Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Pole sana aisee... Ulipata tabu sana daah
Haha mimi hii ilinipata nikiwa kidato cha kwanza nilienda kung'oa jino nimechomwa sindano ya ganzi haijakolea hata naona jamaa anachukua machuma, niko mbona bado akasema kwa hiyo unataka tusing'oe? (Dr alikuwa ndugu yangu) akaning'oa hivyohivyo aisee nilipiga makelele hadi wagonjwa wengine walikuja kuangalia kunani huku
 
Story yangu inaanza kama ifuatavyo baada ya kumaliza shughuli zangu za kuuza chipsi usiku napita karbu na nyumba ya jiran namsikia bwana mifugo akimwambia jiran yangu ambae ngombe wake alkuwa kasha dead amzike Mara moja kwani alkuwa ana anthrax basi nikaendelea kupeleleza nkaona alpomzka walipomaliza walivyoondoka nikaenda mfukua skuwa na gloves nikavaa mifuko ya Rambo maana nlsikia akisema ugonjwa ni hatar unaambukzwa na bacteria aina ya bacillus anthrax sjui kama nimepatia spelling au laa ila hayanihusu basi tuendelee na story basi bwana nikamuosha nikamkatakata vipande kesho nikamuuze mishkak vipande vilivyobakia nikampa mshkaj aweke kwenye freezer lake maana anatuchaj per day bwana nikauza wee mara watu wakaanza kuanguka baada ya kula wengne kutapika na kuhara palepale RAIA waliponishtukia wakaanza nikimbiza na mapanga wengine magongo sauti zilisikika zikisema "lazma tukukate vipandevipande" kwa bahat nzur kulikuwa kuna fuso sjui Lori hata skumbuk vzr lilikuwa linaanza kuondoka sjui lilikuwa linaenda WAP bas bwana nikalidandia baada ya masaa mawil mule ndan ya fuso simu yangu inaita mama mwenye nyumba anasema upo WAP mbona kuna polis wanakutafuta hapa nikakata Sm mara tena simu inaitaa kapiga RFK take yule mshkaj anatuifadhia nyama akasema nyama yako ina nn jamaa alikuibia kdogo kaenda itumia gheto sahiv ninavyokwambia tumemuwahisha hospital nikakata Sm .gar likiwa linaenda ktk kukaguakagua mule ndan nikakuta magunia kuyacheck ndani naona bangi pia kulikuwa na madawa mengne syajui kumbe skudandia fuso nilidandia kifo Mara gar likasimama kumbe hlo eneo kulikuwa na police patrol nkasikia shuken wote tukague gari
Kwaiyo stori ilivyo bila shaka wewe ulikufa aisee!
 
Mimi mwezi wa nane tu nilinusurika kifo ..wanavyosema usiendeshe ukiwa umelewa nimeamini.. Bwana hiyo siku nimepiga vodka nusu chupa nikaamua kuchukua baskeli kuanza kuendesha nikaenda mpaka kilimani sasa kuteremka nikawa sipigi break bwana bwana kuna ya mwisho kunakua na kingo na chuma sasa nikazikosa zile chuma maana zingenitoboa utumbo kabisa .. Nikagonga kingo nikatupwa huko.. Bahati nzuri kuna watu niliwapita nikawa nimekaa nawasubiri maana simu imevunjika vipande u can imagine hiyo crush ilikuwaje suruali imetatuka kila mahali tena sehemu tofauti tofauti.. Wale watu wakapiga simu emergency polisi na ambulance wakatinga.. Hospital wakanipiga ct-scan kucheki kuwa uti wa mgongo na brain ipo sawasawa.. Sasa huko hospital nikaishia kutengua mkono maana niliutwist mwenyewe kwa bahati mbaya wakati nimelazwa...
Huwa nawaza Yale machuma yalivyonikosa
....yani kama muvi...
 
daah nakumbuka nilikua darasa la tatu nilikua napenda sana mambo ya ufundi umeme na redio, hasa kuna siku alikuja fundi umeme nyumbani kuna vioande vya wire vikabaki, nilikua na kiredio kidogo cha betri nikajiuliza kwa nini ninunue betri wakati nyaya zipo? basi bwana nikajifanya fundi nikachukua mult plug moja nikaifungua nikaunga nyaya nikaja kuunga na sehemu ya kuweka betri kwenye redio.
Ile kuwasha naona redio kimya sijui niliwaza nini asee nikashika zile nyaya daah nilikula shoti moja ya maana sana hadi leo sielewi nilichomokaje pale!! kuanzia hapo hadi leo sitaki kucheza na umeme tena imezidi sana labda nibadili taa!
..hahahahahahahahaha...
 
Nakumbuka enzi nikiwa darasa la nne nilienda kudumbukia kwenye mapipa ya kutengenezea guru kwa ajili ya piwa au gongo kilicho nikuta cjui hata nimeokolewaje. Nilichokumbuka nilidumbukia dramu kubwa ya molases kesho nkajikuta nipo hospital. daaaaaah utoto ina mambo yake.
Pole sana
 
....yani kama muvi...
Nguo na sehemu...
IMG-20180805-WA0002.jpeg
IMG-20180805-WA0000.jpeg
IMG-20180808-WA0028.jpeg
 
Kuna siku niliumwa tumbo nikiwa alone nikasema leo nakufa nikawa naomba toba kimoyomoyo tena ukifkiria sku hiyo hiyo nilikua na mgonjwa ndugu yang hosp anafanyiwa operation ya tumbo.

Baada ya kumaliza kuomba nikajisemea kimoyo moyo liwalo naliwe nkapanda kitandan baada ya masaa 2 likapoa. Nilishukuru sana
Hata Mimi nimewahi ugua tumbo balaa, siku ambayo sister wa mbali alikuwa hospital anafanyiwa surgery ya tumbo.
 
I want to say something but am holding back. Ni wapi nimesema hawajui kutofautisha kilo na lita? Someone help me...hivi ni kweli hakuna sehemu amnayo wanapima mahindi, maharagwe viazi n.k kwenye lita? Hivi mtu wa kijijini ametoka shambani na njegere zake au huyo muokota kumbikumbi ametoka zake huko kuziokota hiyo kilo ya kupimia akaichukulie wapi? Madam why must we argue over something so insignificant? Hivi hata hapa Dar ukipita barabarani humo watu wanauza njegere mbichi kwenye lita moja au nne au mwenzetu mitaa ya huku uswahilini hujawahi kupita we wapitaga tu masaki?
Achana nae mpuuzi huyo tena narudia mpuuz kbs mbona mpaka leo tunatumia lita kupimia hadi mchele sijui lengo lake nn boyaaa uyooo!!
 
Back
Top Bottom