SoC02 Tunaweza kupitia njia zifuatazo kuepuka changamoto ya ukosefu wa ajira kuwa kubwa sana ili kuimarisha uchumi wetu

Stories of Change - 2022 Competition

Dat4

Member
Aug 24, 2022
96
148
Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wanapaswa kuchukua hatua endelevu kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ili kukuza uchumi.

UKOSEFU WA AJIRA NI NINI?
- Ni ile hali ya mtu kutafuta kazi/ajira bila kuipata.
images.png
Tanzania unemployment rate (www.theglobaleconomy.com)

Ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto ambazo hutokea ulimwenguni kote lakini huzidiana ukubwa wa tatizo.
Hali ya ukosefu wa ajira katika taifa ndiyo hupima afya ya uchumi wa nchi husika.

Ripoti zinaonyesha uwiano uliopo kati ya waombaji wa ajira na nafasi za ajira zilizopo kuna utofauti mkubwa sana, wapatao ajira kila mwaka ni chini ya asilimia 15% ya waombaji wenye vigezo.
Jitihada zinatakiwa kufanyika ili kupunguza tatizo hili hasa kwa vijana ambao ndio wahanga wakubwa na ndio injini ya ukuzaji wa uchumi wa nchi.

Taifa linapaswa kuwa na mijadala mipana juu ya tatizo hili ambalo linazidi kukua kwa kiasi kikubwa, kwa sasa tatizo ni kubwa je vipi kwa miaka 20 ijayo hali itakuaje?

Tunaweza kuzingatia mambo yafuatayo katika kutafuta ufumbuzi:-

(i) Kubadili kabisa mifumo ya elimu tuliyonayo!
- Mifumo ya elimu ndiyo muelekeo wa uchumi wa nchi, uchumi wa nchi hauwezi kuwa imara endapo kuna tatizo kubwa la ukosefu wa ajira!
mtakubali kuwa ni wakati sasa kama taifa lenye malengo ya kupiga hatua yatupasa kuwa na uthubutu wa kubadili mifumo yetu mizima ya elimu,
swala hili limezungumziwa sana lakini limekua halipatiwi ufumbuzi, ni wakati sasa tuamue, mfumo wa elimu ni wa zamani sana na unachangia kuzalisha tatizo la ukosefu wa ajira, mfumo huu unamuandaa mhitimu zaidi ya 80% kuajiliwa na hapa ndipo hukuta wahitaji wa ajira ni wengi sana kuliko soko la ajira lililopo,
Tufumue na kufuma upya hicho ndio kiini cha ufumbuzi wa tatizo la ajira

(ii) Kuweka sera nzuri na kuwasapoti wanaojiajiri!
- Wengi wameshindwa kujiajiri na kufanya shughuli za uzalishaji uchumi kutokana na sera mbovu zinazowabana,
taifa linabidi kuweka sera nzuri kwa vijana hususa wale wanaoingia kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa kujiajiri, utitili wa kodi unasababisha wengi kushindwa na kuamua kusubiri ajira za kuajiriwa maana huko ndiko kwenye unafuu,

Mwaka 2018 nilipohitimu chuo nilianzisha blogu ya burudani! nilipanga niiendeleze mpaka nipate uwezo wa kuajiri watu wengine nilianza taratibu na nilikua nimeanza kupata kipato japo kidogo sana ilikua inaniingizia kama elfu 90 kwa mwezi, nilipanga kuwa baada ya miaka kadhaa iwe blogu kubwa sana nipate mpaka studio, sikua nawaza swala la kuajiliwa na mtu mawazo yangu yalikua huko lakini baada ya muda mfupi serikali ikaja na sheria ya kuwa kuchapisha maudhui mtandaoni na kuendesha channel youtube lazima uwe na leseni, kupata leseni ilikua si chini ya milioni moja! na walikua serious haijalishi blog yako ina miaka 10 au mwezi mmoja nyote mnalipa kiasi sawa, na wengi walioshindwa kulipa na kuendelea kuchapisha maudhui walifunguliwa mashtaka,
ilikua ni ngumu kwangu na ikanibidi nifunge blogu na ndoto zikaishia hapo nikaanza kuwaza kuajiliwa,

hii ni moja ya sera iliyowafanya watu wengi sana ikiwemo mimi kushindwa kujiajiri na kutegemea ajira za kuajiliwa na kuongeza zaidi tatizo la ukosefu wa ajira nchini,
zipo sera nyingi sana sio rafiki zinawakatisha tamaa vijana kujiajiri na kusababisa wengi kusubiri kuajiliwa

(iii)Taifa kuongeza uzalishaji!
- Taifa lenye lengo la kutatua tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana ni muhimu tujikite katika uzalishaji wenye kuleta tija, tusijikite zaidi katika utumiaji bila uzalishaji, kwa mfano tukiacha maneno mengi na tukajikita zaidi katika kilimo kwa vitendo tunaweza kuvutia vijana wengi wengi kujiajiri na kupitia sekta hii tukatengeneza ajira nyingi sana, mfano sera ya kilimo kwanza iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt Jakaya Kikwete kama ingetiliwa maanani kwa vitendo, ingewavutia vijana wengi na ingeongeza wigo mpana kujiajiri na kutengeneza ajira nyingi! sijui ile sera iliishia wapi lakini kiujumla ni kama ilifeli, na hii ni kutokana na kuwa na mipango na sera zisizo endelevu!

Mfano mzuri ni kuwa Nchi yetu ina ardhi kubwa sana na ina rutuba lakini kuna viwanda vingi tu vinaagiza ngano kutoka nje ya nchi hadi ulaya na hii ni kwasababu uzalishaji kwetu bado sio kipaumbele sana, Kuna kiwanda fulani (jina kapuni) nilishuhudia kinaagiza mtama kutoka nchi ya zimbabwe na zambia, je sisi kama nchi tumeshindwa kufanya uzalishaji wa mazao haya mpaka kuagiza ughaibuni? Je, bajeti ya kilimo inakidhi mahitaji ya watumiaji bidhaa za kilimo? Je, sekta ya kilimo ina msaada gani kwa vijana?

Je, kwanini tumejikita zaidi kwenye jembe la mkono na sio large scale agriculture na hufanywa mara nyingi na wale ambao sio wasomi? je hatuoni tatizo hapo?

(iv) Kuongeza na Kuimarisha viwanda.
- Sera ya Tanzania ya viwanda yapaswa kutazamwa upya, kimsingi ni sera nzuri sana kama ikitiliwa maanani, sera hii inapaswa kuboreshwa sambamba na kuweka mikakati mbalimbali katika kufanya mapinduzi ya viwanda.
Uimarishwaji na uongezaji wa viwanda ni uzalishaji wa ajira, sambamba na ukuaji wa uchumi,
ukuaji wa uchumi huenda sambamba na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, je kuna sera nzuri zinazovutia uanzishwaji wa viwanda?, je kama taifa tunavyo viwanda vingapi? je vinatosheleza kulingana na idadi ya watu tulionao? Je, upo mkakati gani wa kuwawezesha wenye viwanda vidogovidogo?
Je, gharama za usajili wa viwanda vidogovidogo pamoja na makadirio ya kodi ni rafiki kwa vijana wanaotaka kujiajiri? ikumbukwe tukiwa na sera nzuri za kuthamini viwanda vidogo vidogo pamoja na kuvitambua kupitia mashindano na kuwapa tuzo na sapoti washindi mbalimbali tunaweza kuwainua vijana na kuwapa molari na hii itawavutia vijana wengi wenye fani mbalimbali kuvutika kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa kiasi kikubwa.

(v) Kukontroo uzalianaji bila mpango (Population control)
- Taifa linalokuwa na wingi wa watu zaidi (overpopulation) husababisha hali ya ukosefu wa ajira kuwa kubwa na hivyo taifa hilo huitaji sera nzuri na mikakati mizuri ya kuimarisha uchumi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linalopelekea (jobless) kuwa wengi na endapo tatizo la ajira linapokuwa kubwa hupelekea uhalifu kuzidi kama vile kuongeza wezi na waasi, ni vyema taifa kutunga sera za kukontroo uzalianaji usio na mpango na sera hizi ziwe endelevu kwaajili ya vizazi vya baadaye

Hizo ni miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kukabili swala la ukosefu wa ajira nchini ili kukuza uchumi kwa kasi!

Nawasilisha Karibuni!!
 
Unahisi ivi vitu vinaeweza kufanyiwa kazi na unahis inawezwkana tuachane na competition nambie tyu ukweli
 
Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wanapaswa kuchukua hatua endelevu kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ili kukuza uchumi.

UKOSEFU WA AJIRA NI NINI?
- Ni ile hali ya mtu kutafuta kazi/ajira bila kuipata.
View attachment 2333626Tanzania unemployment rate (www.theglobaleconomy.com)

Ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto ambazo hutokea ulimwenguni kote lakini huzidiana ukubwa wa tatizo.
Hali ya ukosefu wa ajira katika taifa ndiyo hupima afya ya uchumi wa nchi husika.

Ripoti zinaonyesha uwiano uliopo kati ya waombaji wa ajira na nafasi za ajira zilizopo kuna utofauti mkubwa sana, wapatao ajira kila mwaka ni chini ya asilimia 15% ya waombaji wenye vigezo.
Jitihada zinatakiwa kufanyika ili kupunguza tatizo hili hasa kwa vijana ambao ndio wahanga wakubwa na ndio injini ya ukuzaji wa uchumi wa nchi.

Taifa linapaswa kuwa na mijadala mipana juu ya tatizo hili ambalo linazidi kukua kwa kiasi kikubwa, kwa sasa tatizo ni kubwa je vipi kwa miaka 20 ijayo hali itakuaje?

Tunaweza kuzingatia mambo yafuatayo katika kutafuta ufumbuzi:-

(i) Kubadili kabisa mifumo ya elimu tuliyonayo!
-Mifumo ya elimu ndiyo muelekeo wa uchumi wa nchi, uchumi wa nchi hauwezi kuwa imara endapo kuna tatizo kubwa la ukosefu wa ajira!
mtakubali kuwa ni wakati sasa kama taifa lenye malengo ya kupiga hatua yatupasa kuwa na uthubutu wa kubadili mifumo yetu mizima ya elimu,
swala hili limezungumziwa sana lakini limekua halipatiwi ufumbuzi, ni wakati sasa tuamue, mfumo wa elimu ni wa zamani sana na unachangia kuzalisha tatizo la ukosefu wa ajira, mfumo huu unamuandaa mhitimu zaidi ya 80% kuajiliwa na hapa ndipo hukuta wahitaji wa ajira ni wengi sana kuliko soko la ajira lililopo,
Tufumue na kufuma upya hicho ndio kiini cha ufumbuzi wa tatizo la ajira

(ii) Kuweka sera nzuri na kuwasapoti wanaojiajiri!
- Wengi wameshindwa kujiajiri na kufanya shughuli za uzalishaji uchumi kutokana na sera mbovu zinazowabana,
taifa linabidi kuweka sera nzuri kwa vijana hususa wale wanaoingia kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa kujiajiri, utitili wa kodi unasababisha wengi kushindwa na kuamua kusubiri ajira za kuajiriwa maana huko ndiko kwenye unafuu,

Mwaka 2018 nilipohitimu chuo nilianzisha blogu ya burudani! nilipanga niiendeleze mpaka nipate uwezo wa kuajiri watu wengine nilianza taratibu na nilikua nimeanza kupata kipato japo kidogo sana ilikua inaniingizia kama elfu 90 kwa mwezi, nilipanga kuwa baada ya miaka kadhaa iwe blogu kubwa sana nipate mpaka studio, sikua nawaza swala la kuajiliwa na mtu mawazo yangu yalikua huko lakini baada ya muda mfupi serikali ikaja na sheria ya kuwa kuchapisha maudhui mtandaoni na kuendesha channel youtube lazima uwe na leseni, kupata leseni ilikua si chini ya milioni moja! na walikua serious haijalishi blog yako ina miaka 10 au mwezi mmoja nyote mnalipa kiasi sawa, na wengi walioshindwa kulipa na kuendelea kuchapisha maudhui walifunguliwa mashtaka,
ilikua ni
ngumu kwangu na ikanibidi nifunge blogu na ndoto zikaishia hapo nikaanza kuwaza kuajiliwa,

hii ni moja ya sera iliyowafanya watu wengi sana ikiwemo mimi kushindwa kujiajiri na kutegemea ajira za kuajiliwa na kuongeza zaidi tatizo la ukosefu wa ajira nchini,
zipo sera nyingi sana sio rafiki zinawakatisha tamaa vijana kujiajiri na kusababisa wengi kusubiri kuajiliwa

(iii)Taifa kuongeza uzalishaji!
-Taifa lenye lengo la kutatua tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana ni muhimu tujikite katika uzalishaji wenye kuleta tija, tusijikite zaidi katika utumiaji bila uzalishaji, kwa mfano tukiacha maneno mengi na tukajikita zaidi katika kilimo kwa vitendo tunaweza kuvutia vijana wengi wengi kujiajiri na kupitia sekta hii tukatengeneza ajira nyingi sana, mfano sera ya kilimo kwanza iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Dkt Jakaya Kikwete kama ingetiliwa maanani kwa vitendo, ingewavutia vijana wengi na ingeongeza wigo mpana kujiajiri na kutengeneza ajira nyingi! sijui ile sera iliishia wapi lakini kiujumla ni kama ilifeli, na hii ni kutokana na kuwa na mipango na sera zisizo endelevu!
Mfano mzuri ni kuwa Nchi yetu ina ardhi kubwa sana na ina rutuba lakini kuna viwanda vingi tu vinaagiza ngano kutoka nje ya nchi hadi ulaya na hii ni kwasababu uzalishaji kwetu bado sio kipaumbele sana, Kuna kiwanda fulani (jina kapuni) nilishuhudia kinaagiza mtama kutoka nchi ya zimbabwe na zambia, je sisi kama nchi tumeshindwa kufanya uzalishaji wa mazao haya mpaka kuagiza ughaibuni? je, bajeti ya kilimo inakidhi mahitaji ya watumiaji bidhaa za kilimo? je, sekta ya kilimo ina msaada gani kwa vijana?
je, kwanini tumejikita zaidi kwenye jembe la mkono na sio large scale agriculture na hufanywa mara nyingi na wale ambao sio wasomi? je hatuoni tatizo hapo?

(iv) Kuongeza na Kuimarisha viwanda.
- Sera ya Tanzania ya viwanda yapaswa kutazamwa upya, kimsingi ni sera nzuri sana kama ikitiliwa maanani, sera hii inapaswa kuboreshwa sambamba na kuweka mikakati mbalimbali katika kufanya mapinduzi ya viwanda.
Uimarishwaji na uongezaji wa viwanda ni uzalishaji wa ajira, sambamba na ukuaji wa uchumi,
ukuaji wa uchumi huenda sambamba na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, je kuna sera nzuri zinazovutia uanzishwaji wa viwanda?, je kama taifa tunavyo viwanda vingapi? je vinatosheleza kulingana na idadi ya watu tulionao? Je, upo mkakati gani wa kuwawezesha wenye viwanda vidogovidogo?
Je, gharama za usajili wa viwanda vidogovidogo pamoja na makadirio ya kodi ni rafiki kwa vijana wanaotaka kujiajiri? ikumbukwe tukiwa na sera nzuri za kuthamini viwanda vidogo vidogo pamoja na kuvitambua kupitia mashindano na kuwapa tuzo na sapoti washindi mbalimbali tunaweza kuwainua vijana na kuwapa molari na hii itawavutia vijana wengi wenye fani mbalimbali kuvutika kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa kiasi kikubwa.

(v) Kukontroo uzalianaji bila mpango (Population control)
- Taifa linalokuwa na wingi wa watu zaidi (overpopulation) husababisha hali ya ukosefu wa ajira kuwa kubwa na hivyo taifa hilo huitaji sera nzuri na mikakati mizuri ya kuimarisha uchumi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linalopelekea (jobless) kuwa wengi na endapo tatizo la ajira linapokuwa kubwa hupelekea uhalifu kuzidi kama vile kuongeza wezi na waasi,
ni vyema taifa kutunga sera za kukontroo uzalianaji usio na mpango na sera hizi ziwe endelevu kwaajili ya vizazi vya baadaye

Hizo ni miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kukabili swala la ukosefu wa ajira nchini ili kukuza uchumi kwa kasi!

Nawasilisha Karibuni!!
Great
 
Back
Top Bottom