Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Tundu Lisu kasema hana kodi ya pango na ya chakula ubelgiji na hana hela za ada za watoto anawaomba watanzania walioko marekani kumchangia .


Ni nani aliyekwambia Lissu alikuwa anachangiwa na kuhudumiwa na ubeligiji?.
 
Sasa ulitaka afe, jamani tumefikia hapa siamini. Mimi nilienda leba mtoto anauma jamani. Tuachane na siasa, pigs picha mtoto wako wakiume uambiwe amepigwa risasi ametelekezwa. Mungu adhihakiwi mteme mate chini hakijawafika
 
Wamenusa harufu kuwa muda si mrefu kuna omba omba mmoja atatua ofisi za Bavicha kutaka achangiwe chakula,mavazi ,Kodi ya pango na ada za watoto wake michango ambayo wao hawajazoea ndani ya Bavicha na chadema kwa ujumla
Afadhali kuchangia kuliko kuiba
 
Ikiwa MzeeMwanakijiji, Nyaningabu wanasurvive ughaibuni kwa kubeba boksi, hivi kwa elimu aliyo nayo TL kama mnavyomkubali atashindwa kusurvive huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunachangia harusi sembuse kuokoa maisha ya mtu! kuwa binadamu kidogo baasi!!
 
Hata mimi sijaona cha ajabu sana Tundu Lissu kuomba msaada kwani tangu Nairobi mpaka Ubelgiji amekuwa akisaidiwa na wasamaria wema. Halafu huyu jamaa bado anaendelea na matibabu tar 20 anafanyiwa operation nyingine. Tuendelee kumchangia kwa nguvu wenye roho mbaya wanaumia sana.
 
Mbona hakuna kitu cha ajabu.Tumeanza kumchangia toka akiwa Nairobi na hadi Ubelgiji.Yaani huyu bwana sisi ndio tunampa Coverage,maana tunamzungumzia sana wakati kuna mambo yetu kama Chama na serikali tunatakiwa kuyatolea majibu.

Job huo mshahara aliozuia hata yeye sio wake,ni kodi za wananchi.Ukiwa mwanasiasa,pesa unayotumia ni kodi za wananchi na sio zako.

Lissu kaanza kusaidiwa kwa watu kuzunguka kumuombea misaada...Alipopata nafuu akasema ye mwenyewe atazunguka,na ataenda kuwashukuru wote waliomchangia mpaka kafikia hapo.Account zilitolewa toka akiwa Nairobi na tulichanga.Sasa hapa kuna kipi labda kipya?

Kuna watu walitegemea wakikata mshahara huyu bwana atapiga magoti,sasa wanadhani kwa kuweka video hii wanamdhalilisha Lissu.Kitengo chetu cha mikakati na Propaganda kimefubaa sana.

Tunatakiwa kumjibu Lissu kwa namna ya matendo ambayo yeye atakosa hoja,hizi hoja za ombaomba hazina mashiko.Sisi kama Taifa tunakopa na kuomba kila siku.Hao tunaoita mabeberu,mwezi ujao bunge la bajeti Mh.Mpango atawataja kwenye hotuba kama wadau wa maendeleo na si mabeberu.

Lissu katibiwa kwa pesa za wasamalia wema toka siku amenyanyuka Dodoma na ndege ya Flight link.

Mwisho wa siku,kila mtu ataonja mauti,licha ya kutukana na kusakama watu nyuma ya keyboard.Taifa linalofikia kuona uhai wa mtu ni kama uhai wa kuku,na watu wake kufurahia,ni Taifa linaloelekea kuvurugika kwa chuki.
Umemaliza kila kitu mkuu, mwenye sikio na asikie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtazidi kuumia kwa Lissu, yeye anacheka tu, nyie hamlali
 
Haya ndio mambo niliyakataa mimi.

Lissu mh,huwezi shindana na mtu anayekuweka mjini,hawa wafuasi fulsa wa humu jf na kwingineko hawana msaada wowote kwako.zaidi ya kujichukulia point tatu muhimu.

Hata kama unaituhumu serikali kwa balaa lililokupata bado kuna njia nyingine ya maana zaidi ya hii uliyotumia,wewe ni mwanasheria mzuri na unajua haya.

Embu niambie bw job akiiona hii video anajisikiaje!!!

Hata wanajf na wadau wengine wakiamua kukuchangia,hawatafanya hivyo wakati wote,kuna wakati watachoka.

Anyway pole sana kwa kipindi unachopitia.

Lissu genius

tunamuangalia
 
Ana watu wake wa kutembeza bakuli akina Mahiga, Masilingi, Slaa n.k

Huoni Deni la Taifa limeongezeka sana kwa kipindi cha miaka 3 tu.
Umeshasema deni,kwani lisu anaomba msaada au mikopo?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
very sory for him,,ila amepitia mengi na ana haki yakupungukiwa na fedha kwa muda aliokaa kwenye matibabu huku mkewe nae akisimamisha shughuli zake nyingi hvyo lazima wameyumba....KWA KUWA LISU NI SHUJAA NA MFANO MZURI KWA WENGI WAPENDA HOJA HATAAIBIKA KAMA WANAVYOWAZA MAFISI WE WILL HELP YO BROTHER.....
 

Attachments

  • tundulissu-300x160.jpg
    tundulissu-300x160.jpg
    6.1 KB · Views: 20
Huyu jamaa ataelewa tu baadae ngoja tuone huko mbele akipoteza kila kitu kuanzia ubunge mpaka mashabiki na hapo atabaki mwenyewe na familia yake wakikodoleana macho na wasijue wa kumlaum, kitakachomsaidia ni kufungua ka ofisi ka uwakili kuganga njaa.... Ni jambo la muda tu.

Over

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndicho mnachomtakia baada ya kushindwa kumuua?
 
Back
Top Bottom