Mbona hakuna kitu cha ajabu.Tumeanza kumchangia toka akiwa Nairobi na hadi Ubelgiji.Yaani huyu bwana sisi ndio tunampa Coverage,maana tunamzungumzia sana wakati kuna mambo yetu kama Chama na serikali tunatakiwa kuyatolea majibu.
Job huo mshahara aliozuia hata yeye sio wake,ni kodi za wananchi.Ukiwa mwanasiasa,pesa unayotumia ni kodi za wananchi na sio zako.
Lissu kaanza kusaidiwa kwa watu kuzunguka kumuombea misaada...Alipopata nafuu akasema ye mwenyewe atazunguka,na ataenda kuwashukuru wote waliomchangia mpaka kafikia hapo.Account zilitolewa toka akiwa Nairobi na tulichanga.Sasa hapa kuna kipi labda kipya?
Kuna watu walitegemea wakikata mshahara huyu bwana atapiga magoti,sasa wanadhani kwa kuweka video hii wanamdhalilisha Lissu.Kitengo chetu cha mikakati na Propaganda kimefubaa sana.
Tunatakiwa kumjibu Lissu kwa namna ya matendo ambayo yeye atakosa hoja,hizi hoja za ombaomba hazina mashiko.Sisi kama Taifa tunakopa na kuomba kila siku.Hao tunaoita mabeberu,mwezi ujao bunge la bajeti Mh.Mpango atawataja kwenye hotuba kama wadau wa maendeleo na si mabeberu.
Lissu katibiwa kwa pesa za wasamalia wema toka siku amenyanyuka Dodoma na ndege ya Flight link.
Mwisho wa siku,kila mtu ataonja mauti,licha ya kutukana na kusakama watu nyuma ya keyboard.Taifa linalofikia kuona uhai wa mtu ni kama uhai wa kuku,na watu wake kufurahia,ni Taifa linaloelekea kuvurugika kwa chuki.