Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Tundu Lissu akiomba misaada Marekani

Haya ndio mambo niliyakataa mimi.

Lissu mh,huwezi shindana na mtu anayekuweka mjini,hawa wafuasi fulsa wa humu jf na kwingineko hawana msaada wowote kwako.zaidi ya kujichukulia point tatu muhimu.

Hata kama unaituhumu serikali kwa balaa lililokupata bado kuna njia nyingine ya maana zaidi ya hii uliyotumia,wewe ni mwanasheria mzuri na unajua haya.

Embu niambie bw job akiiona hii video anajisikiaje!!!

Hata wanajf na wadau wengine wakiamua kukuchangia,hawatafanya hivyo wakati wote,kuna wakati watachoka.

Anyway pole sana kwa kipindi unachopitia.
 
AMELIPIGANIA TAIFA.TUTAMPIGANIA NA YEYE.MNASITISHA MSHAHARA WAKE.MMESUSIA MATIBABU YAKE.MNAFIKIRI YEYE NI BENKI.KAMA WAZEE WA DARESSALAAM MIAKA YA 50 WALIVYOMBEBA NYERERE.NA SISI TUTAKUBEBA LISSU.

CHADEMA WEKENI UTARATIBU TUMSAPOTI MPIGANAJI WETU.
CHADEMA wenyewe hawamsapoti Lissu kwa sasa.
 
It's okay Lissu kuomba wamsaidie, matibabu yake ni cost full.
Na baada ya spika kumpoka haki zake anahitaji msaada aweze ku survive(yeye na família yake).
Binafsi nitamchangia Lissu, by the way ana deserve kuchangiwa after all the drama he has been through.
Si mlisema mnamchangia tangu wiki iliyopita baada ya Spika kusema Bunge linaangalia namna ya kutomlipa Lissu maana ni mtoro kazini,mnasubiri nini au ilikuwa mikwara tu
 
Mkuu, usiwe na hasira hii ndio dunia ina kanuni zake za kuishi!

Mwambie Lisu aache jeuri hataweza kuwapigania watanzania akaweza, mwambie arudi kuwawekea mazingira mazuri watoto wake basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lissu hajawahi kuwa mtumwa wa fikra za watala wajinga

Kukubali kuwa mtumwa za fikra za watawala ni kuuza utu, jambo ambalo lissu kwake ni msamiati mgumu

Hao akina Nelson Mandela walikuwa wanaahidiwa mamilioni ya fedha na cheo ili waache harakati za kutetea waafrika wenzao, lakini pesa na vyeo hawakuona thamani yake ikiwa jamii ya watu weusi wenzio wakiwa ktk mateso ya makaburu

Lissu namfananisha na akina Dr Rev. Martin Luther King Jr, Malcolm x na wapigania haki za watu weusi wengine nchini Marekani waliojitoa kwa ajili ya jamii pana ya wamarekani weusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo bado hajapokwa Ubunge na ni Juzi tu kalipwa almost 200M, navuta picha after 2020 akiwa sio mbuge na Mashabiki wote wamehamisha majeshi si atakufa njaa mana kwa sasa tu analipwa Ndio ivo tena anaanza kupitisha bakuli, TAL angekuwa na busara angerudi tu nyumbani aje apige kazi au nae anataka kuwa mchuuzi wa supermarket kama W.slaa

Hayo ndio maisha ya mwanaume. Hakuna cha ajabu kwa mpiganaji, labda kama ww unategemea mshahara tu ndio utaona tofauti.
 
Lissu yuko tayari kuishi kwenye umasikini ila siyo kulamba nyayo za mtawala

Lissu ni shujaa haishi kwa kumpigia magoti mtawala

Huyu ndio Lissu nimjuaye mimi

Lissu atoe tu akaunt namba ya bank tumpe pesa za kujikimu

Pesa tutamchangia zaidi ya mshahara wa ubunge

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Asante sana kwa KUKANDAMIZA kwenye hili.
 
Mbona hakuna kitu cha ajabu.Tumeanza kumchangia toka akiwa Nairobi na hadi Ubelgiji.Yaani huyu bwana sisi ndio tunampa Coverage,maana tunamzungumzia sana wakati kuna mambo yetu kama Chama na serikali tunatakiwa kuyatolea majibu.

Job huo mshahara aliozuia hata yeye sio wake,ni kodi za wananchi.Ukiwa mwanasiasa,pesa unayotumia ni kodi za wananchi na sio zako.

Lissu kaanza kusaidiwa kwa watu kuzunguka kumuombea misaada...Alipopata nafuu akasema ye mwenyewe atazunguka,na ataenda kuwashukuru wote waliomchangia mpaka kafikia hapo.Account zilitolewa toka akiwa Nairobi na tulichanga.Sasa hapa kuna kipi labda kipya?

Kuna watu walitegemea wakikata mshahara huyu bwana atapiga magoti,sasa wanadhani kwa kuweka video hii wanamdhalilisha Lissu.Kitengo chetu cha mikakati na Propaganda kimefubaa sana.

Tunatakiwa kumjibu Lissu kwa namna ya matendo ambayo yeye atakosa hoja,hizi hoja za ombaomba hazina mashiko.Sisi kama Taifa tunakopa na kuomba kila siku.Hao tunaoita mabeberu,mwezi ujao bunge la bajeti Mh.Mpango atawataja kwenye hotuba kama wadau wa maendeleo na si mabeberu.

Lissu katibiwa kwa pesa za wasamalia wema toka siku amenyanyuka Dodoma na ndege ya Flight link.

Mwisho wa siku,kila mtu ataonja mauti,licha ya kutukana na kusakama watu nyuma ya keyboard.Taifa linalofikia kuona uhai wa mtu ni kama uhai wa kuku,na watu wake kufurahia,ni Taifa linaloelekea kuvurugika kwa chuki.
 
Lissu yuko tayari kuishi kwenye umasikini ila siyo kulamba nyayo za mtawala

Lissu ni shujaa haishi kwa kumpigia magoti mtawala

Huyu ndio Lissu nimjuaye mimi

Lissu atoe tu akaunt namba ya bank tumpe pesa za kujikimu

Pesa tutamchangia zaidi ya mshahara wa ubunge

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha uongo NA kujigamba, kama ungekuwa NA nia nzuri unge enda ufipa NA ingepewa kila njia ya kumfikishia huo mchango.
 
Huyu jamaa ataelewa tu baadae ngoja tuone huko mbele akipoteza kila kitu kuanzia ubunge mpaka mashabiki na hapo atabaki mwenyewe na familia yake wakikodoleana macho na wasijue wa kumlaum, kitakachomsaidia ni kufungua ka ofisi ka uwakili kuganga njaa.... Ni jambo la muda tu.

Over

Sent using Jamii Forums mobile app
M/mungu atamlisha yeye ña wanae, hawezi kubakia peke yake, iyo aliyopitia Kaka lissu ni njia ambayo watu wengi walipitia kabla Mungu kuwanyanyua madaraja ya juu ktk dunia, aliweza kumuokoa ña kifo, hatashindwa Kwa hayo mepesi kbs
 
Back
Top Bottom