Namtumbo: Wazazi waacha kupeleka Watoto Shuleni wakiaminishwa Yesu Kristo anakaribia kurudi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya amefanya msako wa Wanafunzi ambao hawajaripoti Shule za Msingi na Sekondari Vijijini ambapo katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa Mtumishi wa Mungu Erick Manyanya (33) Mwinjilisti wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua Kanisa Kijijini hapo akiwahubira Wazazi wasiwapeleke Watoto Shule kwakuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda Shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni Kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri akaacha Chuo na kwenda kuanzisha Kanisa hilo Namtumbo “Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa Mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu, mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya Wazazi baada ya kujitambua Mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chap- ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu”

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni Wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato Kijijini hapo na wameachisha Watoto wao Shule ili wajiandae kumpokea Yesu ambapo hadi sasa Watoto 13 tayari wameacha kwenda Shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na Elimu Dunia inayotolewa na Shule za Serikali na binafsi.

DC Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na Mwinjilisti mwenzake anayemsaidia kazi za Kanisa Anthony Mkomela kwa mahojiano zaidi.

Pia soma

 
Huyu msabato wa wapi? Maana kanisa lineandikwa Country living hii itakuwa ni tafsiri yake katika maandiko sababu kanisa la Waadventista wasabato huwa linaongozwa na mchungaji katika mtaa husika, wainjilisti huwa wanapelekwa kusambaza injili lakini sio kuanzisha kanisa ili kanisa lianzishwe lazima liwe na baraka ya uongozi wa juu wa kanisa, na lazima lipewe mchungaji

Pichani ni mfumo wa kanisa kuanzia juu mpaka chini
 

Attachments

  • 40-Figure1-1.png
    40-Figure1-1.png
    8 KB · Views: 11
Back
Top Bottom