Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

wengi wenu humu mngekufa kwa kuharisha..

okey mimi wakati niko na miaka mi5 nikiwa na pacha wangu, marehemu kwa sasa, niliwasha kiberiti tukiwa kitandani, moto ukaniunguza nikakitupa godoro likashika moto, nikashuka nikatoka mbio kumwita baba ambaye alikuwa nje, kurudi ndani dadayangu alikuwa ndio anajitahidi kutoka mle ndani, lakini alikuwa amevuta moshi mwingi, baada ya muda alipatwa na ugonjwa flani anakuwa anakakamaa hivi, na baada ya siku tatu alifariki dunia..nikabaki mimi apa...kwa msaada wa bi mkubwa ndio alikuja nihadithia baada ya kuwa na akili timamu..
Duuh pole sana mzee...!
 
Pole sana
 
Pole mkuu

Kiwa na miaka kama mitatu Nliwahi potea baada ya wenzangu kushindwa kuenda sambamba nami nkaachwa nyuma wakatoweka na mitaa siijui... Nkaanza kuwatafuta kumbe naelekea kwingine kabisa nkaja tokea barabara kuu ya lami mbali kabisa hukoo...nkakaa pembeni ya kingo za barabara nalia.. Sentimita chache mbele yangu magari yanapita kwa spidi..
Bahati kuna mkaka alikua anafanya biashara pembeni akanichukua.
Nabembelezwa nyamaza mama anakuja mi nabetua kichwa huku napewa karanga.. Mamangu mwenyeqe hamjui kwenu wapi nanyoosha kidole,miaka hiyo simu anasa.nlikaa kwenye kibanda asubuhi hadi jioni
Sijui ilikuaje ghafla anaambiwa kuna mama anamtafuta mwanae..ndo ikawa pona yangu
Pole lakini hao uliokuwa unatembea nao unafikiri akili zinawatosha?
 
Angesema hivyo sasa..maana mimi namwambia kuwa kijijini ndo tunapima hivyo ananiambia hata kijijini wanajua kutofautisha. Wtf
Pengine hajaa kaa kijijin.... vijijin kuna yale makopo unapimiwa unga.. mchele... maharage yanaitwa litaaa... kawaida hiyo
 
Vijiji vinatumia lita, kijijini kwetu makopo tunayonywea kinibu ya lita 1 ndiyo hayo hupimiwa nafaka na vitu vingine.
Ndivyo nilivyotarajia kueleweshwa, nilielewa tofauti
 
Nilikujibu mwanzo kabisa pale kwamba vijijini tunatumia lita hayo ya kilo hatuyajui umeliona jibu lako?
Kijijini wanajua. Kipimo cha kilo na lita ni vitu viwili tofauti. Wanaweza kuwa wanaita kivingine ila wanayoakili ya kutofautisha maji na unga.
Ndivyo nilivyotarajia kueleweshwa, nilielewa tofauti
 
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.
My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.
Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui). Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.
Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?
Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa..
Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
Nakumbuka enzi nikiwa darasa la nne nilienda kudumbukia kwenye mapipa ya kutengenezea guru kwa ajili ya piwa au gongo kilicho nikuta cjui hata nimeokolewaje. Nilichokumbuka nilidumbukia dramu kubwa ya molases kesho nkajikuta nipo hospital. daaaaaah utoto ina mambo yake.
 
Eeh pole mkuu

Back
Top Bottom