Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa..

Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
41,020
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
41,020 2,000
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.

My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.

Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui).

Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.

Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?

Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa.

Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
 
cariha

cariha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Messages
7,691
Points
2,000
cariha

cariha

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2015
7,691 2,000
Umenikumbusha nikiwa mtoto bwana nililia kumbikumbi acha zidakwe nikaangiwe Nile, acha nianze kutapika had nikaishiwa nguvu kabisa, tangu siku hyo sipendi kumbi kumbi, kisa kingine nilikuwaga mtundu niliye kubuhu acha nitumbukie kisimani nikiwa mtoto sijui hili wala lile nikaja kuokolewa na wenzangu. Aisee kikubwa mimi nimepitia mengi na kunusurika kifo mara nyingi sana. Namshukuru Mungu dunia hii siji kuondoka had niwe mbibi na mkongojo
 
Danpol

Danpol

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Messages
2,894
Points
2,000
Danpol

Danpol

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2013
2,894 2,000
Poleee sana,

Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya

Anyway.. tuyaache hayo

miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
 
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
41,020
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
41,020 2,000
Umenikumbusha nikiwa mtoto bwana nililia kumbikumbi acha zidakwe nikaangiwe Nile, acha nianze kutapika had nikaishiwa nguvu kabisa, tangu siku hyo sipendi kumbi kumbi, kisa kingine nilikuwaga mtundu niliye kubuhu acha nitumbukie kisimani nikiwa mtoto sijui hili wala lile nikaja kuokolewa na wenzangu. Aisee kikubwa mimi nimepitia mengi na kunusurika kifo mara nyingi sana. Namshukuru Mungu dunia hii siji kuondoka had niwe mbibi na mkongojo
Daah pole best kutumbukia kisimani utakuwa ulikuwa mtundu sana
 
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Messages
6,467
Points
2,000
Desire Dizaya

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2015
6,467 2,000
eti upaki vitu vyako uondoke duniani
Poleee sana,

Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya

Anyway.. tuyaache hayo

miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
 
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
1,621
Points
2,000
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
1,621 2,000
Daaah pole san.

Kumbikumbi nimewala san, nadhan usichokijua ww ni kwamba kumbikumbi hawaliwi hivihivi na ukiwala ivoivo bila chchte basi ule kdg san, ukizidisha kitakupata ulichokipata siku hiyo.

Mm binafsi kuna siku nikiwa mdg nlikuwa naumwa malaria. Bahat mbaya sikupelekwa hospitali kwa sabab ziko mbali na tulipokuw tunaishi ni kijijini san.

Asbh km kawaida wazee waliondoka kwenda shamba, mm huku nyuma nikazidiwa, nilianza kuharisha san na kutapika. Baada ya muda niliishiwa nguvu, nikaendelea kufanya vyote palepale. Mama aliporud saa sita kupika alinikuta niko hoi san, ndipo ikawa hamna namna zaid ya kupelekwa hospitali.
 
Mwamba028

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Messages
3,996
Points
2,000
Mwamba028

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2013
3,996 2,000
Poleee sana,

Kwa upande wangu, kuna simbilis moja almanusra inifanye nipak vitu vyangu niondoke duniani, shenzi sana, mapenzi haya

Anyway.. tuyaache hayo

miaka ya Nyuma kidogo hapo, nikiwa kama standard three hv au two, nikiwa kwa babu mzaa mama moshi vijijin huko, siku moja nimepanda juu ya mti wa mmerez, (kwa wanao ifahamu hii miti ukiwa umekomaa n mrefu sana) nilikua naupunyua matawi, bwana wee huku na huko nimekata tawi lina kama V hv, hiyo V si ikaja ikanivaa shingon kama tai hv... nilijaribu kulivua weee lakn wapi, huku na huko wapi (nilikua bado mdogo, chini ya miaka 10) so uamuz wa haraka ukanijia nijiachie tu nidondoke nalo, nikaachia panga likatangulia kwanza... Yaan ilitokea kama miujiza vile, ile nataka kujiachia tu likanivuka lenyewe, niko hoi bin taaban hapo, nguvu zenyewe zalisha anza kuisha, nikashuka nikaenda kulala
ha ha ha utundu ungekuua mwana,,
 
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
41,020
Points
2,000
Khantwe

Khantwe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
41,020 2,000
Si unajua uroho boss haha
Daaah pole san.

Kumbikumbi nimewala san, nadhan usichokijua ww ni kwamba kumbikumbi hawaliwi hivihivi na ukiwala ivoivo bila chchte basi ule kdg san, ukizidisha kitakupata ulichokipata siku hiyo.

Mm binafsi kuna siku nikiwa mdg nlikuwa naumwa malaria. Bahat mbaya sikupelekwa hospitali kwa sabab ziko mbali na tulipokuw tunaishi ni kijijini san.

Asbh km kawaida wazee waliondoka kwenda shamba, mm huku nyuma nikazidiwa, nilianza kuharisha san na kutapika. Baada ya muda niliishiwa nguvu, nikaendelea kufanya vyote palepale. Mama aliporud saa sita kupika alinikuta niko hoi san, ndipo ikawa hamna namna zaid ya kupelekwa hospitali.
 
Forum statistics

Threads 1,336,292
Members 512,585
Posts 32,533,664
Top