Tuliowahi 'kuchungulia kaburi' tukutane hapa

Mwaka 2008 nikiwa Standard 7, Tulienda kufanya mitihani ya Jumamosi shule ya msingi KALOBE Mbeya Mjini

Hapo tulikutana shule zaidi ya 10 kufanya paper moja la kujipima na tulifanya hivyo kila jumamosi lakini kwa kubadili badili shule ya kufanyia kwa malipo ya shilingi 300.

Sasa baada ya Kufanya paper zetu, huwa tulikuwa tunacheza mpira na michezo mingine tukisubiri TOKEO.

Mimi na majamaa mengine kutoka Mixture ya shule mbalimbali tukawa tunacheza TOBO DUNDA Halafu ukipigwa TOBO inatakiwa ukimbie ukamshike Demu mmoja alikuwa anaitwa Grace ILI Uepukane na Kipigo kitakatifu kutoka kwa MASELA.Kwahiyo tuliita TOBO DUNDA, SHIKA GRACE

TUMEcheza tumecheza, Wahuni wakanipiga TOBO, Dah kile kipigo nilipewa na maraia kutoka shule ya 10 siji kukisahau.

Nilikong’otwa kweli kweli mpaka wakaacha wenyewe maana nilikuwa napigiwa kwenye Dawati baada ya kukimbia toka uwanjani nikimSaka Grace nimshike nipone Kipondo.

Nilikuja kushtuka baadae nimelazwa kwenye nyasi na marafiki zangu napewa maji ninywe.

Wale Jamaa zangu walinisindikiza mpaka home nikiwa na Nundu Kama Zote usoni na Damu puani na mdomoni.

Baada ya kufika Home Mzee nae akaniongezea Stiki za kutosha kukazia.

Siji kusahau maana nilipigwa Kama Mwizi Aisee.

Mpaka kesho ,mtoto wangu acheze michezo yote lakini TOBO DUNDA AACHANE NAYO
 
Dodoma kipigo cha mbwa koko

2010, dodoma kulikuwa kuna bash royal village dogo wangu akanitunuku rafiki zake wawili niende nao, walikuwa wamevaa ovyo, party ikaisha mda wa kuondoka tunatoka nje tunaelekea kweny gari mob ikaanza kuwavuta wale mademu, ikabidi nikimbie fasta kuchukua gari mademu nimewaacha na mshkaji wangu wamezongwa zongwa, kurudi pale wademu wameingia mmoja seat ya mbele mwingine kakaa nyuma na mchizi, kufumba na kufumbua mob imezingira gari wanataka mademu, mara kioo kimevunjwa mlango umefungulia mademu wanavutwa wamebebwa juu juu ndio kushuka na mimi kwenda kuwaokoa, ebanaeeee nilichezea kichapo siyo cha nchi hii, nilichoropoka nikarudi hotelini, gari la aunt yangu nyang’a nyang’a, demu mmoja aliokolewa na mabaunsa mwingine aliliwa mtungo vichakani
Duuuh, kweli dunia ina mambo aiseee.....walipona lkn hao mademu?
 
Story yangu inaanza kama ifuatavyo baada ya kumaliza shughuli zangu za kuuza chipsi usiku napita karbu na nyumba ya jiran namsikia bwana mifugo akimwambia jiran yangu ambae ngombe wake alkuwa kasha dead amzike Mara moja kwani alkuwa ana anthrax basi nikaendelea kupeleleza nkaona alpomzka walipomaliza walivyoondoka nikaenda mfukua skuwa na gloves nikavaa mifuko ya Rambo maana nlsikia akisema ugonjwa ni hatar unaambukzwa na bacteria aina ya bacillus anthrax sjui kama nimepatia spelling au laa ila hayanihusu basi tuendelee na story basi bwana nikamuosha nikamkatakata vipande kesho nikamuuze mishkak vipande vilivyobakia nikampa mshkaj aweke kwenye freezer lake maana anatuchaj per day bwana nikauza wee mara watu wakaanza kuanguka baada ya kula wengne kutapika na kuhara palepale RAIA waliponishtukia wakaanza nikimbiza na mapanga wengine magongo sauti zilisikika zikisema "lazma tukukate vipandevipande" kwa bahat nzur kulikuwa kuna fuso sjui Lori hata skumbuk vzr lilikuwa linaanza kuondoka sjui lilikuwa linaenda WAP bas bwana nikalidandia baada ya masaa mawil mule ndan ya fuso simu yangu inaita mama mwenye nyumba anasema upo WAP mbona kuna polis wanakutafuta hapa nikakata Sm mara tena simu inaitaa kapiga RFK take yule mshkaj anatuifadhia nyama akasema nyama yako ina nn jamaa alikuibia kdogo kaenda itumia gheto sahiv ninavyokwambia tumemuwahisha hospital nikakata Sm .gar likiwa linaenda ktk kukaguakagua mule ndan nikakuta magunia kuyacheck ndani naona bangi pia kulikuwa na madawa mengne syajui kumbe skudandia fuso nilidandia kifo Mara gar likasimama kumbe hlo eneo kulikuwa na police patrol nkasikia shuken wote tukague gari
Baada ya hapo ilikuwaje mkuu? Hadi nimeogopa
 
Nimefikiria hayo "matapishi ya njano" halafu hapa nimekaa kwa mama ntilie nakula wali na dengu za "njano' (kama rangi ya hayo matapishi) Aggghhrrr..!!!;
Nimeacha kula kabisa!
Bwana Yesu asifiwe kwa wale wenzangu na mimi. Wengine habari zenu?

Ninapoelekea kutimiza miongo kadhaa ya kuwepo hapa duniani nimejikuta natafakari maisha yangu tangu pale nilipoanza kupata akili hadi leo hii nimejikuta natabasamu na kumshukuru sana Mungu maana nimekutana na mengi mazuri, mabaya, ya kukatisha tamaa ila katika yeye anitiaye nguvu nimeyaweza yote na nitaendelea kuyaweza yote.

Nimejikuta nakumbuka tukio moja la huko nyuma nikiwa na miaka sita hivi au saba (sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani). Mimi bwana nilikuwa naishi na sister tangu nikiwa mdogo sana na mpaka leo ukisikia nasema naenda nyumbani maana yake naenda kwa sister (naonekana kituko si eti eeh?)..tuachane na hayo kwanza.

My sister miaka hiyo alikuwaga mwalimu vijiji vya ndani kabisa huko, akiwa anaenda kuchukua mshahara anatumia siku tatu..siku ya kwanza kwenda, siku ya pili anaitumia kuchukua mshahara na kufanya mambo yake na hakukuwa ATM miaka hiyo kwa hiyo unaweza kupata picha na siku ya tatu anaitumia kurudi na wakati mwingine alikuwa anaweza kutumia hata siku nne.

Siku hiyo kabla hajasafiri alinunua kumbikumbi (wenyeji wa mikoa ya nyanda za juu kusini mtakuwa mnazijua, nilikuwa nazipenda sana) basi nilizifakamia zile ndude kama ugomvi, nilizikula kama lita moja hivi. Asubuhi ameamka zake hana hili wala lile akaondoka, mimi mida ya saa moja asubuhi nikaanza kuendesha, baadae nikaanza kutapika matapishi ya njano (mnaitaga nyongo sijui).

Kwa hiyo ikawa ni mwendo wa kuharisha na kutapika, sijui dawa yoyote na hata akili ya kwamba niende kwa jirani nikamwambie hali yangu nikawa sina sijui ndio utoto? Inafika mida ya saa nne mtoto nimechoka nikalala kwenye mkeka nje siwezi tena kusimama nikawa natapika hapohapo sina hata nguvu ya kusimama tena yaani nikawa nikifumbua macho hivi naona kila kilichopo mbele yangu kinazunguka. Ni miaka mingi imepita lakini picha ya siku ile haijawahi kunitoka.

Bahati nzuri akaja rafiki yake sister alikuwa hajui kama kasafiri ndio kunikuta katika hali hiyo akanibeba kunipeleka kwake maana kile kijiji hakikuwa hata na dispensary hadi kijiji cha jirani ... yule dada alikuwa anaitwa Fausta (RIP). Ndio ikawa pona yangu na sister alirudi baada ya siku tatu. Huwa najaribu kutafakari hivi asingekuwa yule dada kuja pale sister angenikuta niko hai kweli?

Tangu siku hiyo hakuwahi kuniacha peke yangu akisafiri maana siku zote nilikuwa najifanya konki siogopi kulala peke yangu. Tena wale wadudu niliwachukia jumla jumla sijawahi kuwala tenaa.

Kama na wewe mdau ulishawahi kupitia ugonjwa au hali yoyote ukaona kifo hiki hapa karibu tushee
 
Pole sana aiseeee.
 
Near death experiance ilinikuta darasa la 4 hiyo,tumechukuana wanne tukaogelee posta hapa pembeni ya pastoni.

Sasa pale kina chake tofauti na sehemu nyingine, hatua tano tu unazama ukizingatia nilikuwa mdogo.

Nakumbuka tulivua sare zetu za shule ya msingi maana tulitoroka shule siku hiyo.Hazikupita hata dk.10 nilikuwa naogelea maji ya kifuani si ndo nikarudi nyuma,kumbe hukohuko kwenye maji kuna shimo ghafla nilivyorudi nyuma hatua moja nikatumbukia.Nilipiga vikombe vyangu vya kutosha bahati nzuri mmoja kati yetu alikuwa darasa la 7 halafu ni mtoto wa bagamoyo,maji anayajua,basi ndo akaja niokoa,nikatoka nje nikawa nimekaa nalinda nguo macho mekundu nimetulia kama ndezi vile.Nashangaa shangaa
Khe khe [emoji1787] khe [emoji1787] khe[emoji1787] khe[emoji1787] khe
 
Story yangu inaanza kama ifuatavyo baada ya kumaliza shughuli zangu za kuuza chipsi usiku napita karbu na nyumba ya jiran namsikia bwana mifugo akimwambia jiran yangu ambae ngombe wake alkuwa kasha dead amzike Mara moja kwani alkuwa ana anthrax basi nikaendelea kupeleleza nkaona alpomzka walipomaliza walivyoondoka nikaenda mfukua skuwa na gloves nikavaa mifuko ya Rambo maana nlsikia akisema ugonjwa ni hatar unaambukzwa na bacteria aina ya bacillus anthrax sjui kama nimepatia spelling au laa ila hayanihusu basi tuendelee na story basi bwana nikamuosha nikamkatakata vipande kesho nikamuuze mishkak vipande vilivyobakia nikampa mshkaj aweke kwenye freezer lake maana anatuchaj per day bwana nikauza wee mara watu wakaanza kuanguka baada ya kula wengne kutapika na kuhara palepale RAIA waliponishtukia wakaanza nikimbiza na mapanga wengine magongo sauti zilisikika zikisema "lazma tukukate vipandevipande" kwa bahat nzur kulikuwa kuna fuso sjui Lori hata skumbuk vzr lilikuwa linaanza kuondoka sjui lilikuwa linaenda WAP bas bwana nikalidandia baada ya masaa mawil mule ndan ya fuso simu yangu inaita mama mwenye nyumba anasema upo WAP mbona kuna polis wanakutafuta hapa nikakata Sm mara tena simu inaitaa kapiga RFK take yule mshkaj anatuifadhia nyama akasema nyama yako ina nn jamaa alikuibia kdogo kaenda itumia gheto sahiv ninavyokwambia tumemuwahisha hospital nikakata Sm .gar likiwa linaenda ktk kukaguakagua mule ndan nikakuta magunia kuyacheck ndani naona bangi pia kulikuwa na madawa mengne syajui kumbe skudandia fuso nilidandia kifo Mara gar likasimama kumbe hlo eneo kulikuwa na police patrol nkasikia shuken wote tukague gari
Malizia story mkuu
 
Dodoma kipigo cha mbwa koko

2010, dodoma kulikuwa kuna bash royal village dogo wangu akanitunuku rafiki zake wawili niende nao, walikuwa wamevaa ovyo, party ikaisha mda wa kuondoka tunatoka nje tunaelekea kweny gari mob ikaanza kuwavuta wale mademu, ikabidi nikimbie fasta kuchukua gari mademu nimewaacha na mshkaji wangu wamezongwa zongwa, kurudi pale wademu wameingia mmoja seat ya mbele mwingine kakaa nyuma na mchizi, kufumba na kufumbua mob imezingira gari wanataka mademu, mara kioo kimevunjwa mlango umefungulia mademu wanavutwa wamebebwa juu juu ndio kushuka na mimi kwenda kuwaokoa, ebanaeeee nilichezea kichapo siyo cha nchi hii, nilichoropoka nikarudi hotelini, gari la aunt yangu nyang’a nyang’a, demu mmoja aliokolewa na mabaunsa mwingine aliliwa mtungo vichakani

Duuu.
 
Pole sana mkuu.
Naona huu uzi umekufit haswaa.

Lake chala, hili ziwa lipo mpakani mwa kenya na tanzania, nimechungulia kifo mara 2, nikasema sitakaa niende tena huko

1. Nilinusurika kuzama, ziwa lina kina kirefu sana hatua moja kutoka ulipo inatosha kabisa kukuzamisha, nimejifanya mtaalamu nikasogea kidogo, nikahisi kama kuna kitu kimenishika miguu kunivuta chini, nikazama, nikarudi juu nikazama tuna kurud juu kwa kasi nikamvuta jamaa aliyekuwa karibu mimi nikatoka, bahati jamaa alijitahidi kurudi nchi kavu

2. Tulienda kwa mara ya pili nikasema siogelei, nikakaa pembeni nimevua tshirt yangu mpyaa kwa ajili ya siku hiyo, mda wa kuondoka nikawa nimeisahau ile tshirt pale chini (huwa ninajiuliza sababu) nimeambaa na mawe umbali wa kutosha nikakumbuka afu wenzangu wametangulia daah, nikarudi na kuichukua, hapo hapo nasikia kitu kinanipush kupita njia nyingine tofauti na na tuliyoshukia (ziwa lipo kwa chini) nipo mwenyewe nimeanza kumake step ninaona bonge moja la nyoka ananiangalia daah hizo mbio zake halafu kwenye mawe makubwa, nikateleze nikaingia kwenye maji nikajitajidi nikatoka na kufanikiwa kuwapita hata wale wliokuwa wameanza safari wa kwanza kabisa...sitasahau hii
Nimekumbuka nyingine niligongwa na gari,

Hii ilinikuta mtoni pale himo, tulikuwa tumeenda kuogelea, wakati tunarudi askari nao wakawa wametoka kupeleka farasi wao, kuna farasi ambaye nilikuwa nimemzoea uncle wangu alikuwa anakuja nae home(kikosi cha farasi) alivyoniona akawa ananifuata mwenzake wanamfuata daah nkaingia uoga nilijikuta ninakimbia nikagongwa na gari, nakumbuka nilijikuta niko hospital naletewa mtori
Moshi town kukatwa na sime

Hii nayo ingenisababisha niage dunia, mshkaji wangu kabisa tulikorofishana, aliiba kitu home kwetu nikawa ninamwambi arudishe ugomvi ukaanzia hapo, iyo siku amerudisha nipo home nikamwambia mwanzo na mwisho kukanyaga home, ghetto nilikuwa nina sime ya kimasai jamaa aliivuta kaniletea shingoni nikahepa kidogo ikanichubua mpaka leo nina alama, ilienda kutua kwenye ukuta kwa namna ilivyo chimba ukuta isingeniacha salama
 
Kwa wale wanaojua flow ya maji ya mto, kuna mahala ambako unakuta maji yanarotate kwa speed ya ajabu, sehemu hii huwa na kina kirefu mnoo ni kama shimo refu katikati ya mkondo wa maji.

Kuna siku tukawa tunavuka eneo la hivi kwa kuruka upande mmoja kwenda mwingine kupitia mawe. Ile naruka keenda upande wa pili nikateleza nakuzama pale kati. Nilizinduka baada ya masaa mawili nikiwa nimezungukwa na ndugu na jamaa hosp.

Ila inshort wanasema ni muujiza tu maana rafiki zangu niliokuwa nao walikaa pale kwa dkk nzima niibuke nikaibuka mara ya 1 wakashindwa nidaka ya 2 pia wakashindwa ya 3 wakafanikiwa ila nikiwa sipumui kabisaa.

Yaliyoendelea ni kazi ya Mungu.
 
Lake chala, hili ziwa lipo mpakani mwa kenya na tanzania, nimechungulia kifo mara 2, nikasema sitakaa niende tena huko

1. Nilinusurika kuzama, ziwa lina kina kirefu sana hatua moja kutoka ulipo inatosha kabisa kukuzamisha, nimejifanya mtaalamu nikasogea kidogo, nikahisi kama kuna kitu kimenishika miguu kunivuta chini, nikazama, nikarudi juu nikazama tuna kurud juu kwa kasi nikamvuta jamaa aliyekuwa karibu mimi nikatoka, bahati jamaa alijitahidi kurudi nchi kavu

2. Tulienda kwa mara ya pili nikasema siogelei, nikakaa pembeni nimevua tshirt yangu mpyaa kwa ajili ya siku hiyo, mda wa kuondoka nikawa nimeisahau ile tshirt pale chini (huwa ninajiuliza sababu) nimeambaa na mawe umbali wa kutosha nikakumbuka afu wenzangu wametangulia daah, nikarudi na kuichukua, hapo hapo nasikia kitu kinanipush kupita njia nyingine tofauti na na tuliyoshukia (ziwa lipo kwa chini) nipo mwenyewe nimeanza kumake step ninaona bonge moja la nyoka ananiangalia daah hizo mbio zake halafu kwenye mawe makubwa, nikateleze nikaingia kwenye maji nikajitajidi nikatoka na kufanikiwa kuwapita hata wale wliokuwa wameanza safari wa kwanza kabisa...sitasahau hii
Kule siyo kuzuri mkuu usiende tena kabisa
 
Mimi nakumbuka vyenye nilipata ajali ya piki piki hapo Makumbusho nikitokea kwenye shughuli ya kuaga mwili wa classmate wa o'level alafu nawahi kupiga paper mahali.

Ilikua ni split-second event, nikajikuta katikati ya lami, mbele ya daladala kwa chini, derava wa daladala anatoa kichwa dirishani anauliza umeumia. Sikumjibu nikainuka hapo kila mtu ameduwaa magari yote yamesimama nikasogea pembeni nikamuona boda nae kainuka akachukua chombo chake akasoge nilipokuwa akaniuliza vipi umeumia.

Sikuumia hata kidogo wala mchubuko sikupata japo pikipiki ili slide pale kwenye lami kama mita 10 hivi. Boda nae hakuumia watu wanatuangalia tu akawasha chombo nikadandia hao tukasepa mwendo wa kidosi tukawaacha watu wasijue chakufanya.

Hii siku nilikua na rafiki yangu ambae yeye alishatangulia na boda yake, kufika namwelezea story ilivyokuwa mpaka leo huwa anabisha maana sikuwa na hata ushahidi wa jeraha zaidi ya vumbi vumbi kwenye jeans.
 
Daah inanikumbusha miaka 1996 nikiwa Mpanda, kipindi hicho nikiwa Secondary ili kila inapofika ijumaa nilikua natoroka kwenda machimboni kwakua kipindi hicho hela ilikua inapatikana kirahisi sana.

Nilikua nikifika huko naingia kwenye shimo lenye urefu wa zaidi ya mita ishirini, chini kabisa nilikua naingia ndani ya "fonka " liliokaa mfano wa chumba ambalo ndio nakwenda kuchimba katika mkondo wenye Dhahabu nyingi.

Kwakua nilihitaji pesa nilizoea kufanya shughuli hiyo kwa siri na sikutaka mtu yeyote shuleni na nyumbani ajue kama naendaga machimboni kwasababu nilikua bado mwanafunzi.

Siku moja tulipata jiwe kubwa la dhahabu na baada ya mgao nilipewa milioni 12 malipo ya mwanzo ila kutokana na umri wangu ilikua ni nyingi sana na siku hiyo niliamua kwenda kumpa dada angu aniwekee kisha nikarudi kwa kusubiria hela nyingine.

Tukiwa ndani walikuja jamaa wakiwa na silaha wakitaka wapewe pesa zote, watu walikula bakora siku hiyo ni balaa. Kuna brother mmoja nakumbuka alijisaidia pale pale. Mimi nilitumbukizwa kweny pipa la maji ikawa kila napotoa kichwa nje nakutana na kibao cha kichwani narudi kwenye maji,ilifikia muda nikapoteza fahamu nimekuja kupata fahamu jamaa wamechukua kila kitu lakini bahati yangu ni kwamba hela nilikua nishazipeleka kwa dada angu.

Pamoja na hayo sikuacha kwenda katika uchimbaji na kipindi hicho nikanunua kipimo cha zahabu ambazo zinapatikana juu juu ya kwenye ardhi nikawa naingiza pesa kwenye mashine na kwenye mashimo marefu niliendelea ku- hustle kama kawaida.

Siku moja nikiwa ndani ya shimo chini kabisa udongo ulikua ukiporomoka na maji yalikua yameanza kujaa hivyo nikawa nachota maji naweka kwenye ndoo kisha inavutwa maji yanamwagwa nje ya shimo lakini wakati shughuli inaendelea ulibomoka ukuta na kurudisha ndoo chini,mimi niliona giza ghafla hivyo nikakimbilia kwenye chumba cha shimo ambako nako hakuna njia ya kutokea. Hewa ilikua inapita lakini maji yalikua yakizidi kuongezeka hivyo nikajua lazima nife.

Kwamba mbaaali sana nilikua nasikia sauti za watu wakigombana kwamba waite polisi ndipo waje waanze kutoa udongo Lakin kuna jamaa yangu mmoja siji kumsahau, yeye alikataa akawaambia wachimbe kwanza wautoe mwili ndipo waite polisi kwasababu wakiacha muda mrefu bila kuwahi kuutoa mwili maji yanaweza kuwa mengi alafu ikawa shida ndipo kazi ikaanza.

Nashukuru Mungu kuna mmoja wao aliona mwanga wa tochi yangu kupitia kitundu kidogo sana,akawaeleza wenzake kwamba nitakua mzima kwasababu kama ningekua nimepoteza uhai tochi ingezama kwenye maji na isingetoa mwanga hivyo wakapiga kazi kwa kufuata mwanga mdogo wa tochi.

Kuna muda nikawa naita ila kwasababu ya kishindo cha sululu ya kuchimbia wakawa hawasikii baada ya muda walitoboa tundu angalau hewa ikaongezeka na tukawasiliana vizuri hadi nilipo okolewa kutoka kwenye fonka hiyo.

Tangu siku hiyo sikutaka kusikia tena habari za machimbo. Huko roho mkononi maana kazi ngumu, hatari ni nyingi na bado ukipata vihela kidogo majambazi wanakuvizia.
 
Back
Top Bottom