Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

IMG_20220105_212055_611.jpg

IMG_20220105_212055_689.jpg
 
Mwendawazimu tu ndio atamuunga mkono Ndugai, kwanza anasema hiyo hoja ni ya kutunga. Pili ameomba msamaha kwa hoja hiyo. Kama yeye binafsi anakataa hoja yake, kwanini sisi tujipe jukumu la kuitetea hoja yake? Akitaka hoja yake ibaki na nguvu ashikilie msimamo wako.
 
Kuomba msamaha kwake hakuondoi hoja aliyoiweka mezani
 
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Akafie mbele huko, hoja zake zitajibiwa wakisharudi kutoka kibla
 
Unataka ajibiwe Nini wewe ,hii nchi ni maskini Tena maskini kweli kweli .....

imekuwa ikikopa Toka inapata uhuru ,na hakuna mwaka umeisha bila kukopa ,huyo ndugai analijua Hilo ....

Kitendo cha kusimama na kulopoka ujinga ule ni dharau kabisa ....Sasa unataka ajibiwe Nini hasa ....kwamba hii nchi inaweza kujiendesha kwa tozo ? ....

Mambo mengine ni ujinga mtupu ..

Mama kashasema hii nchi lazima ikope ,ni maskini ..

Tanzania ni masikini ,lazima ikope
 
Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."
Mkuu Yericko, kwa hiyo unaamini kuwa tuna bunge lililopatikana kwa kufuata taratibu na mchakato wa kikatiba ?
 
Mimi binafsi nipo na Ndugai.
Wapinzani tutakosea sana tukiwa upande wa Samia kisa Ndugai ni mtu tusiyempenda, Hoja ya Ndugai ni moja kati ya sera zetu "kupunguza mikopo na kutumia rasilimali zetu na uwekezaji"
Ndugai hatumpendi lakini upepo wa wananchi wajinga wa Tanzania upo na Ndugai maana wanaamini Magufuli alikuwa jembe hakopi nje.
 
Tatizo ni hata wewe kuona kwamba ile Hoja ni ya Ndugai na sio Hoja /Swali / Issue sio tu inayotakiwa kujibiwa bali majibu yake yawe wazi kwa kila mwenye macho au Mtanzania apate kujua na sio kuambulia kejeli...

Sisi watanzania ni watu wa matukio na kuangalia nani kasema na sio nini kimesemwa ndio maana always tunajikita kwenye personalities na sio issues....

Thus tupende kuangalia nini kimesemwa na sio nani kasema...., na kila kilichosemwa hata kama ni upuuzi kipatiwe majibu na sio kejeli ili kuwekana sawa, hii nchi yetu sote na kama ilivyo kukopa harusi kulipa matanga hata ambao hawakuwepo kwenye hizo harusi kwenye matanga watajumuika watake wasitake....
 
Kuomba msamaha kwake hakuondoi hoja aliyoiweka mezani
Ndugai hana hoja.Ndugai hana hoja. Siyo kweli unachosema. Bunge ndiyo hupitisha bajeti ya recurrent and development. Wanaposema makusanyo yatakuwa Tsh 24 T rillion huku Bajeti ya mwaka ni Tsh 32 Trillion unadhani hiyo nakisi inatoka wapi? Nakisi hujazwa kwa grants, donations and loans. Ndugai hajitambui, he is lunatic and unfit to the position
 
Back
Top Bottom