Ukosefu wa ajira: Upepo wanaoutumia sekta binafsi

Quartz360

Senior Member
Mar 27, 2023
124
302
Tatizo la ukosefu wa ajira limekuwa ni kilio kwa vijana walio wengi, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa ni asilimia kumi 10% tu ya wahitimu huweza kupata ajira rasmi kila mwaka. Huku asilimia 90% wakibaki bila ajira rasmi.

Tatizo hilo limeibua fursa kwa upande wa makampuni, Biashara binafsi, NGOs na mashirika. Ambapo kwa kiasi kikubwa wamekuwa hawatoi ajira tena badala yake wanatembea na kile wanachokiita VOLUNTEERING na INTERNSHIPS.

Kwa malipo kiduchu ama hakuna kabisa ukilinganisha na kazi wanazofanya vijana hao. Na hilo limefanya vijana wengi wasiwe na chaguo, badala yake wanaona ni bora wakafanye hizo Internships ama kujitolea ili tu siku ziende kwa kuwa ajira imekuwa ni kilio cha taifa.

Mbaya zaidi waajiri wao pia wamekuwa na kiburi kwa sababu vijana wako wengi mtaani, anaweza kukufukuza leo, kesho akapata mwingine.

Very Sad.
 
Makanisa yanaongezeka nchini kwa speed kubwa kuliko viwanda.
Shame upon us TANZANIA
 
Mbele kuna giza kubwa sana nchi inababaika kupata hela inawabana waliojiajiri sector binafsi ili kupata hela za kuwalipa walioajiriwa serikalini.
MSIZALIANE HOVYO JAMANI MBELENI WATOTO WETU WATATUZEEKEA MAJUMBANI KWETU.
ITAFIKA MUDA WATOTO WATATAMANI WAZAZI WAFE/AU KUTUUA KABISA ILI WARITHI MALI ZA WAZAZI.
 
Back
Top Bottom