Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Nimekusoma miaka mingi sana licha ya kuwa umekuwa mfano lakini leo kwenye wasilisho( final submission) ulilofanya umedhirisha kuwa wewe ni kitabu chema
Kitabu cha kujifunza namna ya kutetea ukweli
Hakika kama Mungu aishivyo hutaanguka bali utaishi kushuhudia ukuu wa Mungu
Wenye utu watasema amina. Na Chacha Heche
1790196479009.jpg
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema kesi inayomkabili ya uhaini katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ni ya kwanza katika historia ya Tanzania ambapo mshtakiwa mmoja anashtakiwa kwa uhaini unaohusishwa na kuitishia Serikali bila kutuhumiwa kumuua Rais au kuipindua Serikali.

Lissu ameyasema hayo leo, Septemba 23, 2026, wakati akiendelea kutoa wasilisho lake la mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.

Katika wasilisho lake, Lissu amesema kesi yake ni ya tatu ya uhaini katika historia ya Tanzania, akizitaja kesi za Grey Likungu Mataka na wenzake ya mwaka 1970 pamoja na kesi ya Khatibu Ghandi na wenzake ya mwaka 1983.

Amesema kesi hizo mbili zilizotangulia zilihusisha washtakiwa wengi na madai ya mipango ya kumuua Rais pamoja na kuipindua Serikali, tofauti na kesi inayomkabili ambayo amesema imefunguliwa chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.

“Tofauti na hizo kesi mbili za mwanzo, hii ya kwangu imefunguliwa kifungu cha 39(2)(d) na uhaini wa hapa ni wa kuitishia Serikali. Hakuna kumuua Rais wala kuipindua Serikali, hii ni kesi ya kwanza,” amesema Lissu.

Lissu pia amesema uamuzi wa Mahakama katika shauri hilo unaweza kuweka msingi wa kisheria utakaotumika katika kesi zinazohusu uhaini nchini kwa miaka ijayo, akitolea mfano kesi ya Grey Likungu Mataka ambayo amesema imeendelea kuwa rejea ya kisheria kwa zaidi ya miaka 50.

“Vyovyote vile mtakavyoamua mtaweka msingi wa kisheria kuhusu uhaini wa kuitishia Serikali.”

Amesema majaji hawataamua tu kuhusu hatima ya mshtakiwa mmoja, bali uamuzi wao unaweza kuwa na athari katika namna sheria kuhusu uhaini wa aina hiyo itakavyotafsiriwa na kutumika siku zijazo“

"You are setting the law for the future,” amesema Lissu, akisisitiza kuwa uzito wa uamuzi huo unakwenda zaidi ya shauri linaloendelea mahakamani.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

TAREHE 24.9.2026

SEHEMU YA 1.

Lissu ameingia, wakafuatia Majaji.

Karani wa Mahakama anajiandaa kusoma kesi Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha Mawakili wenzake.

“Iwapendeze Waheshimiwa Majaji, naitwa Ajuaye Zegeli, nikisaidiana na:

1. Nassoro Katuga — Wakili wa Serikali Mkuu
2. Ignas Mwinuka — Wakili wa Serikali Mkuu
3. Job Mrema — Wakili wa Serikali Mkuu
4. Tawabu Issa — Wakili wa Serikali Mwandamizi
5. Cuthbert Mbilinyi — Wakili wa Serikali
6. Winiwa Kasara — Wakili wa Serikali

Waheshimiwa Majaji, tunaiwakilisha Jamhuri.

Mshitakiwa yupo kizimbani, anajiwakilisha mwenyewe.

Shauri limekuja kwa ajili ya mawasilisho ya upande wa utetezi.

Tupo tayari kuendelea, Waheshimiwa Majaji.”

Jaji Ndunguru: Mshitakiwa?

Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa Jaji.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Nashukuru. Naomba kwanza nikumbushwe niliishia wapi.

Jaji Ndunguru: Ulisema unamaliza kwenye sheria, unaanza kuzungumzia ushahidi sasa. Unakumbuka?

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nashukuru. Kabla sijaendelea na ushahidi, naomba nizungumzie kitu kimoja muhimu ambacho Mahakama hii ilipata kusema kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe.

Kuto kufafanua “Essential Elements” kwenye Hati ya Mashitaka

Mahakama hii, katika kesi ya Freeman Aikael Mbowe, ilikuwa inajadili kushindwa kwa upande wa mashtaka ku-disclose mamlaka halali.

Mamlaka halali maana yake ni nini?

Mahakama hii ilisema katika ukurasa wa 53 wa hukumu:

«“Statutes must give fair notice or warning to those subject to them.

They must guard against arbitrary and discriminatory enforcement and they must not reasonably ...”»

Sheria zinatakiwa kutoa tahadhari sahihi/muafaka kwa wale wanaotegemewa kuzifuata.

Ziwalinde watu dhidi ya mamlaka holela/matumizi holela ya madaraka yanayotumiwa na sheria.

Na sheria zisinyime watu uhuru wa kuzungumza. Isipolinda wote, tutakuwa wafungwa.

Mahakama ilisema yafuatayo kuhusu sheria za aina hii:

«“Such statutes must be under the doctrine of overbreadth.”»

«“If the statute is so overbroadly written that it could chill free speech, then it can be struck down because of its chilling effects.”»

Maana ya Overbreadth Doctrine ipo katika kamusi ya Black’s Law, toleo la saba.

Kesi ya Freeman Aikael Mbowe ilimalizia kwa maneno haya ukurasa wa 58.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1. TAREHE 24.9.2026

MAHAKAMA INAANZA VERY SOON

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Back
Top Bottom