Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 3,520
- 6,503
Huenda wakati mwingine kama wazazi huwa tunapenda wenetu wasome katika shule zenye majina makubwa au zile ambazo ni maarufu hapa jijini dar es salaam, lakini kiukweli maumivu ya usafiri wa daladala wanapata watoto wetu.
Huwa wananyanyaswa Sana na makondakta, huzuiwa kupanda Magari,kama tunavyojua sio makonda wote ni wenye kujali, wengi wao hawana huruma Kwa hawa malaika wa Mungu, inafika kipindi watoto wanalazimisha kupanda hivyo hivyo na kuhatarisha usalama wao.
Jana nikiwa posta mida ya saa kumi na moja jioni, watoto wakiwa wanapanda magari ya kwenda gongo la mboto, niliona watoto wadogo wakilazimisha kupanda daladala huku likiwa linaondoka na kuhatarisha usalama wao, huwezi ukawalaumu hawa watoto kwakuwa wamechoka na wanataka kwenda nyumbani kupumzika.
Kutokana na changamoto wanazo kutana nazo kila siku imewafanya wawe ngangali kama watu wazima vile, unakuta vitoto vya darasa la kwanza au la pili vinakomaa na watu wazima kupanda katika daladala na wakati huo huo wanapambana na roho mbaya za makondakta wasio na huruma.
Utavikuta maskini vinakimbilia basi hili mara lile na kote huko saa nyingine vinakataliwa, utaviona vinyonge na vyenye kukata tamaa.
Wazazi, serikali ilipoamua kujenga shule za kata lengo lilikuwa kuwapunguzia watoto adha ya kwenda kusoma mbali na kuleta ahueni katika harakati nzima za kutafuta elimu yao , walau basi wangekuwa watoto wa sekondari sio mbaya kwanza ni wakubwa na wanajielewa, lakini hawa wa msingi ni mtihani sana kwao.
Ebu tuwaonee huruma hawa wenetu kwa kuwatafutia shule za karibu ili kuwapunguzia adha ya usafiri ukichukulia wengi wetu hatuna uwezo wa kulipia mabasi maalumu ya wanafunzi.
Mbona wengi wetu huko miaka ya nyuma tulisoma shule za kawaida tu na tulimaliza shule za msingi na kuendelea na elimu ya sekondari bila shida yoyote?
Ukitaka uyaamini haya ninayosema kwa wewe mzazi ambaye hujapata ona adha ya usafiri ambayo wanapata wenetu ebu siku moja nenda kituo cha daladala uone Show yake, ndo utajua purukushani ambazo wanakutana nazo watoto wetu.
Ngoja niishie hapa naona kama kalamu yangu inaisha wino na bahati mbaya usiku huu maduka mengi yamefungwa hivyo si rahisi kupata peni nyingine.
Ni hayo tu!