Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 29,020
- 40,837
Shukran mkuu
Pole sana mkuu
Pole sana mkuu
Aisee nimecheka sana maana tukio kama hili lilinitokea nikiwa nakata majani juu ya mti unaoitwa "mhesi" kule Rombo, kumbe nilikuwa nimeshikilia kimti kikavu kikakatika nikashuka kwa kichwa hadi chini phuuh!.
Nilijaribu kuinuka nikae lakini nikashindwa na sauti ya kulia nayo ikawa haitoki. Nikatulia kama dakika moja nguvu zikanijia lakini shingo sidhubutu kuigeuza maana ilikuwa inauma balaa.
Niliposimama nikageuka kumbe pale chini palibakibaki na nywele za kichwani kutokana na kile kishindo nilichoanguka nacho [emoji23][emoji23]
Siku nyingine tena nilitoka shule nikawahi fasta kwenda kupanda juu ya mwembe kujisevia kama ilivyo kawaida yangu, baada ya kula na kushiba hukohuko juu ikawa ni wakati wa kushuka sasa.
Nilikuwa na tabia ya kushuka kwa kutumia matawi ya huo mwembe,, sasa wakati natumia tawi kushuka si likaachia kule juu/likakwanyuka kwa kuzidiwa na uzito! Nilitangulia chini nikiwa nabembea na ule mti hadi chini alafu matawi yake yakanifunika nikalala palepale usingizi mzito hadi usiku wa saa 2 kasoro ndio nilizinduka
USHUHUDA wangu mimi :
Mimi mwaka 1998, nikiwa nasoma primary huko Arusha tulikuwa na tabia ya kutoroka kipindi cha dini siku ya ijumaa na kuondoka na wanafunzi wa kiislam waliokuwa pekee wanaruhusiwa kwenda nje ya campus ya shule kwenda msikitini.
Tulikuwa tunatembea na manati kulenga ndege na kwenda kuogelea mto themi. (Wakati huo ulikuwa na maji mengi sana hata kuuvuka ni tabu)
Siku moja tukaenda kuogelea wanne...mmoja alikuwa mdg zaidi wakati wa kuogelea tukafika mahali penye kina kirefu haswa na kuogelea penyewe hatujui vizuri...nilikunywa maji haswa mpaka tumbo likajaa tukaja nikaja kutapishwa maji na jamaa mmoja alikuwa anakata ndizi shambani.
Wakati nipo nje natetemeka baridi nikakumbuka yule dogo alikuwa kwny maji...akaibuka mara moja na kuniambia kwa sauti
"MUAGE MAMA YANGU" wakati huo mimi nilikuwa na begi lake la sport, viatu na soksi miguuni kwangu.
Rafiki yangu tena alihamia kutoka shule ya msingi huko Moshi na tulikuwa tunakaa siti moja alifia palepale....sintosahau anaitwa ROMAN ARMANDO MLAKI.
Siku ya kumzika tulienda wanafunzi wa karibu darasa zima na yawezekana hata hapa wapo wanaomkumbuka na siku ya kuvunja matanga nikapewa vile viatu vyake, sox na madaftari.
Ilikuwa ni Mazishi ya KWANZA mimi kuhudhuria na nlikuwa kama naota vile.
Watu wakawa wanasema hajafa kachukuliwa na Chunusi...mpk leo sijui chunusi ni nini.
Daah pole sana mkuu
Sasa hukuungua??ahsante mkuu nia yangu ilikuwa ni kuiba sukari guru si ndiyo nikateleza, bwana weee m2 askwambie kwan ilikuwa ni gumzo pale kijijini mpk school.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hatarii sanaa ulizimiaaAisee nimecheka sana maana tukio kama hili lilinitokea nikiwa nakata majani juu ya mti unaoitwa "mhesi" kule Rombo, kumbe nilikuwa nimeshikilia kimti kikavu kikakatika nikashuka kwa kichwa hadi chini phuuh!.
Nilijaribu kuinuka nikae lakini nikashindwa na sauti ya kulia nayo ikawa haitoki. Nikatulia kama dakika moja nguvu zikanijia lakini shingo sidhubutu kuigeuza maana ilikuwa inauma balaa.
Niliposimama nikageuka kumbe pale chini palibakibaki na nywele za kichwani kutokana na kile kishindo nilichoanguka nacho [emoji23][emoji23]
Siku nyingine tena nilitoka shule nikawahi fasta kwenda kupanda juu ya mwembe kujisevia kama ilivyo kawaida yangu, baada ya kula na kushiba hukohuko juu ikawa ni wakati wa kushuka sasa.
Nilikuwa na tabia ya kushuka kwa kutumia matawi ya huo mwembe,, sasa wakati natumia tawi kushuka si likaachia kule juu/likakwanyuka kwa kuzidiwa na uzito! Nilitangulia chini nikiwa nabembea na ule mti hadi chini alafu matawi yake yakanifunika nikalala palepale usingizi mzito hadi usiku wa saa 2 kasoro ndio nilizinduka
Pole sana mkuuBwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?
Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.
Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.
My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.
Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui). Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.
Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?
Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa..
Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
Pole sanaUmenikumbusha nikiwa mtoto bwana nililia kumbikumbi acha zidakwe nikaangiwe Nile, acha nianze kutapika had nikaishiwa nguvu kabisa, tangu siku hyo sipendi kumbi kumbi, kisa kingine nilikuwaga mtundu niliye kubuhu acha nitumbukie kisimani nikiwa mtoto sijui hili wala lile nikaja kuokolewa na wenzangu. Aisee kikubwa mimi nimepitia mengi na kunusurika kifo mara nyingi sana. Namshukuru Mungu dunia hii siji kuondoka had niwe mbibi na mkongojo
Aisee pole sana mkuu, embu tupe na hicho kisa cha simbilisPoleee sana,
Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya
Anyway.. tuyaache hayo
miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
Mimi nilihitaji ufafanuzi nikashushuliwa.Kwa kilo lita sikuelewaa
Nmecheka Mimi jmn[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Poleee sana,
Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya
Anyway.. tuyaache hayo
miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
Hahahahaaaa ikaweje sasaStory yangu inaanza kama ifuatavyo baada ya kumaliza shughuli zangu za kuuza chipsi usiku napita karbu na nyumba ya jiran namsikia bwana mifugo akimwambia jiran yangu ambae ngombe wake alkuwa kasha dead amzike Mara moja kwani alkuwa ana anthrax basi nikaendelea kupeleleza nkaona alpomzka walipomaliza walivyoondoka nikaenda mfukua skuwa na gloves nikavaa mifuko ya Rambo maana nlsikia akisema ugonjwa ni hatar unaambukzwa na bacteria aina ya bacillus anthrax sjui kama nimepatia spelling au laa ila hayanihusu basi tuendelee na story basi bwana nikamuosha nikamkatakata vipande kesho nikamuuze mishkak vipande vilivyobakia nikampa mshkaj aweke kwenye freezer lake maana anatuchaj per day bwana nikauza wee mara watu wakaanza kuanguka baada ya kula wengne kutapika na kuhara palepale RAIA waliponishtukia wakaanza nikimbiza na mapanga wengine magongo sauti zilisikika zikisema "lazma tukukate vipandevipande" kwa bahat nzur kulikuwa kuna fuso sjui Lori hata skumbuk vzr lilikuwa linaanza kuondoka sjui lilikuwa linaenda WAP bas bwana nikalidandia baada ya masaa mawil mule ndan ya fuso simu yangu inaita mama mwenye nyumba anasema upo WAP mbona kuna polis wanakutafuta hapa nikakata Sm mara tena simu inaitaa kapiga RFK take yule mshkaj anatuifadhia nyama akasema nyama yako ina nn jamaa alikuibia kdogo kaenda itumia gheto sahiv ninavyokwambia tumemuwahisha hospital nikakata Sm .gar likiwa linaenda ktk kukaguakagua mule ndan nikakuta magunia kuyacheck ndani naona bangi pia kulikuwa na madawa mengne syajui kumbe skudandia fuso nilidandia kifo Mara gar likasimama kumbe hlo eneo kulikuwa na police patrol nkasikia shuken wote tukague gari
Pole sana mkuu ile homa ilikuwa hatariNakumbuka kupindi hicho niko form 4 aisee nasoma boarding nilishikwa na homa kalii sana ambayo Kimsingi ilikuwa ni Dengu maana dengu kipind hicho ilikuwa Imeua sana watu na dalili zangu zilikuwa sawa... Yani nimefika hosp manesi wananiwekea Drip za maji tu me homa inazidi kupandaa mara wakataka kuanza kunichoma sindano za UTI akati hata hawajajua Naumwa nini... Dadaa angu akawa mkali sana ikabdi aende kuomba kibali shule nichukuliwe maana hali ni mbayaa..wakawa wanazingua sister akaja hosp me homa ipo juu Kichwa kinawakaa motoo naona nakufa najionaa wee Dada alipokuja nkamshika mkono nkamwambia cster ukiniacha hapa NAKUFA...sister ikabdi akomae manesi wakamind sana wakampa form zakujaza kwamba akinichukua nikifa njiani wenyewe hawausiki aisee akanichukua kwenye Gari nasweat hatarii... Kufika hosp binafsi wakanipiga Panadol za ujerumani na drip za kutoshaa hapo ndo nkaona nafuu.. Aisee acha tu kifo kipo