Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Ushasema Alikua na mabaya yake mengi Sana, usipoukemea ubaya wake atakuja kuibuka mwingine akifuata nyayo zake akijua ndio wengi wanapenda rais anaetafuta kiki kuliko usawa wa haki.
 
Umechambua vizuri sana kuhusu kukubalika kwa Magufuli.

Lakini jambo mmoja unatakuwa ulitambue ni kwamba sio kwamba Watu wanapenda kumshambulia bali ni namna ya utendaji kazi wa mambo unavyofanyika.Katika siasa na hata utendaji wa kawaida watu hutoa matamko kwa ulinganisho wa matukio yaliyopo,yaliyokuwepo na future.

Sasa katika hilo kutokana na Mtawala aliyopo ambaye hana sifa kama za Magufuli na katika kurekebisha mambo yaliyopita,kwa vyovyote vile ni lazima utataja jina la Magufuli maana ndio alikuwa Champion wa mambo mengi,Kama ingetokea Mama SAMIA ana sifa kama za Magufuli kiutawala basi jina LA Magufuli lingekuwa linatajwa kwa njia ya kusifu lakini kiongozi huyu mlengo wake ni tofauti.

Kutokana na hatua hizo za watu kufanya reference katika maongezi hata iweje Jina LA Magufuli litaendelea kutajwa tu tena kwa Ubaya labda ipite Tawala zaidi ya mmoja.
 
Watanzania wengi hawakumpenda Magufuli kwa kuwa aliwanyanyasa tabaka la juu.

Katika Uongozi wa Magufuli tulishuhudia improvement kubwa sana katika huduma za kijamii. Watanzania wengi walikuwa wahanga wa huduma mbovu, na sasa tunarejea huko kwa kasi ya ajabu...
Ndugu yangu kiongozi bora anapimwa kwa vitu vitatu tu. Kusikiliza, kuheshimu na kuwatii wale anaowaongoza. Bahati mbaya sana Magufuli hakuwa na sifa hata moja katika hizo. Magufuli alikuwa mbabe, mkatili na mjuaji kwenye kila kitu.

Magufuli hakupendwa na watu bali alilazimisha aonekane anapendwa na kila mtu, ndio maana baada ya kufa kwake hata wale wasaidizi wake wa karibu wameamua kumgeuka na kumkana, maana wanajua hakupendwa kiuhalisia.

Kuhusu wamachinga na mama ntilie kutetewa na Magufuli wafanye biashara holela ule ulikuwa ni uhuni wa kiongozi kuvunja sheria ili aonekane anawajali. Sio kipimo sahihi cha uongozi bora.
 
Zitto huwa anajiona ana akili kumbe hamna kitu , yeye anafikiri adui yake ni magufuli wakati adui yao ni ccm. Kosa hilohilo linafanywa na chadema ambao wanagombana na zitto au wanamsema magufuli huku wanaiacha ccm.

Wameacha kujadili ripoti ya cag, mfumuko wa bei vitu vinavyogusa watu wanamjadili magufuli kwa kifupi wanacheza muziki wa ccm.
 
Watanzania wengi hawakumpenda Magufuli kwa kuwa aliwanyanyasa tabaka la juu, hapana.

Katika Uongozi wa Magufuli tulishuhudia improvements kubwa sana katika huduma za kijamii ambazo kimsingi Watanzania wengi walikuwa wahanga wa huduma mbovu kabla yake, na sasa tunarejea huko kwa kasi ya ajabu...
Kilichowagusa watu wa chini pekee ni elimu bure lakini hivyo vingine sidhani Kwa kweli.
 
Zitto anajua yeye na chama chake haitaji kura za wananchi hasa huku bara, ameshapata anachotaka huko Zanzibar anagawiwa vinono kwenye, sahani ameshaisahau njaa aliyoipata wakati wa Magufuli.

Ujuaji wake alijaribu kugombea Mbagala akapigwa, akadhani CCM watamuachia tu, ndio akaibuka na madai ya Tume Huru, kwake Katiba Mpya haina maana, ni mwanasiasa cheap anayetumika kila wakati na watawala hasa wakiwa wa "upande" wake.

Kama akija na madai kumhusu Magufuli, basi aje na uthibitisho, sio anakuja na maneno matupu, hii inaonekana kabisa ana chuki binafsi, au anatumiwa na kundi la watawala linalomlea siku hizi.
 
Zitto huwa anajiona ana akili kumbe hamna kitu , yeye anafikiri adui yake ni magufuli wakati adui yao ni ccm. Kosa hilohilo linafanywa na chadema ambao wanagombana na zitto au wanamsema magufuli huku wanaiacha ccm.
Wameacha kujadili ripoti ya cag, mfumuko wa bei vitu vinavyogusa watu wanamjadili magufuli kwa kifupi wanacheza muziki wa ccm.

Tanzania wote ni CCM Mkuu sijui kama Hilo walijua. Kidogo aliyejaribu ni Tundu Lisu. Ila wengine sinaimani nao
 
Kiburi wanapata kwa dada maana nae anamnanga kaka Sasa wadogo wataachaje!.. Mkuu usiseme hakuna maskini ambao hawakufaidika na awamu hiyo kiuchumi unahabari huko geita wachimbaji wadogo wadogo walineemeka! Ila kwa ninayosikia sahivi ni yale ya kufurumushwa!.

Kitendo cha hata kuleta nidhamu serikalini tayari ni neema maana watu watahudumiwa ipasavyo.

Kelele za umeme zilikuwa hakuna umeme unatumika na watu wote na ukiwa stable faida twapata sote.

Unakumbuka alizuia uvuvi kwa miezi kadhaa, unafikiri ilikuwa ni kwa faida ya nani kama sio taifa kiujumla japo na hao wavuvi wakiwemo watu wa chini aliwagusa!.

Leo hii wamachinga alivyowagusa kwa kuwaachia uhuru wa kutengeneza vipato vyao hatuwezi kusema hakuna alieneemeka kiuchumi!.

Maswala mengine ya kuvunja nyumba yaangaliwe kwa weledi mtu anavunjiaa nyumba kwa haki au sio haki maana watu wengine ni wabishi tu!.. Kama huko dar watu wanakaa kwenye mabonde Tanzania inaeneo kubwa tu na wakipata majanga serikali ndo inalalamikiwa..😁

Leo atanangwa juu ya covid lakini twende ndani turudi nje mzee alifanya maamuzi sahihi juu ya lile swala,hilo gonjwa tutaishinalo tu hata huko nje sasa wanaishinalo.

Magufuli hakukataa chanjo ila alitaka uhakika wa chanjo hizo kama ni salama kwanza.

Kinachofanyika sasa ni kutoa ile imani ya utendaji Kama wa magufuli ndani ya akili za watu!,maana watu wanaamini ule utendaji wake kama ndio kiongozi anavyopaswa kuwa maana waliopo wanajua tutawahukumu kwa kumtumia magufuli kama mfano!..

😅
Mfano swala la upatikanaji wa umeme lilivyoanza kusuasua ni mashahidi tosha watu walianza kupiga kelele!,hii ni kwasababu tulishazoeshwa huduma hii kutokuwa ya kusuasua ktk awamu yake!.

By the way kila mtu ahukumu vile aonavyo ila mzee angepewa muda wa kutosha vingebadirika vingi!,Kama ni mtu unaejua kuwaza vyema utajua taifa letu limekosa nini.
 
Kiburi wanapata kwa dada maana nae anamnanga kaka Sasa wadogo wataachaje!.. Mkuu usiseme hakuna maskini ambao hawakufaidika na awamu hiyo kiuchumi unahabari huko geita wachimbaji wadogo wadogo walineemeka...

Tatizo la Mzee bado hujalijua tuu Mkuu?

Ulimwengu WA sasa hautaki mtu kuwafanya watu wawe Sawa yaani kuleta ujamaa katika Karne ya 21 ni kujitafutia vita usiyoiweza.

Zaidi jpm alifanikiwa kwenye propaganda
 
Kwema .

Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea simu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.
Taikon Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
Rekebisha tuu hapo kwenye red najua ulimaanisha kuandika sumu, ukaandika simu.
Naunga mkono hoja.
P
 
Tatizo la Mzee bado hujalijua tuu Mkuu?
Ulimwengu WA sasa hautaki mtu kuwafanya watu wawe Sawa yaani kuleta ujamaa katika Karne ya 21 ni kujitafutia vita usiyoiweza.

Zaidi jpm alifanikiwa kwenye propaganda
Kwahiyo wenye system yao wanataka wakubwa wabaki wakubwa na wadogo wabaki wadogo wasikue!.. nimekupata mkuu..😃
 
Tatizo lililopo ni hao wanaojiita wanyonge kueendelea kumsifia hata alipokuwa amekufa ina saidia nini walioumizwa ni wengi kuliko walionufaika asilimia kubwa ni wale wasiojitambua kama wameumizwa na badala yake waliishia kushangilia tu bila kujielewa
Unaongea ukweli mkuu,kuna watu Magufuli aliwaumiza moja kwa moja kama kuwafungia biashara,kuwaweka ndani,kuvunja nyumba zao,kuwatumbua e.t.c hao hata uwaambie nini hawawezi kuona mazuri ya Magufuli na kuna watu wa hali ya chini ambao wameona ujenzi wa miundo mbinu nao huwezi kuwaambia kitu,so mwisho wa siku tutaishia kuingia kwenye mgogoro ili hali muhusika ameshafariki.Sijui watu wanajaribu kuachieve nini kumsema Magufuli daily.
 
Ndio maana nawashauri viongozi Kama kina Zitto Kabwe wawaachie watu wa mitandaoni mambo haya kwani wao hawana chakupoteza Ila Kwa Viongozi Kama wao haiwezi kuwa nzuri kwao Kisiasa
Bado mimi naamini mtu kama Zitto tutamkumbusha wakati wa kampeni juu ya hiki anachokifanya.

Busara ni kutbua kuwa kwa kadri ya kipimo cha chuki uliyonayo juu ya JPM.... Kipimo hicho hicho cha upendo na heahima juu ya Magu kimo kwenye mioyo ya Watanzania wengi
 
Kwahiyo wenye system yao wanataka wakubwa wabaki wakubwa na wadogo wabaki wadogo wasikue!.. nimekupata mkuu..😃

Ndivyo Dunia ilivyomkuu!

Hata Lusifa alipojaribu kutaka nafasi ya Mungu tunajua kilichompata, akaitwa Shetani na mpaka leo watu wanamlaumu pasipo hata kumpa nafasi ya kujitetea!😀😀

Nisiseme MENGI
 
Ujinga kweli ni kumshambulia aliyekufa lakini ni ujinga zaidi kumsifia mtu aliyekufa na hili ndiyo tatizo kubwa
Umenena vyema sana,
Na ukifanya tathimini ya kina uku mitaani utaona ni Jinsi gani JPM anapendwa sana na walalahoi na baadhi ya wachache waliokuwa wanachuma mkate wao ki halali.....
 
Back
Top Bottom