Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Itakuwa muanzisha uzi ni mtu wa iringa...nilienda kutembea huko mwaka huu nikashangaa kichombo/kipimio kikiitwa Lita, wanakitumia kupima vitu vya uzito kama njegere, maharagwe...ukitumia akili ya shule unaweza usielewe maana mambo ya lita ni kwenye vi/kimiminiko tu
Hata wa nanjilinji tunaita ivo
 
Umenikumbusha kukwea miti lol, yaani nilikuwa napenda kukwea miti mimi jamani!!!!
Hahahahahaha utundu mwingine huu sijui inakuaje ....home kulikua na mdure ambao ulijengwa kwa miti sasa ulibomoka na kubakia miti ikiwa na misumari yake .....ilikua tabia yangu kupanda kwenye ile miti siku hiyo nguo ikanasa kwenye misumari nikawa naning'inia huko juu mpaka walipokuja watu kunishusha......utoto raha jamani mpaka Leo nakaribia kuitwa mama nimepitia vingi doh
 
Sijui kwenu, ila kwetu tunasema ni "kopo" au "debe" na sio lita. Actually huwa watu wanadhani kopo moja ni sawa na kilo moja kwa vitu vingi, which is wrong.

Kuhusu bei, tunaandikiwa kopo ni shs. 200 na sio lita, huwezi kusema lita ya mahindi..

Sorry, labda nyie mna terminologies tofauti.
Sisi tunaita "lita ya mahindi"[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Khantwe, ulikula kumbikumbi "lita moja", how? Kuna lita moja ya kumbikumbi?..[emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi kikombe cha lita moja kinapima hata mchanga!!! Yan kinaitwa lita.haswa wa bara. Kwa wenzetu wa pwani sijui. Yan lita ya maji ..lita ya mchanga...lita ya senene..lita ya mahindi...irrespective..!!!!!
 
Sisi kikombe cha lita moja kinapima hata mchanga!!! Yan kinaitwa lita.haswa wa bara. Kwa wenzetu wa pwani sijui. Yan lita ya maji ..lita ya mchanga...lita ya senene..lita ya mahindi...irrespective..!!!!!
Lita ya mahindi..teh teh, sawa mkuu. Basi mleta mada yupo sahihi kwa mrengo wenu...
 
NImenusurika mara kibao sana hata nashindwa nisimulie lipi
kama vipi wasiliana na Mungu akusimulie kisa kikubwa zaidi
I can Say Thanks God Am Alive
 
Yaani mimi hata sijuagi nitahadithia nini utotoni mwangu. Sinaga Janga wala Taharuki yoyote!
 
Ulikuwa bado kidogo tu u balance nature maana ulikuwa una distrub equal system
 
Nakumbuka enzi nikiwa darasa la nne nilienda kudumbukia kwenye mapipa ya kutengenezea guru kwa ajili ya piwa au gongo kilicho nikuta cjui hata nimeokolewaje. Nilichokumbuka nilidumbukia dramu kubwa ya molases kesho nkajikuta nipo hospital. daaaaaah utoto ina mambo yake.
Hii itakua moshi tu hii...
 
Mie bhana nakumbuka ilikuwa 2003 nipo Darasa la Tano Kunduchi Dar.

Kisa kenyewe ilikuwa ni ugomvi baina yangu mm na mwanafunzi mwenzangu wa darasa la saba.

Sijui ni utoto au nini tukapanga tupigane baada ya muda wa masomo kuisha. Mie nilikuwa na kundi kubwa la wapambe asikwambie mtu ukiwa na wapambe unajiamini balaaa.

Mwenzangu yupo peke ake baada ya muda wa masomo kuisha tukaruhusiwa, Wana wakanipanga twende zetu na yule mpinzani wangu akatafutwa tukatokomea porini uko.

Nikavua Begi wapambe wakanishikia jamaa akasogea ngumi zikaanza Daah mie nina bonge la nyomi la wapambe Piga huyo!! Mng'oe Meno huyo!!

Bichwa likavimba Mbwembwe nyingi ,Basi mara Ngumi Mara Teke, Kwepa Tena Kwepa Nikampatia Moja Saafi ya Mdomo Akachanika Kidogo Damu Ikaanza Kutoka.

Daah kumbe ndo nimemjeruhi simba, Nilikula mbata za kutosha hadi nikaona kizunguzungu nikazirai.

Wana wote wakakimbia nililala pale sijitambui kwa nusu saa. Bahati kuna mzee alikuwa anapita akaniona nimelala uso umevimba Shati limechanika Daah

Ndo akanibeba kunipeleka shule uku sijitambui kuwaelezea walimu nikamwagiwa maji sijui ndo kunipeleka hospital Wakaitwa wazazi.

Daah Kesi ilikuwa kubwa mno, Wazazi wote wakaitwa.Nashukuru Mungu yaliisha ila nimekoma Kupewa Sifa za Kijinga Inaponza Watu.
Haya ya shule nimepigana sana tu!
Siku hiyo nkaingia kwenye 18 za jamaa mmoja alkua anaonekana mzembemzembe hivi afu mpolee darasani, wee nilichezea makonde ya haja, ngumi kama jiwe mpaka pambano linaisha nilimpiga ngumi 2 tu,

Nyingine tukamchangia jamaa tupo wawili yeye peke yake, tukiwa tunataka kumzidi akamng'ata mwenzanzangu, wakati mabishano yakiendelea mimi nikawa nimeinama nafunga kamba za kiatu nilipigwa teke la uso likaniinua hadi juu network ikakakata nkajazindukia mtoni baada ya kumwagiwa mimaji...
 
Mwezi wa 2 mwaka huu home tulikula chakula chenye sumu(inasemekana ilikua samaki) asubuhi tumeamka ilkua siku ya j2, mke kaamka katoka nje baada dk 10 hv karudi mbio akasema watoto(wapo mapacha) pamoja na mdada wa kazi wanaharisha sana, wakati wanajiandaa kwenda hospitali mara kaja mlinzi aliekuja kumpokea mwenzake anadai mwenzie yupo hoi kaharisha usiku kucha hata kuinuka hawezi (alikua anakula home jioni) wakapigia ndugu zake wakaja na gari ya kampuni wakampeleka hospitali,
Nikapakia mke, dada na watoto nkawapeleka pale kwa hospital kwa mama ngoma, nkarudi home maana alibaki mtoto mdogo,

Baada ya kurudi na mimi nkanza trip mdogo ndogo hadi ikafika namwaga maji tu lkn najiskia poa wala siumwi popote kufika saa 6 nkaona hii hali sio ntaishiwa nguvu maana kila dk toi, nkaanza safari kwenda hospital nkaanza kuhisi nguvu zinaisha, sikuchukua gari nkaenda kupanda daladala niende hospital niliyoizoea ipo kkoo, nimetokea sinza mapambano kufika kwa remi hali ikawa mbaya sana, nkawa nachungulia vibao pembezoni nikionna cha hospital nishuke (sikutaka kwenda Palestina) kufika karibu na kijiweni nkaona kibao nkamwambia konda akanishusha, kufika hospital drip 3 za fastaa huku vipimo vinaendelea, hali ilizidi kua mbaya nilijiskia kufakufa nikawa napiga ule ukuta wa wodini makofi tu mara nkazima mazima kuja kushtuka saa 2 usiku niko vizuri kiasi...
Nashkuru Mungu hakuna aliedhurika zaidi....
 
Kuna siku niliumwa tumbo nikiwa alone nikasema leo nakufa nikawa naomba toba kimoyomoyo tena ukifkiria sku hiyo hiyo nilikua na mgonjwa ndugu yang hosp anafanyiwa operation ya tumbo.

Baada ya kumaliza kuomba nikajisemea kimoyo moyo liwalo naliwe nkapanda kitandan baada ya masaa 2 likapoa. Nilishukuru sana
Khaaa
 
Haya ya shule nimepigana sana tu!
Siku hiyo nkaingia kwenye 18 za jamaa mmoja alkua anaonekana mzembemzembe hivi afu mpolee darasani, wee nilichezea makonde ya haja, ngumi kama jiwe mpaka pambano linaisha nilimpiga ngumi 2 tu,

Nyingine tukamchangia jamaa tupo wawili yeye peke yake, tukiwa tunataka kumzidi akamng'ata mwenzanzangu, wakati mabishano yakiendelea mimi nikawa nimeinama nafunga kamba za kiatu nilipigwa teke la uso likaniinua hadi juu network ikakakata nkajazindukia mtoni baada ya kumwagiwa mimaji...
Hahaha we utakuwa ulikuwa na kimwili kidogodogo huwa mnakuwa wakorofi halafu nguvu hamna
 
Back
Top Bottom