Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 21,372
- 55,711
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI
SEHEMU YA 2.
**“The failure to lay a name of lawful authority targeted by utterances prejudiced the first accused, upon which it can evaluate if the words in question were calculated to achieve the act or conduct said to be seditious.
The charge was defective.”**
Kwa kifupi, Hati ya Mashitaka inayosema alichochea umma.
Wasafiri, wasio wasafiri, wageni, wenyeji, watoto wachanga — hao wote ni umma.
Huwezi kujitetea kwa hati ya namna hiyo.
Ndiyo maana Mahakama imesema haya maneno yafafanuliwe katika Hati ya Mashitaka.
Yasipofafanuliwa, hayo mashitaka ni batili.
Hati imeingiza neno “umma” ambalo halipo katika sheria, na pili, haijalifafanua.
Kwa sababu hiyo, ni Hati ya Mashitaka batili.
Waheshimiwa Majaji, baada ya kujibu hivyo, naomba sasa nijibu maswali niliyoyaacha jana.
Ukiachilia mbali ubatili wa namna hiyo, je, ushahidi wao unasemaje?
Waheshimiwa Majaji, hapa nazungumzia ushahidi unaohusu nia ya kuchochea umma iliyoletwa na wanaonishitaki.
Ushahidi kuhusu nia ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Na hiyo nia haipo katika sheria.
Je, ushahidi unasemaje kuhusu hiyo nia ya kuzuia umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?
Waheshimiwa Majaji, jambo la kwanza kabisa ni kwamba, katika mashahidi 17 wa upande wa mashtaka walio toa ushahidi kwa kiapo mbele yenu, Waheshimiwa Majaji, ni mashahidi wanne tu ndiyo waliotoa ushahidi kuhusiana na suala hili.
Mashahidi hao ni:
PW1 — ACP George Byagemu
PW2 — Inspector John Kaaya
PW16 — Assistant Commissioner of Police Amin Mahamba
Na PW17 — (shahidi wa gizani).
Hao ndiyo waliotoa ushahidi wa mimi kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu.
Jambo la pili katika ushahidi huu:
Watatu kati ya hao mashahidi wanne ni polisi.
Mmoja tu, PW17, ndiye ambaye hakuwa Polisi.
Watatu kati ya hao wanne hawakuwepo katika huo mkutano; hawakuhudhuria.
Mmoja tu, PW17, ndiye aliyekuwepo katika mkutano.
Waheshimiwa Majaji, PW17 ndiye shahidi pekee katika mashahidi wote 17 ambaye ni eye witness.
Ndiye aliyekuwepo na aliyesikia.
Wengine wote hawakuona wala kusikia yaliyozungumzwa. Waliona tu mambo ya mtandaoni.
Huyo PW17 si tu aliona na kusikia, ndiye aliyerusha matangazo.
Sasa hii inahusu suala ambalo lipo mbele yenu, ambalo ninatuhumiwa kwamba mimi ndiye niliyerusha matangazo ambayo yanadaiwa kuwepo katika mtandao wa Jambo TV.
Waheshimiwa Majaji, kesi ya upande wa mashtaka imejengwa kwenye nini?
Kesi ya upande wa mashtaka imejengwa katika ushahidi wa PW1, PW2 na PW16.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI