AFCON 2027: Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,129
2,982
Zaweza kuwa ni nchi zitakazofanikisha sana mashindano haya. CAF wasione haya wayalete tu huku kwenye mzuka wa mpira. Ufunguzi iwe Tanzania na ufungaji pia iwe Tanzania.

Dua zenu tafadhari.

=====

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limepitisha ombi la pamoja la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027.

Ni rasmi michuano hiyo itachezwa katika nchi hizo tatu.

Screenshot 2023-09-27 151229.png
 
nawaza tu hiyo Afcon watachezea wapi Tanzania nzima kuna kiwanja kimoja, Kenya, Uganda viwanja hakuna chenye sifa!

Viwanja huwa vinaboreshwa au kujengwa vipya mkuu, maana hii ni 2023 na uwanja unaweza jengwa kwa mwaka hadi miaka 2...

Mfano Tanzania tayari tuna Amani Karume, Benjamin Mkapa na kuna tetesi za kujengwa uwanja mpya Dodoma...

Uwanja kama wa Kirumba unaweza ukawekwa fresh ukachezwa mechi za makundi moja au 2...

Kenya kuna Nyayo na Moi Kasarani...

Uganda wana Mandela, Nakivumbo, Namboole...
 
Mawazo mengine yanafurahisha sana.
Mambo ni 🔥🔥
 
nawaza tu hiyo Afcon watachezea wapi Tanzania nzima kuna kiwanja kimoja, Kenya, Uganda viwanja hakuna chenye sifa!

Mkuu nadhani hujafanya utafiti wa viwanja walivyonavyo Kenya na Uganda...

Juzi juzi tu hapa Kenya ametoka kuhost mashindano ya riadha ya IAAF sababu ana uwanja wa Moi ambao ni multi events...
 
Back
Top Bottom