Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Hakuna atakayemsema Hayatti Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa chini.

Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea sumu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.

Magufuli anamabaya yake mengi mno, lakini pia hatuwezi kujidanganya kuwa anamazuri yake pia mengi tuu.

Hayo mazuri aliwafanyia kina man? Kisha hayo mabaya aliwatendea kina Nani?
Hapo ndipo tunaweza kukokotoa mlinganyo huo, ili Wale wakosoaji na wanaomtukana Magufuli waone Kama watafaidika au laah!

Tabaka la juu la wasomi, Wataalamu, matajiri, na wafanyabiashara, wanasiasa wa Vyama vya upinzani Kwa kweli walionja joto la jiwe. Wapo waliolia kuhusu Ajira, wapo waliolalamika kutekwa na kupotezwa, wapo waliotiwa Korokoroni Kwa kesi za uhujumu uchumi, wapo waliofunguliwa kesi za ugaidi, wapo waliofunga biashara zao n.k. kundi hili sio watu wengi ukilinganisha na Kundi la Tabaka la chini.

Tabaka la chini, la watu wasiosoma, Masikini hohehahe, wasio na Vyama, vibarua, Machinga na Mama ntilie, na watifua udongo(Wakulima wadogo) hawa walimpenda Magufuli Kwa sababu mbili kuu, mosi walimuona Kama mtetezi wao; pili, Kwa kuleta kilio Kwa Tabaka la juu.

Masikini wengi sio kama maisha yao yalibadilishwa na JPM, hilo halikutokea Ila walifurahia jinsi jpm alivyokuwa akiwahenyesha mavi matajiri, wafanyabiashara na akiwafokea na kuwadhalilisha wasomi na Wataalamu. Unajua Masikini anamsemo wake usemao; msiba wa wengi ni sherehe, hivyo awamu ya JPM ilikuwa ni sherehe Kwa masikini kwani sio wao tuu waliokuwa wakiteseka bali haya matajiri walikuwa wakiteseka Kwa namna Yao.

Sasa kitendo cha JPM kufariki, kilikuwa ni huzuni Kwa Tabaka la chini kwani mtetezi wao na kuumiza tabaka la juu hayupo tena. Sasa msiba umebakia tabaka la chini, tabaka la juu limeanza kuneemeka Kwa Kula asali ya nchi.

Ukweli ni kuwa Nchi hii zaidi ya 80% ni Tabaka la chini. Hivyo kumshambulia Magufuli ni kushambulia Watanzania waliowengi. Kuwazomea, kuwakashfu, JPM Kwa tabaka la chini ni Kama Mtume au Nabii wao aliyekuja kuwakomboa lakini ungejiuliza kuwakomboa na kitu gani? Maana Kama ni umasikini bado wanao na hawana Mabadiliko yoyote yale, ndipo hapo nikakuambia kuwa labda ni Kwa sababu alifanya Tabaka la juu lihenyeke na hiyo ni sherehe Kwa tabaka la watu masikini.

Wengine tulimkosoa Magufuli akiwa hai tukiwa na Nia nzuri tuu, wala hatukuwa na chuki naye isipokuwa kuwekana Sawa. Lakini ameshakufa tunamuwekaje Sawa marehemu aliyekwisha kufa na kuzikwa. Kama ni chuki nafikiri ingekuwa imeisha ndani ya miezi sita tangu alipozikwa lakini kinachoendelea sasa hivi kinashangaza.

Hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai.

Zitto Kabwe na wengine wote mnaomshambulia JPM hakuna faaida yoyote mtakayoipata katika Jambo Hilo, zaidi Sana mnapoteza kukubalika Kwa Watanzania waliowengi ambao ni Wafuasi wa jpm waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wa matajiri ambao masikini huwaona Kama mafisadi na wezi wa Mali za nchi. Ambao masikini huwaona matajiri ndio wanaowasababishia umasikini wao

Huwaona matajiri ndio waliowasababishia wasisome
Ambao huwaona matajiri ndio wanaowatesa viwandani Kwa kuwalipa mishahara midogo.

Taikon Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
 
Unaongea ukweli mkuu,kuna watu Magufuli aliwaumiza moja kwa moja kama kuwafungia biashara,kuwaweka ndani,kuvunja nyumba zao,kuwatumbua e.t.c hao hata uwaambie nini hawawezi kuona mazuri ya Magufuli na kuna watu wa hali ya chini ambao wameona ujenzi wa miundo mbinu nao huwezi kuwaambia kitu,so mwisho wa siku tutaishia kuingia kwenye mgogoro ili hali muhusika ameshafariki.Sijui watu wanajaribu kuachieve nini kumsema Magufuli daily.
 
Umenena vyema sana,
Na ukifanya tathimini ya kina uku mitaani utaona ni Jinsi gani JPM anapendwa sana na walalahoi na baadhi ya wachache waliokuwa wanachuma mkate wao ki halali...

Chuki kubwa sana ni baadhi ya janjajanja wachache waliozibiwa mianya yao ya upigaji ama waliotumbuliwa(hasa wako huku mitandaoni),wanachuki kuu mana wako wengine mpaka sasa bado hawaja recover.

Kumshambulia JPM ni kama kupunguza machungu yao miyoni mwao lakini haisaidii mana bwana yule hayupo katika ulimwengu wa kawaida..

Ujinga ni kwamba wanamshambulia mtu alishakufa...
Unafurahishwa na kifo chake ila ameshaishi maisha ya neema kuu na alishamaliza ujana aliuanza uzeee...

Amekaa serikalini zaidi ya miaka 20 ya Neema,

Je ni bata gani hakula?

Kaacha legacy wewe ukifa utaacha nini dunia?ama ni hizi comments zako za chuki kujaza servers za jf?

Ukifikiri urais na nafuu kwa nini usigombee wewe tuone kama kana maali unaweza fika.

Kumbuka hakuna atakayeishi milele,kifo ni lazima no matter utaishi vipi...so wakati wake ulifika ni jambo la wakati tu,na sisi tunaoshangilia zamu yetu inakuja.
 
Umenena vyema sana,
Na ukifanya tathimini ya kina uku mitaani utaona ni Jinsi gani JPM anapendwa sana na walalahoi na baadhi ya wachache waliokuwa wanachuma mkate wao ki halali....
Ndio maana nawashauri viongozi Kama kina Zitto Kabwe wawaachie watu wa mitandaoni mambo haya kwani wao hawana chakupoteza Ila Kwa Viongozi Kama wao haiwezi kuwa nzuri kwao Kisiasa
 
Unaongea ukweli mkuu,kuna watu Magufuli aliwaumiza moja kwa moja kama kuwafungia biashara,kuwaweka ndani,kuvunja nyumba zao,kuwatumbua e.t.c hao hata uwaambie nini hawawezi kuona mazuri ya Magufuli na kuna watu wa hali ya chini ambao wameona ujenzi wa miundo mbinu nao huwezi kuwaambia kitu,so mwisho wa siku tutaishia kuingia kwenye mgogoro ili hali muhusika ameshafariki.Sijui watu wanajaribu kuachieve nini kumsema Magufuli daily.
hy kukubalika na watu wa hali ya chini mpk sasa ili hali hayupo.ndo kinafanya wamseme ili watu hao wamkatae
 
Moja Kati ya kitu siwaelewi hawa wakosowaji ukiwafuatilia comment zao wenyewe wanasema Magufuli anapendwa na watu wengi wasio na elimu na Masikini na kweli ipo hivyo lakini hao hao wanasema Uchaguzi wa mwisho Magufuli aliiba kura na hakustahili kushinda kwasababu wananchi walimkataa but kiuhalisia hao watu wanasema Wanaompenda Magufuli ndio wapo wengi inchini kuliko hata wasomi hapo ndio wanajitekenya na kucheka wenyewe kiufupi hata siwaelewi vizuri
 
Magufuli alishakufa.
Tuachane naye, hana jipya au jema la kuja kutufanyia sasa. Chuki dhidi ya Magufuli na wapambe wake zitaendelea milele maana Magufuli alizipandikiza na kuzikuza mpaka kumea. Kwa sasa tunavuna chuki alizozipanda yeye mwenyewe.

Ni kama ilivyokuwa kwa Hitler kule Ujerumani, mpaka leo hii kumbukumbu za ukatili wake zipo japokuwa ni mtu aliyeacha Legacy kubwa kwa wajerumani.
 
Moja Kati ya kitu siwaelewi hawa wakosowaji ukiwafuatilia comment zao wenyewe wanasema Magufuli anapendwa na watu wengi wasio na elimu na Masikini na kweli ...
Kura za Urais Kwa kweli hazikuibwa hilo ni dhahiri Ila za ubunge Nina mashaka nazo Kwa sehemu kubwa.

Magufuli alipita Kwa kishindo, kwenye watu Mia wanaonizunguka 95% walimchagua Magufuli Mimi na wengine wachache ndio hatukumchagua. Kufikia hapo hata kabla matokeo hayajatangazwa nikajua Lissu kagaragazwa vibaya mno
 
Moja Kati ya kitu siwaelewi hawa wakosowaji ukiwafuatilia comment zao wenyewe wanasema Magufuli anapendwa na watu wengi wasio na elimu na Masikini na kweli ipo hivyo lakini hao hao wanasema Uchaguzi wa mwisho Magufuli aliiba kura na hakustahili kushinda kwasababu wananchi walimkataa but kiuhalisia hao watu wanasema Wanaompenda Magufuli ndio wapo wengi inchini kuliko hata wasomi hapo ndio wanajitekenya na kucheka wenyewe kiufupi hata siwaelewi vizuri
Kwa hiyo wewe unaamini mwaka 2015 au 2020 Magufuli alishinda kihalali kwenye uchaguzi?

Pole sana ndugu.
 
Magufuli alishakufa.
Tuachane naye, hana jipya au jema la kuja kutufanyia sasa. Chuki dhidi ya Magufuli na wapambe wake zitaendelea milele maana Magufuli alizipandikiza na kuzikuza mpaka kumea. Kwa sasa tunavuna chuki alizozipanda yeye mwenyewe.

Ni kama ilivyokuwa kwa Hitler kule Ujerumani, mpaka leo hii kumbukumbu za ukatili wake zipo japokuwa ni mtu aliyeacha Legacy kubwa kwa wajerumani.

Kwa Viongozi kutamka hadharani sidhani Kama Una Afya kwao hasa hawa viongozi chipukizi
 
Watanzania wengi hawakumpenda Magufuli kwa kuwa aliwanyanyasa tabaka la juu, hapana.

Katika Uongozi wa Magufuli tulishuhudia improvements kubwa sana katika huduma za kijamii ambazo kimsingi Watanzania wengi walikuwa wahanga wa huduma mbovu kabla yake, na sasa tunarejea huko kwa kasi ya ajabu.

Magufuli alileta elimu bure, aliwasaidia Watanzania wengi sana. Takwimu zinathibitisha hili baada ya wanafunzi wengi sana kuongezeka.

Magufuli alitatua kero za wanyonge na walioonewa ambao walishaomba msaada kwa wasaidizi wake karibu wote bila kusaidiwa, unategemea wamchukie?

Magufuli alilinda rasilimali za nchi. Tulifikia wakati hadi twiga wanapanda ndege! Unatarajia Watanzania wengi tungemchukia?

Magufuli aliwatetea machinga na mama ntilie, nao wakawa walau na uhuru wa kufanya boashara zao halali kwa amani ili kupata vipato vya kusaidia familia zao. Unatarajia wangemchukia?

Walimpenda kwa kuwa alikuwa kiongozi bora, not kwa kuwa aliwahenyesha matajiri. Magufuli hakuhenyesha matajiri, alihenyesha wapigaji.
 
Kura za Urais Kwa kweli hazikuibwa hilo ni dhahiri Ila za ubunge Nina mashaka nazo Kwa sehemu kubwa.

Magufuli alipita Kwa kishindo, kwenye watu Mia wanaonizunguka 95% walimchagua Magufuli Mimi na wengine wachache ndio hatukumchagua. Kufikia hapo hata kabla matokeo hayajatangazwa nikajua Lissu kagaragazwa vibaya mno
Hivyo ndio unavyojidanganya?

Eti Magufuli hakuiba kura 2020!

Bora hata huo ubunge au udiwani huenda wizi wa kura ulifanywa kwa aibu, lakini kwenye Urais ilikuwa ni lazima wizi ufanyike kwa kiwango cha SGR ili Magufuli abakie madarakani.
 
Back
Top Bottom