Changamoto ya ajira kwa vijana

Nafaka Store

Member
Feb 24, 2024
7
3
Unadhani kuwa na elimu ya juu ni kigezo kitakachokusaidia kupata ajira? Tunasisitizwa kuhusu elimu, lakini kwa nini mwenye elimu ya juu zaidi hapati ajira?

Wanaogopa kumuajiri kwamba atakuwa juu zaidi yao au wanaogopa atatakiwa kulipwa mshahara mkubwa wasioumudu?

Watu wana elimu za juu lkn kupata ajira ni kitendawili lkn utashangaa ofisi nyingi wanaajiriwa Bsc holders, wenye diploma n.k. Je ufaulu ni kigezo mbadala kwamba MSc holder ana GPA ndogo?

Na je vijana tunashindwa kujiunga na kudevelop business idea itakayotukwamua kutoka kwenye wimbi la ukosefu wa ajira? Kidole kimoja hakivunji chawa, umoja ni nguvu. Je tumepotezeana imani, hatuaminiani? Je mitaji hatuna? Hamna vyanzo vya kupata mitaji? Hatuna ideas?
 
Watu wamekalili kusoma hadi chuo ili utoboe! Sio kila mtu asome mpaka chuo ili aajiliwe! Japo kama fursa ya kusoma hadi chuo hipo, basi soma lakini sio ili uajiliwe! Tumia vipawa Mungu alivyokuumba navyo kukuwezesha kujitambua na kuona fursa kwa kutumia elimu uliyoipata ili utoboe! Ni aibu graduate kulialia kuajiliwa! Peleka akili kazini!
Jamii inashangaa kuona graduate mzima anakosa shughuli za kumuingizia kipato na kulialia mitaji! Mtaani laki moja ni mtaji tosha kuanza biashara hela ambayo ulikuwa unaipata ulipokuwa Chuo. Shida vijana hawajielewi na hawajui wanachokitaka!
 
Mtawasema sana graduates, and guess what? Bado tupo kwenye vicious cycle.. Serikali inabidi kubeba lawama kwa hili. Kama hamna total overhaul kwenye sekta elimu na multisectoral usitegemee muujiza. Graduates mnawafanya punching bag . Je kiini cha haya yote mnakijua?
 
Mafanikio unaza na mindset kuna watu walisoma mambo amabyo hayapo kisa tu walimsikia mwanasiasa wa ccm kasema hizo course ndo zinasoko .

Njia za kupunguza tatizo la Ajira ni MTU kusoma kitu ambacho anakipenda na sio kuwa chini ya mwanasiasa.

Kuiboresha Elimu iwe na skills na maarifa mtambuka. Yakunoa ufahamu Wa MTU.
 
Unadhani kuwa na elimu ya juu ni kigezo kitakachokusaidia kupata ajira? Tunasisitizwa kuhusu elimu, lakini kwa nini mwenye elimu ya juu zaidi hapati ajira?

Wanaogopa kumuajiri kwamba atakuwa juu zaidi yao au wanaogopa atatakiwa kulipwa mshahara mkubwa wasioumudu?

Watu wana elimu za juu lkn kupata ajira ni kitendawili lkn utashangaa ofisi nyingi wanaajiriwa Bsc holders, wenye diploma n.k. Je ufaulu ni kigezo mbadala kwamba MSc holder ana GPA ndogo?

Na je vijana tunashindwa kujiunga na kudevelop business idea itakayotukwamua kutoka kwenye wimbi la ukosefu wa ajira? Kidole kimoja hakivunji chawa, umoja ni nguvu. Je tumepotezeana imani, hatuaminiani? Je mitaji hatuna? Hamna vyanzo vya kupata mitaji? Hatuna ideas?
Waendeshe BODABODA ndio Ajira ccm imewaandalia
 
Kua na degree ni security katika mengi,ukimaliza level hii kunatakataka kichwani sinapelekwa dampoo zisichanganyikane tena na akili. No matter what you have to struggle!!
 
Wanaofanya siasa namizaha kwenye hili ni vyema wakatafakari upya maana mwisho wa siku mchuma janga atakula na mkewe au mumewe na watoto hao wapambe watabaki kukuchora huku wakichoma nyama.

Najua vichwani mtajiuliza huyu anamaana gani au ana wazimu gani. Binafsi kwa hesabu yaharaka niliyonayo kuna vijana kwa makumi waliijiua kwa kukosa msaada ktk hili, na mamia walioharibikiwa futures..
Ni kosa kubwa kwa serikali yetu pendwa kuruhusu siasa kwenye injini ya Taifa.

Kama kijana mmoja angeharibikiwa kwa upuuzi na utendaji mbovu wa Taasisi au sekta fulani basi wajue watajibu siku moja.

Na sishangai kuona baadhi ya vigogo wakifa au kuishia kwenye maisha ya taabu badala ya kuwa na uzee mwema.

Hakuna dhamiri ngumu na yakuumiza kama ulikuwa na nguvu ya kufanya lolote maishani kisha unaishia kusulubiwa kwa kuona maisha yako na kizaz chako yanaoza huku huwezi kufanya lolote, unaungua kwa kutizama na kuteseka mpk unaku fa.

Nchi ninayoishi ni hapa hapa Africa ila wanalipa 150$ kwa vijana wao haswa waliosoma lkn hawana ajira. Nimejiuliza sana kwani hawa kama si wajibu wao au ni ttz la dunia nzima je wanajipendekeza kwa wananchi au wanatafuta nn???

What goes around comes around.
 
Back
Top Bottom