Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,372
- 55,713
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 10.
Kwa kutumia kesi ya Khatibu Gandi na Grey Kungu Mataka, naomba Mahakama itupilie mbali mashitaka haya kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d).
Mashtaka walipaswa kuthibitisha uhaini katika kesi hii.
Waheshimiwa Majaji, nimemaliza suala la tatu. Naomba niende katika suala la nne.
Suala la nne ni: Je, hayo maneno yaliyotamkwa na mshitakiwa yanatengeneza kosa lolote linalotambuliwa na sheria za nchi hii?
Kama hayo maneno hayatambuliwi kwa mujibu wa sheria, hayawezi kuwa kosa.
Waheshimiwa Majaji, suala hili lilijitokeza kutokana na tuhuma ya upande wa mashtaka wakati wa Preliminary Hearing.
Kwamba hayo maneno yaliyosemwa yalikuwa ni kosa la jinai.
Ukurasa wa 131, Waheshimiwa Majaji.
Wakaona haya maneno yanatengeneza kosa, wakapeleka kwa ZCO, na ZCO akatuleta hapa.
Tuhuma inasema hivi: Kwenye mkutano wa tarehe 03 April 2025, mtuhumiwa alidhihirisha nia yake ya kihaini kwa kusema na kuchapisha maneno yafuatayo.
Wanasema kitu kimoja sahihi hapa. Wanasema hivi: “Msimamo huu unaashiria uasi.” Ni kweli. Ni kweli tunaenda kuhamasisha uasi, tunaenda kukinukisha vibaya sana.
Waheshimiwa Majaji, hakuna mahali popote ambapo upande wa mashtaka wamefafanua haya maneno.
Kwamba kuvuruga uchaguzi maana yake ni nini? Hawajasema kuhamasisha uasi ni nini na kwa nini ni kosa.
Hawajasema kuzuia uchaguzi ni nini na kwa nini ni kosa.
Hawajafafanua “kukinikisha” ni nini na kwa nini ni kosa.
Waheshimiwa Majaji, siyo wajibu wangu mahali popote.
Siyo wajibu wangu kisheria.
Ni wajibu wa upande wa mashtaka kufafanua hayo maneno yana maana gani na kufafanua kwa nini hayo maneno ni kosa.
It’s the question of burden of proof.
The prosecution bears the burden of proof and it never shifts.
Na hawajafafanua hayo maneno; wameleta hisia juu ya hayo maneno.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa upande wa mashtaka juu ya haya maneno upo katika ukurasa wa 146 kwa PW1, ukurasa wa 183 hadi 184 kwa PW2, na ukurasa wa 444 hadi 446 kwa PW16.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE