nje wajue kile kilichomtokea na hakuna alichotukana hapo..!!Hiv kuambiwa kuwa Serikali haijafanya lolote kuhusu tukio la kushambuliwa kwake ni kuitukana serikali? Kwamba Serikali ya CCM imekataa kumlipia gharama za matibabu ni kuitukana serikali? Kuhoji kwamba CCTV Camera ziling'olewa kwenye makazi aliyokuwa akikaa kabla ya shambulio ni kutukana Serikali? Kama madai hayo ni uongo mbona Serikali ya jomba haijitokezi hadharani na UTHIBITISHO kuwa anachodai Lissu ni UZUSHI au UONGO wakamaliza ubishi?

Spika Ndugai alijitututumua juzi Bungeni ati ataweka MKEKA(Bank statement whatsoever) wa malipo ya Mhe. Lissu kiasi cha 250m/= ati za matibabu kumbe ilikuwa ni stahili zake za mishahara na posho za Mbunge akiwa kwenye matibabu na wala si malipo ya Hospitali kama alivyotaka kupotosha...!!.
Tunataka Serikali wajibu hoja zile CCTV Camera ziko wapi na zili-record nini wakti wa tukio siku ile ya 7th Sept,2017.Kwa kawaida CCTV Camera hu-record matukio yote kwa siku, saa, dakika na sekunde yaani 24/7. Mje ya hapo ni longolongo na uzushi wa kuwachanganya watu akili ili kupoteza malengo na hoja.
Anarusha tuhuma zisizo na uthibitisho...ujumbe kwake ni kuwa njaa haina ukamanda. Arudi tu home
 
Njaa haina ukamanda. Lissu tayari kasanda
Adui wa Lissu siyo sisi wananchi ila ni kundi dogo la watawala ambao alishasema atanyamaza akiwa kaburini

Angesanda kwa muuaji wake hapo ningekuelewa, ila kwa kuwa anaomba michango kwa wananchi wenye kujali utu wa mwanadamu sioni tatizo labisa

Na kama tatizo lingeanzia kwenye kuomba michango ya matibabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuuuuuuuuuuh !!!!!
Ama kweli ! Mtu aliyekuwa anaongea kwa ujeuri na ufedhuli mkubwa takribani siku nne zimepita leo hii anabembeleza achangiwe apate chakula ! Anaongea kwa sauti ya unyonge mpaka mimi mwenyewe natamani kulia.
Muuaji hajawahi kutamani kulia pale anapoona aliyekusudia kumuua bado anasurvive

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nimeumia na kujisikia vibaya sana kitendo cha serikali wanachomfanyia Tundu lissu cha kusitisha malipo na mshahara wake.

Mh. Tundu lissu ameingia katika wakati mgumu sana na inasikitisha akiomba sehemu ya kula , kulala na ada kwa ajiri ya watoto wake!

Mungu ibarika Tanzania, mungu mbariki Tundu Lissu

Haya maisha tu! Leo kwake kesho kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa mliokua mnasema analipwa na mabeberu je mabeberu wamemuacha?Ay mlitudanganya?leo tumejua ukweli hatumiki na mabeberu ila mabeberu waliokua wanamlipa ni CCM
 
Dawa pekee ya kumnyamazisha Lissu huko Duniani aliko ili aachane na kuituhumu serikali yake, dawa hiyo aliyenayo ni serikali yenyewe kujishughulisha na suala la Lissu ikiwa ni pamoja na ;

1.Serikali kutoa ushahidi usio na shaka wa mtu halisi aliyehusika kumshambulia Lissu

2. Serikali kuieleza Dunia walikokuwa walinzi waliokuwa zamu kulinda nyumba za serikali wakati Lissu anashambuliwa.

3. Serikali kuieleza Dunia zilikokwenda CCTV camera baada ya Lissu kushambuliwa.

Kwa nini serikali ndo inapaswa kuwa na majibu haya? Kwa sababu ndo pekee ina mamlaka ya kutoa majibu hayo na si mwingine!!! Hayo ndiyo maswali pekee ambayo Lissu amekuwa akiyauliza kila kwenye chombo cha habari cha kimataifa anachoalikwa!!
Masuala haya yote ni ya kiuchunguzi ambao bado haujakamilika kwasabbu victims (Lissu na Dereva wake) hawajayatoa maelezo yao polisi. Sasa unatoaje taarifa ya uchunguzi wakati upande mmoja unaohusika haujahojiwa. Matokeo yake taarifa inaweza kutolewa hadharani wakaja tena kupinga wakasema ni ya uongo na kwamba polisi hawakutaka kuchukua maelezo yao.

Kwahiyo masuala yanayohusu kazi na weledi wa watu tusipende kuyaingilia kutokana tu na ushabiki wetu. Siku Lissu na Dereva wake watakapotua nchini kila kitu kitajulikana.kwanza hiyo CCTV Camera polisi walishasema toka mwanzo kwamba waliichukua kama sehemu ya uchunguzi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utaratibu wa kumchangia Mh, LISSU upoje kwa sisi wa Scandinavian kwa mfano. Kamanda hatokufa njaa na hatolala nje na watoto watasoma.Tutabeba mabox tutakata vitunguu, tutasafisha vyoo na tutalea wazee mpaka kieleweke.
Hivi Mh Lissu atakuja kututembelea huku na sie tupate baraka zake.?
 
Back
Top Bottom