kipusatembo
Member
- Jun 19, 2014
- 88
- 29
Robby acha tu kaka wamama wa kichagga mtoto hakuagi........ Yaan na ukubwa wangu hadi leo bado namgwaya maana hakawii kunichenjia........ Afu si unajua wale mamaza ye ndo faza pia ni shidaaa....
Robby acha tu kaka wamama wa kichagga mtoto hakuagi........ Yaan na ukubwa wangu hadi leo bado namgwaya maana hakawii kunichenjia........ Afu si unajua wale mamaza ye ndo faza pia ni shidaaa....
Tulikuwa tunafuga mbwa home ,baba alikuwa na kawaida ya kila wikend akitoka job anarudi na furushi la mabaki ya vyakula vinono kwa ajili ya chakula cha mbwa...........siku hiyo nakumbuka alileta ukoko wa pilau ulokuwa umechanganyikana na mchuzi na mabakibaki ya nyama za kuku,baada ya shughuli zake akawa amewatengea wale mbwa kwenye chombo chao kila mbwa na sahani yake....... Bwana weeee nkaona mbwa wanafaidi, nkicheki pilau kula hadi xmas haa nkamtaimu mzee katoka tu pale nkazama kwa mbwa mmoja ye anakula huku mi huku .........kilichokuja kutokea baadaye nilishtukia nimedakwa juujuu nilichezea bakora nashukuru mama alikuwepo akaniokoa .........dah RIP my dadi jamani loh!!
Mimi nlikuwa na tabia ya kuaga shule naenda kusali ijumaa kumbe mze naenda zangu beach aga khan kuogelea.
Sasa siku ya siku nmetinga beach kama kawa nmevua nguo zangu nimeweka kwny begi naingia kuogelea na chu.pi(michael phelps)...natoka kuogelea begi halipo ma-beach boy wameiba uniform na madaftari yote wamechukua.
Nkakaa mpk giza limeingia ndio naanza kurudi home na chu.pi yangu V.I.P...nkakuta home wamenitafuta sana mpk school wameenda na police wamefika.
Nlichezea kipigo hatari halafu dingi anakwambia kachume fimbo mwnyw.
R.I.P Baba.
Mimi umabo wangu ulikuwa coco beach mkuu.
Mm aga khan cz haikuwa mbali na home na xul nayosoma
hahahahahahahs kumbe ulikuwa mtukutu
hahah Hii kubwa kuliko naimagine ulikuwa na miaka mingapi
Mimi labda nisimulie: Kisa cha Siku Niliyojua Kuendesha Baiskeli
Nina kaka wawili, Kiokote na Fidodido.
Kaka yangu mkubwa aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rau (W) Moshi (M) Kilimanjaro alipata matokeo yake ya darasa la saba ambapo kwa bahati nzuri alikuwa amefaulu na kupangiwa kwenda kujiunga na shule ya Upili ya Mawezi iliyopo mkoani hapo hapo Kilimanjaro. Ni tukio la kufurahisha hasa kama ulikuwa ukimfahamu. Jina la utani aliitwa, 'kiokote'. Alikuwa mtundu sana. Siku hizi amekuwa mpole hadi wanamwita 'mchungaji'.
Siku moja kaka Kiokote alitoroka shule na kwenda kuiba maembe kwa jirani (maeneo ya kule Rau). Walikula maembe mengi (na yalikuwa mabichi) kiasi kwamba jioni yake alikuwa akiumwa tumbo.
Mama akamuuliza, "Kiokote kwani leo umekula nini shule?"
Kiokote akajibu, "Nimekula maembe tu mama".
Mama akamuuliza tena, "Maembe mangapi kiokote?"
Naye akajibu, "si mengi mama...kama kumi tu!!!"
Siku nyingine kiokote alitoroka shule akaenda kucheza, wakiwa mchezoni akadondokewa na utomvu wa mti fulani hivi (kama umewahi kuangalia movie ya 'The Gods Must be Crazy' utaelewa). Utomvu wake unawasha sana na pengine huweza kuleta upofu. Kiokote alirudi nyumbani huku macho yamemvimba. Mama kwa upendo kwanza (na ni bahati tu alikuwa ananyonyesha) akamwekea maziwa yale machoni akapona. Ila kichapo cha kutoroka shuleni alikisimulia wiki nzima iliyofuata.
Fidodido yeye alikuwa na utundu wa aina yake. Yeye alipenda sana mpira na wasichana. Alikuwa akinishawishi tutoroke shule tukajifiche uwanja wa mpira wa Ushirika hadi muda ambapo watu wanakuja kufanya mazoezi tunashuka tunacheza nao. Jioni tulikuwa tunawasubiri wenzetu watoke shule tunachukua madaftari yao na kukopi notes zao kisha tunarudi nyumbani. (baba yetu alikuwa mkali sana, hivyo lazima tuandike notes).
Siku nyingine kama baba hakukagua notes jana yake, tulikuwa tunakata notes za jana zinakuwa mara mbili, yaani tarehe ya jana na ya hiyo siku.
Fidodido, pia alikuwa akitoroka shule kwenda kufukuzia wasichana, hasa wale waliokuwa mbele yake kimadarasa. Alikuwa na pamba yake moja tu..tshirt nyeupe yenye mchoro wa fidodido nyuma. Hapo ndipo jina lake lilipoanzia. Ukimuona na hiyo nguo wewe jua tu anaelekea Shanty town kuwafuata watoto wa geti kali waliokuwa wakisoma ama Shule ya msingi Kilimanjaro au Kibo.
Anyway, baada ya kiokote kumaliza darasa la saba, baba alimuahidi kuwa akifaulu atamnunulia baiskeli. Hivyo baada ya kupata matokeo tulifurahi sana kwani tulijua na sisi tutakuwa tunaiendesha. Baba alimnunulia baiskeli fulani hivi ambazo breki yake ni kurudisha pedo (paddles) nyuma. Lakini ilikuwa ndefu kama zile PHOENIX. Kwa kaka kiokote ilikuwa ikimtosha. Kwangu mimi ilikuwa shida kwani sikuweza kuendesha.
Siku moja baada ya kuwang'ang'aniza wanifundishe kuendesha baiskeli wakanipakia kwenye baiskeli huku wameishikilia. wakawa wananisukuma huku wapo karibu. Mimi kwa ufupi wangu nilikuwa nakaa tu na kuweka miguu kwenye pedo ambapo nikitaka kusimama, narudisha pedo nyuma, baiskeli inasimama na kama hakuna mtu karibu basi nitaanguka..hivyo ndiyo nilizoea kushuka kwenye baiskeli hiyo kubwa.
Siku hii tulienda kucheza maeneo ya Ushirika (sasa MUCCoBS). Wakanipakiza kwenye baiskeli kama kawaida huku wamenishikilia. Hapo tulikuwa eneo yalipokuwa mabanda ya ng'ombe, kuku na nguruwe (kwa waliokuwa wanapafahamu...na kwa sasa unaweza kusema ni ile barabara ya chini ya magorofa ya O, N, M...). Wakanisukuma kisha wakaniachia. Baiskeli ilianza kwenda kwa mwendo wa kawaida na kwa kuwa miguu ilikuwa kwenye pedo bado niliweza kupunguza mwendo.
Baada ya muda mwendo ukaanza kuongezeka nami nikawa nakaribia kufika mwisho wa barabara, yaani kufikia makutano ya ile barabara ishukayo geti la chini la MUCCoBS. Hapo nilikuwa na options mbili tu; kuendelea na kugonga fensi ya shanti town au kushuka chini kuelekea getini. Nilikunja kona kushoto na kuki-face kiteremko kile cha kwenda geti la chini.
Hapo ndipo kimbembe kilipoanzia. Baada tu ya kukunja kona nilikumbana na bump moja. Hili halikuwa kubwa hivyo nilifanikiwa kuliruka huku baiskeli ikiongeza spidi. Mbaya ni kwamba, baada ya kuruka bump lile miguu ilitoka kwenye pedo hivyo kuua kabisa matumaini yeyote ya mimi kuweza kupunguza mwendo au kusimama kabisa.
Basi baiskeli ikaserereka huku ikiongeza mwendo kama vile gari. Ilikuwa ikienda spidi ambayo sijawahi kuielewa. Hapo ninayapita yale manyumba yaliyoandikwa BGL (baada ya kukua ndio nilikuja kugundua zile BGL zilimaanisha BUNGALOW)..Zikaanza BGL 1, BGL 2, BGL 3, yaani zilikuwa zinaenda mbio sana.
Kati ya BGL 8 na BGL 9 kuna boonge la bump (maeneo ya SEMINAR BLOCK pale). Nilipolifikia sikujua la kufanya. Nilikuja kushtuka niko Mawenzi hospitali na maumivu makali mguuni. Nilikuwa nimeumia sehemu ya goti ambapo ilinibidi kushonwa. Kaka zangu hawakujua nilipokuwa kwani wao baada ya kunisukuma waliendelea kucheza wakitarajia nitarudi nikiwa naikokota baiskeli hivyo wao walijua lazima nitachelewa kurudi.
Ni bahati mmama mmoja alikuwa akiishi (kama sikosei BGL 7 na kama sikosei aliitwa mama Kimwaga) ndo alinikuta na kunipeleka hospitali (na hakuwa akinifahamu kabisaaaa). Ni hadi nilipoamka ndipo nilipoweza kuwaelezea madaktari kuwa mimi ni nani na nyumbani ni wapi. Jioni wazazi walikuja kunichukua na kunirudisha nyumbani. Baba alikuwa amekasirika sana ila kwa ugonjwa wangu adhabu yangu iliwaangukia kaka zangu.
Baada ya kupona nilikaa kama miezi mitatu na siku nilipopakia baiskeli ilikuwa kama nilikuwa nafahamu siku nyingi. Niliamini ule usemi, "Lazima upate ajali ndio ujue kuendesha baiskeli". Kila nikiliangalia hili kovu langu hapa mguuni huwa naikumbuka ile siku...utoto raha, ila very risky..lakini nakumbuka zaidi kama, "SIKU NILIYOJIFUNZA KUENDESHA BAISKELI"
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
Tulikuwa tunafuga mbwa home ,baba alikuwa na kawaida ya kila wikend akitoka job anarudi na furushi la mabaki ya vyakula vinono kwa ajili ya chakula cha mbwa...........siku hiyo nakumbuka alileta ukoko wa pilau ulokuwa umechanganyikana na mchuzi na mabakibaki ya nyama za kuku,baada ya shughuli zake akawa amewatengea wale mbwa kwenye chombo chao kila mbwa na sahani yake....... Bwana weeee nkaona mbwa wanafaidi, nkicheki pilau kula hadi xmas haa nkamtaimu mzee katoka tu pale nkazama kwa mbwa mmoja ye anakula huku mi huku .........kilichokuja kutokea baadaye nilishtukia nimedakwa juujuu nilichezea bakora nashukuru mama alikuwepo akaniokoa .........dah RIP my dadi jamani loh!!