Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Shida ni approach yake. Hauwezi kupitisha jambo na kulibariki bungeni ukatoka nje kulikosoa, haiendi namna hiyo.
Tatizo alilitengeneza yeye kwa mihemuko ya 2025, ndungai mwenye Joho sio ndungai mwenye Suti kabla ya kupata Ndungai mwenye kitenge
 
huu muda unaopoteza kumtetea ndugai Bora ungeenda kwenye mizimu yako kumuombea mbowe
 
Nadhani ndugai hapingwi kama mtanzania wa kawaida anae toa maoni yake no. Ndugai Hana uwezo wakuutenganisha u speaker na yy binafsi hata akiwa nje ya bunge.... Anachopingwa ni kwamba yy ndo mkuu wa mhimili wa bunge alikuwa na kila sababu au Nguvu kushika shilling bunge I na kuwabana mawaziri na serikali, Maan yy ndie anaendesha mijadala yte na ndo boss wa mhimili... Watu wanaona Ndugai kama speaker ndie katufikisha huku, Leo anakuja kuyaongelea nje eti kama mwananchi wa kawaida ili hali alitakiwa kulinusuru taifa akiwa kama boss wa mhimili wa bunge
 
Kwa mujib wa huu mjadala, spika alihoji kuhusu mikopo, kitu ambacho kinaweza kujadiliwa bungeni wakati wa budget. Sasa kama huko wanapitisha na hasemi chochote, iweje huku nje aseme kwamva anashangazwa na mikopo inavyoongeze

Kwa mujib wa huu mjadala, spika alihoji kuhusu mikopo, kitu ambacho kinaweza kujadiliwa bungeni wakati wa budget. Sasa kama huko wanapitisha na hasemi chochote, iweje huku nje aseme kwamva anashangazwa na mikopo inavyoongezeka?
Kwa

Hili la mkopo nafuu wa Covid 19 lilipitishwa bungeni kweli!!???
 
Wewe kiazi una akili? Magufuli miaka mitano ametekeleza miradi mingapi mikubwa? Miradi mikakati ambayo itakuwa na impact kubwa kwa taifa letu?
Ametekeleza miradi gani? Ya Kukata miti ya Selous na kujenga bwawa? Uharibifu mtupu!!

Ya kuelekeza SGR Rwanda ambako kuna mizigo michache kuliko DRC au Zambia!!

Mwehu anajenga international airport Kijijini kwake, matumizi mabaya ya fedha za umma. Muache aendelee kuoza jehanam
 
Kwa

Hili la mkopo nafuu wa Covid 19 lilipitishwa bungeni kweli!!???

Sasa si ndio alitakiwa alihoji akiwa bungeni? Si wanakaa mwezi huu?

Na huko awali si tuliambiwa manunuzi ya ndege na mambo mengine yalikua yakifanyika bila kupata baraka za bunge? Mbona hakuwahi kusema kitu hadharani?

Hata pale walipoitwa ni bunge dhaifu, wakaishia kumuita Baba wa watu kwenye kamati ya maadili.
 
Mwendawazimu tu ndio atamuunga mkono Ndugai, kwanza anasema hiyo hoja ni ya kutunga. Pili ameomba msamaha kwa hoja hiyo. Kama yeye binafsi anakataa hoja yake, kwanini sisi tujipe jukumu la kuitetea hoja yake? Akitaka hoja yake ibaki na nguvu ashikilie msimamo wako.
AMEN
 
Mimi binafsi nipo na Ndugai.
Wapinzani tutakosea sana tukiwa upande wa Samia kisa Ndugai ni mtu tusiyempenda, Hoja ya Ndugai ni moja kati ya sera zetu "kupunguza mikopo na kutumia rasilimali zetu na uwekezaj"
Ndugai hatumpendi lakini upepo wa wananchi wajinga wa Tanzania upo na Ndugai maana wanaamini Magufuli alikuwa jembe hakopi nje.
Kwa hoja ambayo keshaikana? Hebu jitafakari kidogo, inavyoonekana ni kuwa aliyoyasema na anayoyasema sasa yote hayakutokea moyoni mwake.
 
Lakini mtu yeyote aliyemsikiliza Ndugsi vizuri hawezimlsumu maana alihoji nafasi za tozo na mikopo maana hata rais nae alisema tutoe tozo ili mieadi iendelee
 
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Point ya kwanza ni utumbo"pumba"
Hoja ya msingi ambayo haijajibiwa
Tozo ni Kodi juu ya Kodi
Na sababu ya kuipitisha bungeni ni kwamba isadie tuweze kufanya mambo binafsi Kam nchi bila misaada au mikopo..
Sasa Kama Kuna tozo kwa nini tukope mikopo ambayo haizalishi..
Yan unakopa kupambana na covid 19 alaf unajenga madarasa na vyoo.
Wakati huo huo unawasomi lukuki hawana ajira
Bora hata hiyo mikopo ya kibishara inchi inakuwa huru kuamua inawekeza Ela yake wapi ili irudi pia inufaishe watu wote.
2025 itaongea tu!!
 
Magufuli alipokopa Tsh 29 Trillion kwa miaka 5 aliona sawa tu??? Samia kakopa Tsh 1.3 Trillion ndiyo Ndugai anatumia haki yake kikatiba!!

Halafu mbona mwenyewe kaomba msamaha? Sasa aliposema nimekosa Mimi, nimekosa mimi alimaamisha nini?
Brother naomba nikukumbushe kuwa Watanzania hawataki kusikia ukweli akiwemo JPM. Ndiyo maana alipousema ukweli Wana ccm wakapandisha mori na kuanza kumshambulia kwa kumkosoa. Kukosolewa ni kitu ambacho ni very minor sana.

Kutokulisemea suala la JPM kukopa Trillioni 29 kwa miaka 5 ni uoga tu ulimjaa na akashindwa kutumia mamlaka na haki aliyonayo kikatiba katikz kuushauri na kutoa maoni kuhusu mikopo hiyo.

Ila kuhusu mkopo wa sasa, Ayubu aliamua kutumia haki yake ya kikatiba ipasavyo na ndiyo maana aliamua kuusema ukweli uliomchungu ambao Watanzania wengi hatupendi kusikia ukweli huo.

Ayubu baada ya kuusema ukweli hakutakiwa kurudi kwenye vyombo vya habari na kuanza kuomba msamaha wakati hakuna kosa alilotenda kwa mujibu wa sheria zetu za nchi.

Lakini kusema amekosea na hakuna kosa lolote alilofanya kisheria hakumfanyi awe mwenye hatia brother so long as alikuwa anatumia haki yake ya kikatiba.

Ayubu alitakiwa kuonesha msimamo wake kwamba alichokiongea yupo sahihi bila kuonesha uoga wowote.

Kadhalika, Ayubu amekosa mshauri mzuri kuhusu hili saga lililokuwepo mezani. Hakika angeibuka mashindi juu ya hili jambo.
 
Kweli Tanzania imejaa majitu bogus kama joshydama. Yaani unamtetea huyu Spika wa hivyo ambaye Nchi yetu haijawahi kuwa naye kabla yake!

Unamtetea Spika aliyeapisha wanawake 19 na kuwaita wabunge na wanakula mabilioni ya Kodi zetu. Unamtetea Ndugai aliyekataa kushirikiana na CAG kutafuta zilipo Tsh 2.4 Trillion.

Kweli watu wengine vichwa vyenu ni mfuko wa kubebea meno tu
 
Hatetewi Ndugai kama Ndugai!

Inatetewa hoja yake!

Na hata hivyo pamoja na Hanganya kulishambulia bunge kupitia Ndugai, bado hoja ya Ndugai itamtesa hadi anafika 2025
 
Back
Top Bottom