Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Si sheria imeniweka gerezani, ni mama .Mama akiongea nitatoka , Sasa October 29 inahusiana aje na chama changu . Mama kama unanipenda wacha kunitesa! Mke na watoto wananihitaji nyumbani 🇹🇿 #duniadarubini #swahilitime
1781015528730.jpg
 
BREAKING NEWS

Mahakama imesogeza tarehe ya kesi ya Lissu hadi tarehe 3 Julai!!!!
Kwa nini dakika za mwisho na mbali hivi!?
Ule mpango wa kumpa sumu mmeona akitoka kesho mtashindwa kutimiza?! Hii mbaya sana Mahakama mnaendelea kuahirisha uhuru wa Lissu!
1781097692178.jpg
 
Barua kutoka Jukwaa la Wanademokrasia wa Afrika kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, 4 Mei 2026

HE Shirley Ayorkor Botchwey

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola KWA PEPE

Ndugu Katibu Mkuu

Demokrasia nchini Tanzania

Barua zetu za tarehe 23 Februari 2026 na 23 Machi 2026 zinarejelea.

Tumezingatia ziara ya hivi karibuni ya Mheshimiwa Lazarus Chakwera kama Mjumbe Maalum wa Jumuiya ya Madola katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapongeza hatua hii katika kujaribu kutafuta njia ya kuelekea kuanzishwa tena kwa demokrasia na utawala wa sheria nchini humo. Ili kukumbusha, mwishoni mwa ziara yake mwezi Aprili, Mjumbe huyo alisema: 'Ingawa ninatarajia matokeo ya Tume Huru ya Uchunguzi katika siku zijazo, pia ninaungana na Watanzania katika imani yao kwamba kazi ya kujenga amani na ustawi wa kudumu itahitaji msingi wa nia njema, heshima ya pande zote, na kujitolea kwa ukweli na uwajibikaji, mazungumzo ya wazi na yenye kujenga, haki na maridhiano, na michakato ya kidemokrasia iliyo wazi na jumuishi kwa ajili ya kufanya mageuzi.'

Kuna hatari kubwa kwamba ziara hii itaipa serikali jani la heshima badala ya kichocheo cha mageuzi. Hasa, tungeomba mtumie ofisi zenu nzuri kutangaza hadharani kile kinachoitwa Ripoti ya Chande kuhusu vurugu za kisiasa zilizofuata uchaguzi mwaka jana. Hadi hilo litokee, ripoti na matokeo yake yanaweza kuwa mada ya udanganyifu, taarifa za uongo na kejeli, na hayawezi kutoa msingi wa mashauriano na mjadala wa umma. Hii ni hasa ikizingatiwa kwamba upande mmoja tu ndio umeunda timu iliyo nyuma ya Ripoti hii.

Hakuna mapambano yanayoweza kushindwa kwa nguvu za silaha pekee. Yatasimamiwa tu kupitia maelewano ya kisiasa. Maslahi ya uongozi lazima yawe ya pili kwa maslahi ya serikali, na yanatawala tu kulingana na mapenzi ya watu wote.

Kwa hivyo tunawaomba muuombe uongozi wa Tanzania kurekebisha mazingira ya kisiasa kwa kumwachilia Tundu Lissu kutoka gerezani na kupunguza vikwazo vyote kwa wanachama wa upinzani bila masharti. Huwezi kuzungumzia amani wakati unapigana vita. Kama Nelson Mandela alivyosema, haiwezekani kufikiria, sembuse kufanya mazungumzo ya kisiasa, ukiwa gerezani au ukiwa mahakamani.

Amani, nakumbusha, ni usemi wa mahusiano ya madaraka. Haiwezekani kushughulikia amani moja kwa moja bila diplomasia kuzingatia hali zinazounda mahusiano haya.

Tunatarajia kusikia kutoka kwako. Wako katika demokrasia

Imesainiwa kwa niaba ya Jukwaa la Wanademokrasia wa Afrika

Seretse Khama Ian Khama

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Botswana

MWISHO
1781581633012.jpg
 
Bunge la Umoja wa Ulaya (MEPs) limepitisha maazimio mapya na mazito yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu duniani, likiitaka Serikali ya Tanzania kumuachia huru mara moj Mwenyekiti wa CHADEMA, Taifa Tundu Lissu, huku likilaani vikali vitendo vya Urusi kuwateka watoto wa Ukraine.

Katika azimio lake la kwanza lililopitishwa kwa kunyoosha mikono mjini Brussels, Bunge hilo limeeleza wasiwasi mkubwa juu ya mashtaka yanayomkabili Tundu Lissu ambayo yanaweza kupelekea adhabu ya kifo, likiyataja kama yenye misingi ya kisiasa. Wabunge hao wamehimiza mamlaka za Tanzania kurejesha ushiriki kamili wa CHADEMA kuelekea uchaguzi na kukomesha ukandamizaji dhidi ya wapinzani, wanaharakati, na waandishi wa habari.

Kuhusu Urusi, Bunge la Ulaya limelaani vikali kile likichokiita "mkakati wa mauaji ya kimbari" (genocidal strategy) unaoungwa mkono na Belarus, unaolenga kufuta utambulisho wa Ukraine kupitia uhamishaji na uandikishaji wa lazima wa watoto wa Kiukraine kwenda Urusi, likitaka watoto hao warudishwe mara moja.

"Bunge la Ulaya linasisitiza kuwa makubaliano yoyote ya amani ya kweli lazima yahusishe kurudishwa kwa watoto hawa na uwajibikaji wa kisheria kwa wale wote waliohusika na uhamishaji huu wa nguvu," inaeleza sehemu ya azimio hilo lililopitishwa kwa kura 516.

Aidha, katika azimio la tatu, wabunge hao wametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu kifo cha kiongozi wa kidini wa Kibudha nchini Tibet, Tulku Hungkar Dorje, wakilaani vikali ukandamizaji unaofanywa na mamlaka za China dhidi ya uhuru wa kuabudu.

#SasaLive #BungeLaUlaya #TunduLissu #Tanzania #Urusi Ukraine Tibet HakiZaBinadamu HabariZaKimataifa
1782335684804.jpg
 
Lisu kwa kumuangalia macho yake na hayo mashavu yake ya kitapeli

Unajua kabisa huyu ni mtu na hila nyingi

Ikiwa huyu asiye na Elimu hiyoo bado back up imara hivi japo anga limechafuka na nyufa zinaonekana

Hivi akipata mtu kama huyu na akapita wasiwasi anaopitia huyu.! Na Akawa na wakumwezesha katika hilo

Hivi mmewaza Kuna Rangi ngapi hatujaona bado wala kuhisi uwepo wake.!

Mpaka mkienda Kupuu itatakiwa muongozo wa kikatiba
 
TUNDU LISSU KUPELEKWA DODOMA KESHO!

Wakili wa Tundu Lissu, Paul Kisabo ameandika kuwa Tundu Lissu atawahoji Mkuu wa Gereza la Ukonga na Kamishna Mkuu wa Magereza katika kesi ya kikatiba ya namba 7300/2026.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar Es Salaam; 30 Juni 2026; Saa 11:15 jioni

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Tundu Lissu, atawahoji kwa maswali ya dodoso Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga tarehe 1 hadi 3 Julai 2026 katika Shauri la Kikatiba Na. 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.

Shauri hilo lilifunguliwa na Mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga. Katika shauri hilo, Mahakama inaombwa kuamua kuhusu masuala mbalimbali ya kikatiba yanayohusu vikwazo vya Jeshi la Magereza dhidi ya Mhe. Tundu Lissu, mawakili wake, ndugu, viongozi na wanachama wanaomtembelea gerezani.

Miongoni mwa masuala yanayolalamikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa viongozi na wanachama kumuona Mhe. Lissu gerezani, pamoja na vitendo vya askari wa magereza vya kusikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Lissu na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria, jambo ambalo linakiuka haki ya faragha na haki ya mawakili kufanya kazi yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

Aidha, kutokana na uzoefu wao wa kukumbana na changamoto hizo wanapomtembelea Mhe. Lissu gerezani kwa ajili ya mashauriano ya kisheria, Mhe. Lissu anatarajiwa pia kuwahoji mawakili waliofungua shauri hilo ili waweze kuieleza Mahakama kuhusu mazingira halisi wanayokumbana nayo wanapotekeleza wajibu wao wa kitaaluma.

Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha na Mhe. Jaji Dkt. Longopa. Shauri hili ni miongoni mwa mashauri muhimu ya kikatiba yanayoweza kuweka mwelekeo wa kisheria kuhusu haki ya mawakili kufanya mashauriano ya faragha na wateja wao waliopo mahabusu au gerezani, pamoja na kulinda misingi ya haki ya kupata msaada wa kisheria na usiri wa mawasiliano kati ya wakili na mteja.

Paul Kisabo,
Wakili; 30 JUNI 2026
1782870931354.jpg
 
TAARIFA KWA UMMA

Siku ya leo kwa wale ambao mnataka kufuatilia kesi ya Mhe. Lissu dhidi ya Mkuu wa Gereza la Ukonga na Kamishna Mkuu wa Magereza itakuwa LIVE kupitia link hii 👇


Before Hon. Mruma,
Dr Rumisha ,Dr Longopa,JJJ’s

Miscellaneous Civil Cause 7300/2026

Kulwa William Maduhu and 2 others
VS
The Attorney General and 4 others

Mention

at 09:00 am

DATE: 01/7/2026

Jinsi ya kujoin Ukibofya hiyo link itakwambia allow virtualcourt.judiciary to use microphone bofya don’t allow.

Then utaona add your name utaweka jina lako

Then utabofya Join meeting l

Itakupeleka moja kwa moja kwenye kesi
1782915679879.jpg
 
🔥LISSU HAPOI‼️
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, anatarajiwa kuwahoji kwa maswali ya dodoso (cross-examination) Kamishna Mkuu wa Magereza pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga katika Shauri la Kikatiba Namba 7300 la Mwaka 2026 mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma.

Mnyukano huo wa kisheria utaanza kesho Julai 1 hadi Julai 3, 2026. Shauri hilo litasikilizwa kwa njia ya mtandao (online) mbele ya jopo la majaji watatu; Mhe. Jaji Mruma, Mhe. Jaji Dkt. Rumisha, na Mhe. Jaji Dkt. Longopa.

Shauri hilo lilifunguliwa na mawakili Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu, na Paul Kisabo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza, na Mkuu wa Gereza la Ukonga, wakiiomba mahakama kuamua kuhusu ukiukwaji wa misingi ya kikatiba gerezani.
Miongoni mwa mambo makuu yanayolalamikiwa ni pamoja na viongozi na wanachama kuzuiwa kumuona Lissu, pamoja na vitendo vya askari magereza vya kusikiliza mazungumzo ya siri kati ya mwanasiasa huyo na mawakili wake wanapofanya mashauriano ya kisheria—jambo linalokiuka haki ya faragha.

#FreeTunduLissu

‼️🚨TUNDU LISSU UPDATE‼️

The Chairman of CHADEMA, Tundu Lissu, is expected to cross-examine the Commissioner General of Prisons and the Warden of Ukonga Prison in Constitutional case No. 7300 of 2026 before the High Court of Tanzania, in Dodoma. The case was opened by lawyers Kulwa Maduhu, Nashon Nkungu, and Paul Kisabo against the Attorney General, the Commissioner General of Prisons, and the Warden of Ukonga Prison, requesting the court to decide on the violation of constitutional principles in the prison.
Among the main issues complained about are leaders and members of CHADEMA being prevented from seeing Lissu, as well as the eavesdropping of prison guards —listening to confidential conversations between Lissu and his lawyers when they are conducting legal consultations—a violation of the right to privacy.
European Parliament David McAllister
1782915909275.jpg
 
Tunapenda kuwajulisha mabadiliko ya ukumbi wa usikilizaji wa kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, SC Tundu A.M Lissu, inayotajwa leo asubuhi.

Kesi hii itaanza saa 3:00 Asubuhi, katika ukumbi Namba 1, Mahakama Kuu (Masjala Ndogo) – Dar es Salaam (pale tumekuwa tukikutana mara zote).

Sababu za mabadiliko ya ukumbi; Ukumbi wa Mahakama ya Rufaa (Kivukoni) uliokuwa umepangwa awali ni mdogo na hauwezi kutosheleza umati.

Pia, Tundu A.M Lissu aligoma kuandika majina ya watu 40 tu (viongozi na watu wa karibu) ambao ndiyo pekee wangeruhusiwa kuingia mahakamani.

Ukumbi wa Mahakama ya Rufani Tanzania (Kivukoni) ni mdogo sana usioweza kuhimili watu wengi kwa pamoja kama ilivyo ukumbi wa Mahakama Kuu.

“Siwezi kufanya hivyo. Nataka kesi iende kwenye eneo la wazi na pana ili wananchi na wapenda haki waje kusikiliza kwa uhuru.” – Tundu A.M Lissu

Mahakama ya Rufaa Tanzania imesikia maombi hayo na kuamua kukubali na kuuleta mtanange huo wa sheria
20260703_115018.jpg
 
Back
Top Bottom