Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Baada ya kusoma hii thread nimegundua watu waliokulia vijijini walikuwa hatarini sana....
Nakubaliana na hili. Mjini watoto wanachungwa sana na kulelewa kwenye geti kali. Shule wanapelekwa na basi la shule. Maji yapo bombani hawaendi kuchota kisimani. Mjini matunda yananunuliwa sokoni na juisi wanakamuliwa kabisa hakuna haja ya kukwea miti kuchuma matunda. Besides, miti yenyewe ya kukwea mjini ipo wapi!!!! Mjini hakuna kuchunga ng'ombe maporini maziwa yaneletwa kwa bili ya mwez au wanakunywa ya unga. Mjini hakuna kuogelea mtoni wanaenda swimming pool 😁😁. Mjini kucheza ni weekend tu tena wanapelekwa kwa gari kucheza na watoto wa mama mdogo 😎. Mjini bhana............
 
Ilikuwa kwenye bembea kijijini, tulitumia kamba za katani na kitako ilikuwa pande la tawi la mti!
Nilikuwa najipaisha sana kwenye ile bembea (yaani ile sky was a limit), one fuckking day kamba ilikatika, aisee, nilienda kutua chini nikiwa juu ya lile tawi! Nilitoa mlio wa ajabu na ushuzi mreeefu, it was a hell moment! Sikutembea siku kadhaa (sikumbuki ngapi).

Baada ya hapo sikuwahi kusogelea bembea, hadi leo!
 
Kuna pimbi moja ilikuwaga na papuchi tamu sana kidogo inipeleke akhera aisee.
Wayback miaka kadhaa nyuma kuna dem mmoja wa kizaramo alitugonganisha geto na msela alikuwa anasoma TEKU. Ilikuwa Mbeya maeneo ya Block T kilichotokea kutokana na ugomvi nilichomwa kisu mara mbili shingoni.

Ilikuwa ni balaa ndani ya sekunde chache nilianza kuona giza giza huku macho yakipoteza uwezo wa kuona, yaani kitu kama usingizi mzito na kupumua kwa kutumia nguvu kubwa.Mwili wote ulilegea ukiwa hauna nguvu kabisa.

Nilichokigundua ukielekea kufa huwa hakuna maumivu kabisa Ila huwa ni majuto ,hofu ya kufa na kutokuamini kama maisha ndio yanafikia mwisho. Ndani ya mda huo nilitamani ningerudisha mda nyuma hata kwa Siku kadhaa chache.

Anyway thanks God I'm still alive,baada ya kupoteza fahamu nilijikuta hospitali ya rufaa.
Kesi ilifika mahakamani??
 
Daah inanikumbusha miaka 1996 nikiwa Mpanda, kipindi hicho nikiwa Secondary ili kila inapofika ijumaa nilikua natoroka kwenda machimboni kwakua kipindi hicho hela ilikua inapatikana kirahisi sana.

Nilikua nikifika huko naingia kwenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita ishirini, chini kabisa nilikua naingia ndani ya "fonka " liliokaa mfano wa chumba ambalo ndio nakwenda kuchimba katika mkondo wenye Dhahabu nyingi.

Kwakua nilihitaji pesa nilizoea kufanya shughuli hiyo kwa siri na sikutaka mtu yeyote shuleni na nyumbani ajue kama naendaga machimboni kwasababu nilikua bado mwanafunzi.

Siku moja tulipata jiwe kubwa la dhahabu na baada ya mgao nilipewa milioni 12 malipo ya mwanzo ila kutokana na umri wangu ilikua ni nyingi sana na siku hiyo niliamua kwenda kumpa dada angu aniwekee kisha nikarudi kwa kusubiria hela nyingine.

Tukiwa ndani walikuja jamaa wakiwa na silaha wakitaka wapewe pesa zote, watu walikula bakora siku hiyo ni balaa. Kuna brother mmoja nakumbuka alijisaidia pale pale. Mimi nilitumbukizwa kweny pipa la maji ikawa kila napotoa kichwa nje nakutana na kibao cha kichwani narudi kwenye maji,ilifikia muda nikapoteza fahamu nimekuja kupata fahamu jamaa wamechukua kila kitu lakini bahati yangu ni kwamba hela nilikua nishazipeleka kwa dada angu.

Pamoja na hayo sikuacha kwenda katika uchimbaji na kipindi hicho nikanunua kipimo cha zahabu ambazo zinapatikana juu juu ya kwenye ardhi nikawa naingiza pesa kwenye mashine na kwenye mashimo marefu niliendelea ku- hustle kama kawaida.

Siku moja nikiwa ndani ya shimo chini kabisa udongo ulikua ukiporomoka na maji yalikua yameanza kujaa hivyo nikawa nachota maji naweka kwenye ndoo kisha inavutwa maji yanamwagwa nje ya shimo lakini wakati shughuli inaendelea ulibomoka ukuta na kurudisha ndoo chini,mimi niliona giza ghafla hivyo nikakimbilia kwenye chumba cha shimo ambako nako hakuna njia ya kutokea. Hewa ilikua inapita lakini maji yalikua yakizidi kuongezeka hivyo nikajua lazima nife.

Kwamba mbaaali sana nilikua nasikia sauti za watu wakigombana kwamba waite polisi ndipo waje waanze kutoa udongo Lakin kuna jamaa yangu mmoja siji kumsahau, yeye alikataa akawaambia wachimbe kwanza wautoe mwili ndipo waite polisi kwasababu wakiacha muda mrefu bila kuwahi kuutoa mwili maji yanaweza kuwa mengi alafu ikawa shida ndipo kazi ikaanza.

Nashukuru Mungu kuna mmoja wao aliona mwanga wa tochi yangu kupitia kitundu kidogo sana,akawaeleza wenzake kwamba nitakua mzima kwasababu kama ningekua nimepoteza uhai tochi ingezama kwenye maji na isingetoa mwanga hivyo wakapiga kazi kwa kufuata mwanga mdogo wa tochi.

Kuna muda nikawa naita ila kwasababu ya kishindo cha sululu ya kuchimbia wakawa hawasikii baada ya muda walitoboa tundu angalau hewa ikaongezeka na tukawasiliana vizuri hadi nilipo okolewa kutoka kwenye fonka hiyo.

Tangu siku hiyo sikutaka kusikia tena habari za machimbo. Huko roho mkononi maana kazi ngumu, hatari ni nyingi na bado ukipata vihela kidogo majambazi wanakuvizia.
Vipi ulitoboa lakini???
 
wengi wenu humu mngekufa kwa kuharisha..

okey mimi wakati niko na miaka mi5 nikiwa na pacha wangu, marehemu kwa sasa, niliwasha kiberiti tukiwa kitandani, moto ukaniunguza nikakitupa godoro likashika moto, nikashuka nikatoka mbio kumwita baba ambaye alikuwa nje, kurudi ndani dadayangu alikuwa ndio anajitahidi kutoka mle ndani, lakini alikuwa amevuta moshi mwingi, baada ya muda alipatwa na ugonjwa flani anakuwa anakakamaa hivi, na baada ya siku tatu alifariki dunia..nikabaki mimi apa...kwa msaada wa bi mkubwa ndio alikuja nihadithia baada ya kuwa na akili timamu..
Hinasikitisha sana...
 
Ilikuwa kwenye bembea kijijini, tulitumia kamba za katani na kitako ilikuwa pande la tawi la mti!
Nilikuwa najipaisha sana kwenye ile bembea (yaani ile sky was a limit), one fuckking day kamba ilikatika, aisee, nilienda kutua chini nikiwa juu ya lile tawi! Nilitoa mlio wa ajabu na ushuzi mreeefu, it was a hell moment! Sikutembea siku kadhaa (sikumbuki ngapi).

Baada ya hapo sikuwahi kusogelea bembea, hadi leo!
aisee bembea ilikuwa tamu ile, mtu wa kukusukuma awe na mijisifa sasa...hakuna rangi utaacha kuona
 
Zamani nikiwa kijana mdogo mkoani tabora tulikua tunatoroka shule na kwenda stesheni kudandia treni, tulienjoy tu vile tunadandia treni inaenda inarudi, sasa siku moja tuko kundi kila mmoja anang'ang'ania apande na huku treni inatembea basi ile kuvutana tukaanguka mwenzetu mmoja akaingia chini kabisa akasagwa na treni wengine kukatika miguu, mimi sikuumia ila kaptula ya shule ilichanika kuanzia mbele hadi nyuma ikawa kama sketi, shati lote lililoa damu za wale majeruhi, habari ikasambaa mji mzima watu wakaenda kitete hospital kuona kama watoto wao nao wamo, mama yangu alichanganyikiwa sana sasa kurudi mtaani kila mtu anajua stori aisee siku ile mimi na wenzangu tulikula kichapo cha mtaa kila mtu alijifanya anauchungu sitaisahau ile siku, r.i.p pendo hadi leo naikumbuka sura na viatu vyake.
Uliposema RIP Pendo moyo wangu umehuzunika sana :(:(
 
Daah inanikumbusha miaka 1996 nikiwa Mpanda, kipindi hicho nikiwa Secondary ili kila inapofika ijumaa nilikua natoroka kwenda machimboni kwakua kipindi hicho hela ilikua inapatikana kirahisi sana.

Nilikua nikifika huko naingia kwenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita ishirini, chini kabisa nilikua naingia ndani ya "fonka " liliokaa mfano wa chumba ambalo ndio nakwenda kuchimba katika mkondo wenye Dhahabu nyingi.

Kwakua nilihitaji pesa nilizoea kufanya shughuli hiyo kwa siri na sikutaka mtu yeyote shuleni na nyumbani ajue kama naendaga machimboni kwasababu nilikua bado mwanafunzi.

Siku moja tulipata jiwe kubwa la dhahabu na baada ya mgao nilipewa milioni 12 malipo ya mwanzo ila kutokana na umri wangu ilikua ni nyingi sana na siku hiyo niliamua kwenda kumpa dada angu aniwekee kisha nikarudi kwa kusubiria hela nyingine.

Tukiwa ndani walikuja jamaa wakiwa na silaha wakitaka wapewe pesa zote, watu walikula bakora siku hiyo ni balaa. Kuna brother mmoja nakumbuka alijisaidia pale pale. Mimi nilitumbukizwa kweny pipa la maji ikawa kila napotoa kichwa nje nakutana na kibao cha kichwani narudi kwenye maji,ilifikia muda nikapoteza fahamu nimekuja kupata fahamu jamaa wamechukua kila kitu lakini bahati yangu ni kwamba hela nilikua nishazipeleka kwa dada angu.

Pamoja na hayo sikuacha kwenda katika uchimbaji na kipindi hicho nikanunua kipimo cha zahabu ambazo zinapatikana juu juu ya kwenye ardhi nikawa naingiza pesa kwenye mashine na kwenye mashimo marefu niliendelea ku- hustle kama kawaida.

Siku moja nikiwa ndani ya shimo chini kabisa udongo ulikua ukiporomoka na maji yalikua yameanza kujaa hivyo nikawa nachota maji naweka kwenye ndoo kisha inavutwa maji yanamwagwa nje ya shimo lakini wakati shughuli inaendelea ulibomoka ukuta na kurudisha ndoo chini,mimi niliona giza ghafla hivyo nikakimbilia kwenye chumba cha shimo ambako nako hakuna njia ya kutokea. Hewa ilikua inapita lakini maji yalikua yakizidi kuongezeka hivyo nikajua lazima nife.

Kwamba mbaaali sana nilikua nasikia sauti za watu wakigombana kwamba waite polisi ndipo waje waanze kutoa udongo Lakin kuna jamaa yangu mmoja siji kumsahau, yeye alikataa akawaambia wachimbe kwanza wautoe mwili ndipo waite polisi kwasababu wakiacha muda mrefu bila kuwahi kuutoa mwili maji yanaweza kuwa mengi alafu ikawa shida ndipo kazi ikaanza.

Nashukuru Mungu kuna mmoja wao aliona mwanga wa tochi yangu kupitia kitundu kidogo sana,akawaeleza wenzake kwamba nitakua mzima kwasababu kama ningekua nimepoteza uhai tochi ingezama kwenye maji na isingetoa mwanga hivyo wakapiga kazi kwa kufuata mwanga mdogo wa tochi.

Kuna muda nikawa naita ila kwasababu ya kishindo cha sululu ya kuchimbia wakawa hawasikii baada ya muda walitoboa tundu angalau hewa ikaongezeka na tukawasiliana vizuri hadi nilipo okolewa kutoka kwenye fonka hiyo.

Tangu siku hiyo sikutaka kusikia tena habari za machimbo. Huko roho mkononi maana kazi ngumu, hatari ni nyingi na bado ukipata vihela kidogo majambazi wanakuvizia.
Hakika Mungu yupo
 
Duuh
nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma nilikua napenda Sana kuogelea asa mshua mkali sana hataki tutoke njee asa kunasiku nikapata time ijumaa
Nikapitia kwenye bwawa pekeangu bhasi nikaona hapa hakuna wakunisemelea duuuuh!!!!!!!!!!!?????
Nikaona sio kesi nikajirusha kwenye maji mzeee
Mungu alikua Na Mimi maana sikua Na MTU wala mwenzangu ila kumbe Kwa mbali alikuepo baba mmoja akiwa analima asa kumbe alipoona nimerukia kama mbuzi akajua tu huyu mtoto hajui ndo kuwahi
Kati huo nimejititia kitambo sana nimekunywa vikombe vya maji kama vyote sikujua hata nyumbani nimefika vipi ila ninachokumbuka
MPAKA LEO SITAKI KUJUA KUOGELEA KWA JINSI YOYOTE HATA KUOGA MVIVU
 
Sitasahau mara ya kwanza nimetoroka nyumbani kwenda disco na marafiki sasa saa ya kurudi tukapata lifti ya mshikaji kumbe alikua tungi hatari tunatoka bills kwenye corner ya salender nachokumbuka kuna dada alisema naona tunaitafuta morogoro kwa ile speed aliyokua anaendesha kilichofata hapo nilikua nje ya gari ukiniuliza mpk leo nilitokaje au kwakupitia wapi siwezi kukwambia ila waliobaki kwenye gari walipasuka vibaya ingawa hakujuwa na kifo nikajisemea kama nilitoka humu salama na hivi nilitoroka home sitarudia kutoroka tena
 
Duuh
nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma nilikua napenda Sana kuogelea asa mshua mkali sana hataki tutoke njee asa kunasiku nikapata time ijumaa
Nikapitia kwenye bwawa pekeangu bhasi nikaona hapa hakuna wakunisemelea duuuuh!!!!!!!!!!!?????
Nikaona sio kesi nikajirusha kwenye maji mzeee
Mungu alikua Na Mimi maana sikua Na MTU wala mwenzangu ila kumbe Kwa mbali alikuepo baba mmoja akiwa analima asa kumbe alipoona nimerukia kama mbuzi akajua tu huyu mtoto hajui ndo kuwahi
Kati huo nimejititia kitambo sana nimekunywa vikombe vya maji kama vyote sikujua hata nyumbani nimefika vipi ila ninachokumbuka
MPAKA LEO SITAKI KUJUA KUOGELEA KWA JINSI YOYOTE HATA KUOGA MVIVU

umenifurahisha saaana kama nakuona vile ulivyokua mwoga,pole
 
Kuna pimbi moja ilikuwaga na papuchi tamu sana kidogo inipeleke akhera aisee.
Wayback miaka kadhaa nyuma kuna dem mmoja wa kizaramo alitugonganisha geto na msela alikuwa anasoma TEKU. Ilikuwa Mbeya maeneo ya Block T kilichotokea kutokana na ugomvi nilichomwa kisu mara mbili shingoni.

Ilikuwa ni balaa ndani ya sekunde chache nilianza kuona giza giza huku macho yakipoteza uwezo wa kuona, yaani kitu kama usingizi mzito na kupumua kwa kutumia nguvu kubwa.Mwili wote ulilegea ukiwa hauna nguvu kabisa.

Nilichokigundua ukielekea kufa huwa hakuna maumivu kabisa Ila huwa ni majuto ,hofu ya kufa na kutokuamini kama maisha ndio yanafikia mwisho. Ndani ya mda huo nilitamani ningerudisha mda nyuma hata kwa Siku kadhaa chache.

Anyway thanks God I'm still alive,baada ya kupoteza fahamu nilijikuta hospitali ya rufaa.

Dah pole sana
 
Mwezi wa 2 mwaka huu home tulikula chakula chenye sumu(inasemekana ilikua samaki) asubuhi tumeamka ilkua siku ya j2, mke kaamka katoka nje baada dk 10 hv karudi mbio akasema watoto(wapo mapacha) pamoja na mdada wa kazi wanaharisha sana, wakati wanajiandaa kwenda hospitali mara kaja mlinzi aliekuja kumpokea mwenzake anadai mwenzie yupo hoi kaharisha usiku kucha hata kuinuka hawezi (alikua anakula home jioni) wakapigia ndugu zake wakaja na gari ya kampuni wakampeleka hospitali,
Nikapakia mke, dada na watoto nkawapeleka pale kwa hospital kwa mama ngoma, nkarudi home maana alibaki mtoto mdogo,

Baada ya kurudi na mimi nkanza trip mdogo ndogo hadi ikafika namwaga maji tu lkn najiskia poa wala siumwi popote kufika saa 6 nkaona hii hali sio ntaishiwa nguvu maana kila dk toi, nkaanza safari kwenda hospital nkaanza kuhisi nguvu zinaisha, sikuchukua gari nkaenda kupanda daladala niende hospital niliyoizoea ipo kkoo, nimetokea sinza mapambano kufika kwa remi hali ikawa mbaya sana, nkawa nachungulia vibao pembezoni nikionna cha hospital nishuke (sikutaka kwenda Palestina) kufika karibu na kijiweni nkaona kibao nkamwambia konda akanishusha, kufika hospital drip 3 za fastaa huku vipimo vinaendelea, hali ilizidi kua mbaya nilijiskia kufakufa nikawa napiga ule ukuta wa wodini makofi tu mara nkazima mazima kuja kushtuka saa 2 usiku niko vizuri kiasi...
Nashkuru Mungu hakuna aliedhurika zaidi....

Poleni sana
 
Nakumbuka henzi za utoto nilikua mtundu balaa,kuna siku tulienda porin kusanya kuni tumefika mm nikawambia wenzangu kuni zilizodondoka chini sishiki nataka zilizopo juu ya miti tu(matawi yaliokauka)

Baada ya kupanda miti kadhaa nikakutana na miti miwili mirefu balaa imeachana kama mita2 iv alafu yote juu ina matawi makavu ila yapo mbali,sikujali hlo mm nikapanda mti wa kwanza nikakata yale matawi...sasa ili nikate ya mti wa pili lazima nishuke nikaanze upya kupanada..

Kucheki chini ni mbali mpaka nishuke nikapande tena sio leo,si nikaona bora nijirushe kama nyani nirukie kwenye mti wa pili..nikaweka panga vizuri na nikatarget tawi la kudaka upande wa pili..si nikajirusha nikashindwa kulifikia lile tawi..kilichofuata nikuporomoka kwenda chini huku nikijibamiza kwenye matawi ya chini..

Nilivyotua nilikaa pale chini kama dakk1 siwezi kujigusa wala kutoa sauti alafu wenzangu wapo machakani hawajui kinachoendelea..baada ya mda sauti ikarudi nikapiga bonge la yowe wenzangu wakaja..
Kuja kuninyanyua mguu umetenguka ilibidi nibebwe mpaka nyumban nimefika nikapokelewa na kichapo ndio uduma zingine zikaendelea.

Dah wewe unahatari sana
 
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.

My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.

Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui).

Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.

Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?

Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa.

Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
Pole Sana
 
Duuh
nakumbuka miaka kadhaa huko nyuma nilikua napenda Sana kuogelea asa mshua mkali sana hataki tutoke njee asa kunasiku nikapata time ijumaa
Nikapitia kwenye bwawa pekeangu bhasi nikaona hapa hakuna wakunisemelea duuuuh!!!!!!!!!!!?????
Nikaona sio kesi nikajirusha kwenye maji mzeee
Mungu alikua Na Mimi maana sikua Na MTU wala mwenzangu ila kumbe Kwa mbali alikuepo baba mmoja akiwa analima asa kumbe alipoona nimerukia kama mbuzi akajua tu huyu mtoto hajui ndo kuwahi
Kati huo nimejititia kitambo sana nimekunywa vikombe vya maji kama vyote sikujua hata nyumbani nimefika vipi ila ninachokumbuka
MPAKA LEO SITAKI KUJUA KUOGELEA KWA JINSI YOYOTE HATA KUOGA MVIVU
nimecheka hapo kwenye kuoga
 
Back
Top Bottom