Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Baada ya TUNDU LISU kupigwa risasi bila Shaka damu yake ilimwagika sana, alipigwa, tena alipigwa risasi nyingi mno, hakika aliusikilizia mwili wake vyuma vya moto vikiingia mwilini. Hakika vile vyuma viliuchana mwili wake mithili ya NYAMA bucha. Aliyemimina RISASI alizimimina Kweli Kweli, alimimina kwa lengo la kuua, kwa lengo la kutoa roho, kwa lengo la kuiangamiza NAFSI iliyohai, alivaa sura, sura ya kutenganisha nafsi, mwili, na Roho.
Lakini LISU alipona, yupo hai, anavuta pumzi, pumzi ya Baba wa mbinguni, Mungu aliye hai, yawezekana alikosa, tena Kosa kubwa, yawezekana ni msaliti, muongo, mwizi, mhalifu asiyesameheka, yawezekana, hafai kabisa. Lakini cha ajabu asiyefaa amepona kwa jinsi ya ajabu, kwa namna tusiyoijua, maana kanuni ya uhai ni fumbo.
Nakumbuka wakati nikiwa mdogo miaka ya sabini pale kurasini shimo la udongo, wakati eneo lile lilijaa mikorosho mingi sana, haukuwa mji kama Leo. Enzi za Mzee bongo Lolo. Nakumbuka watu walipiga mwizi, walikuwa mamia ya watu, na yule mwizi alipigika hasa, mwili wote ulijaa damu, walimwacha waliamini amekufanya, walimwacha, kila mtu alirudi nyumbani kwake, baada sisi wadogo tulishuhudia Yule mwizi akiinuka, damu ilikuwa imejaa hata USO haukuonekana, alianguka tena chini, msamalia mmoja alimsaidia kusimama, akitia huruma SANA sijui kama alipona.
Inawezekana LISU ni alama tusiyoijua, ni ujumbe tusioujua, maana sisi tu wanadamu. Kwani wangapi tunawaombea mabaya? Wangapi tunatamani wafe, kwa sababu tunahisi ni vikwazo kwenye maisha yetu? Ila hatuna bunduki? LISU survived, NI mzima, mwache aombe, aombe, mwache roho na nafsi yake vihangaike, tumwache, hakuna anayejua mwisho wake, kuna watu walimuombea vibaya LOWASA Leo hawapo, kuna watu wanamuombia raisi mabaya sisi wanadamu tuna roho ngumu SANA. Mwacheni LISU ahangaike, mwacheni. Kupona kwake ni nafuu kwa familia yake, hapo NDIPO tumaini lake lilipo. Pia tuache USHABIKI.

Upupu mtupu
Kuhangaisha watu tu
Jimboni kwake ni wangapi wanateseka na kufa kwa ajili ya ubinafsi wake?
Wamemchagua kuwa mbunge wao lakini yeye kutwa alikuwa Dar tu
Sasa amepona kaamua kwenda kutangatanga huko na li wheelchair lake
Laana ya Tanzania na Africa inamtafuna


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo bado hajapokwa Ubunge na ni Juzi tu kalipwa almost 200M, navuta picha after 2020 akiwa sio mbuge na Mashabiki wote wamehamisha majeshi si atakufa njaa mana kwa sasa tu analipwa Ndio ivo tena anaanza kupitisha bakuli, TAL angekuwa na busara angerudi tu nyumbani aje apige kazi au nae anataka kuwa mchuuzi wa supermarket kama W.slaa
Jitahidi kusoma na kuelewa, zile 200m alizolipwa ni mishahara yake ya miezi 15 ambayo na wabunge wote wamelipwa. Malipo hayo hayajafanyika kwa mara moja, ni malipo ya kila mwezi. Hoja ya spika ni kwamba hizo 200m ni jumla ya hela alizolipwa akiwa nje ya bunge. Kwa hiyo wamezuia hayo malipo ya kila mwezi mpaka arudi kuanza kuhudhuria bungeni aache kuzurula huko ulaya na marekani.
Halafu kenge ligola kaagiza akamatwe!
 
Mi apo sijaelewa. Afu ndo huyu aruhusiwe na mbowe kugombea urais badala ya Lowassa! hajui kuwa mwenzie anaweza kunyang’anywa mke.
 
Unategemea lisu angeishi vp?kwa ukatili aliofanyiwa?lisu yupo sahihi kabisa.yanga kila siku wanatuomba
nch kila siku wanaomba kwa wahisani
wasanii hvyo hvyo
sembuse lisu aliyepata matatizo?
 
Huyu jamaa ataelewa tu baadae ngoja tuone huko mbele akipoteza kila kitu kuanzia ubunge mpaka mashabiki na hapo atabaki mwenyewe na familia yake wakikodoleana macho na wasijue wa kumlaum, kitakachomsaidia ni kufungua ka ofisi ka uwakili kuganga njaa.... Ni jambo la muda tu.

Over

Sent using Jamii Forums mobile app
Jipeni matumaini hewa.Lissu ni mtu wa watu hawezi kwama.
 
Mi apo sijaelewa. Afu ndo huyu aruhusiwe na mbowe kugombea urais badala ya Lowassa! .
Lisu hela ya Kula, kulala ,nguo za kuvaa yeye,mkewe na watoto hana na hana na hela ya ada za watoto hana hiyo hela ya kampeni ya uraisi atatoa wapi? Aachie wenye pesa akina Sumaye,Lowasa,Mbowe na Nyalandu.Tundu Lisu Huyo anataka pia kugombea uenyekiti Chadema taifa amtoe Mbowe anataka ale tu pesa za chadema.
 
Mi apo sijaelewa. Afu ndo huyu aruhusiwe na mbowe kugombea urais badala ya Lowassa! hajui kuwa mwenzie anaweza kunyang’anywa mke.
Kipimo chako hakijazingatia sababu ya kuomba msaada kumbuka kwanza bila wewe kumpiga Risasi asingeweza kuwa na Taabu pili bila Ndungai kuiba mshahara wake na kuzuia pesa za matibabu asingeweza kutoa kilio chake na kama kigezo chako eti kuomba msaada pindi umekomolewa ni aibu utakuwa umebugi sana, Duniani kote wanajua watesi wa CCM mpo busy kumkomoa Tundu Lisu hata mje na visingizio vigezo gani wananchi wanajua kuwa Tundu anakomolewa na watesi wa CCM hivyo usikae kuwaza peke yako ukazani na wengine hawajui roho mbaya ya watesi wa CCM
 
Lisu hela ya Kula na kulala na ada hana hiyo hela ya kampeni ya uraisi atatoa wapi? Aachie wenye pesa akina Sumaye,Lowasa,Mbowe na Nyalandu.Tundu Lisu Huyo anataka pia kugombea uenyekiti Chadema ale tu pesa za chadema.
Huu mfano sidhani kama umesoma ulichokiandika kabla ya kutuma, maana nina imani ukisoma utaacha kuvuta Bangi kisha kuja mitandaoni kutengeneza maneno yasiyo na mashiko, nyie watesi wa CCM endeleeni na roho mbaya zenu lakini mtambue hakuna kisicho na mwisho wake
 
Kuomba msaada siyo dhambi na kutokuwa mbunge siyo kipimo cha kuwa na njaa kwani baada ya ubunge kuna Maisha na watu hujiongeza kulingana na mazingira ya kipindi hicho, kumbuka kaamua kuomba msaada baada ya Ndungai kuiba mshahara wake na pia waligoma kulipia matibabu yake pengine hizo milion 200 kajilipia matibabu na gharama zingine, hakuna ubaya wala Aibu kuomba msaada kutokana na watesi wa CCM kutengeneza mazingira ya kumkomoa.
Ubaya ni pale anapotumia utapeli ili watu wachange - kutumia maneno kama "you can imagine hivi watashangiliaje wakisikia watoto wamefukuzwa shule!" na mengine-ni utapeli.
 
Back
Top Bottom