Tumeandaa AFCON sawa, nchi ipi kati ya Kenya, Uganda na Tanzania itatoa timu mwenyeji wa mashindano?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Kenya Uganda na Tanzania zimepewa nafasi ya kuandaa kwa pamoja fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2027 baada ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) kutangaza kuwa ombi lao pa pamoja limeshinda dhidi ya maombi ya Algeria, Misri na Botswana ambazo nazo ziliomba.

Kwa kawaida utaratibu jinsi ulivyo, ni kwamba nchi mwenyeji hupewa fursa kwa timu yake kukata tiketi ya moja kwa moja kushiriki.

Sasa kwa hizi nchi tatu ni ipi itatoa mwenyeji au zote zitapata nafasi hiyo, utaratibu kwa nchi tatu ukoje?
 
Na nchi gani itakayo andaa fainali ya mwisho?!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Tanzania ndio itaandaa kulingana na Ubora wa kiwanja pia idadi ya wananchi wanaofatilia soka.... Ndio maana Rais wa TFF alilia baada kusikia Afrika Mashariki imekubaliwa kuwa mwenyeji kwa sababu Tanzania kuna Viwanja bora ukilinganisha na majirani pia watanzania ni watu wanaofatilia mpira
 
Daah!! Afadhali aiseee!!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
NIMESIKITIKA KUSIKIA DODOMA UNAJWNGWA UWANJA WA WATAZAMAJI ELFU 30000 TU.

NIKAJUA ITAKUWA ELFU TISINI
Afcon huwa haileti washabiki wengi, 30k tosha sana. Hata arusha wajenge hivyohivyo tu. Vitasaidia ligi kuu baada ya AFCON
 
NIMESIKITIKA KUSIKIA DODOMA UNAJWNGWA UWANJA WA WATAZAMAJI ELFU 30000 TU.

NIKAJUA ITAKUWA ELFU TISINI
Elfu Tisini siyo mchezo mzee..ni rahisi kutamka lakini utekelezaji siyo rahisi ..

Kwa Ulaya nzima ni viwanja viwili tuu vina uwezo wa kuingiza mashabiki elfu 90 na ni Wembley elfu 90na na Camp nou 99,000
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom