Jakaya Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere - Sehemu ya sita (6)

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
332
KIFO CHA AKUKWETI,MIKAKATI YA LOWASSA,KARATA YA KIKWETE NA UTEUZI WA MEMBE.

Habari za siku wasomaji wangu mnaofuatilia "series" yenye "episodes" zinazoelezea historia ya maisha ya kisiasa ya kiongozi nguli nchini Tanzania Bernard Kamilius Membe.

Katika "episode" iliyopita niliahidi kuwaelezea namna ambavyo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa "ofisi nyeti" marehemu Jen.Imrani Kombe na Bernard Kamilius Membe ambaye naye alikuwa mtumishi wa "ofisi nyeti" walivyoelekezwa na Mwl.Julius Kambarage Nyerere kumwajiri Jack Steven Gotham katika utumishi wa "ofisi nyeti".

Lakini kutokana na sababu za kiuandishi wa "series" hii nimeona "episodes" zijazo nitaliandikia suala hili vizuri.

Leo nitazungumzia juu ya kilichotokea katika msiba wa Akukweti,mikakati ya Lowassa,karata ya Kikwete na uteuzi wa Membe.

Naomba muungane nami katika "episode" hii.

Juma Jamaldin Akukweti alikuwa mbunge wa Tunduru tangu mwaka 1990 kupitia Chama Cha Mapinduzi.Alifariki mwaka 2007 mwezi January,tarehe 4.Alifariki akiwa Waziri anayeshughulikia masuala ya Bunge.Kifo chake kilitokana na majeraha ya ajali ya ndege iliyotokea mkoani Mbeya.

Mzee Akukweti alikuwa ni mmoja wa wanasiasa waliokuwa karibu sana na Mzee Kikwete,Edward Lowassa na Bernard Membe.Lakini pia alikuwa ni mmoja wa wanasiasa watokao mikoa ya Kusini kama alivyo Bernard Kamilius Membe na alivyokuwa marehemu Sigfrid Ng'itu wa jimbo la Ruangwa.

Wakati Mzee Akukweti anafariki Bernard Membe alikuwa Naibu Waziri wa nishati na madini chini ya Naziri Mustafa Karamagi.Naye Edward Lowassa ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu kwa wakati ule.

Kama ilivyo kawaida kiongozi mkubwa wa kiserikali anapofariki wenzake hushiriki msiba na hata kusafiri kwenda katika mazishi yake ili kushirikiana na familia.Ndivyo ilivyotokea pia katika msiba wa Mzee Akukweti.

Hapa kuna jambo moja kubwa la kukumbukwa.Wakati msiba wa Mzee Akukweti unatokea siku ya mazishi yake Tanzania ilipata pia bahati ya mmoja wa mawaziri wa wakati huo kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa.Huyu alikuwa Mama Asha-Rose Migiro ambaye kabla ya huo uteuzi alikuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.Na huu ndio msingi mkuu wa "episode" hii leo kwani ina simulizi ambayo sio kila mmoja anaijua.

Baada ya familia ya Mzee Akukweti kushauriana na kukubaliana na serikali kuwa mzee wao atazikwa kijijini kwao Tunduru mkoani Ruvuma ilibidi mawaziri,manaibu waziri,wabunge na baadhi ya viongozi wa chama kusafiri hadi Tunduru ili kushiriki mazishi.

Serikali ilitoa ndege ambapo moja ilimbeba Waziri Mkuu na baadhi ya mawaziri na manaibu waziri na ndege nyingine ilimbeba Rais pamoja na baadhi ya mawaziri na manaibu waziri.Wabunge na baadhi ya viongozi wa chama nao walifanyiwa utaratibu wa usafiri wao na walioamua kutumia usafiri binafsi walifanya hivyo pia.

Bernard Membe ni kati ya viongozi wa serikali waliopangiwa kusafiri na ndege iliyombeba Waziri Mkuu.Akiwa VIP Lounge(JKNIA) kusubiri itifaki zikamilike akajulishwa kwamba Waziri Mkuu kasema ndege yake haina nafasi kwa ajili yake.Hivyo atafute usafiri mwingine.Alipohoji kwanini inakuwa hivyo wakati inajulikana fika yeye ni mmoja wa wasafiri katika ndege hiyo alijibiwa kuwa hayo ni maelekezo kutoka kwa Waziri Mkuu.Baada ya majibu hayo Bernard Membe aliamua kumpigia simu dereva wake na kumjulisha kuwa amfuate ili Airport ili wasafiri kwa gari kuelekea Tunduru katika mazishi ya Mzee Akukweti maana ndege imejaa.

Akiwa bado VIP Lounge akimsubiri dereva wake afike ndipo msafara wa Rais Kikwete ukafika.Rais Kikwete alipoingia VIP Lounge alimkuta Bernard Membe na kumhoji mbona hajasafiri ndipo alipomjibu kuwa ndege aliyopaswa kuondoka nayo ameambiwa imejaa.Rais Kikwete akamwambia kuwa katika ndege yake kuna nafasi hivyo waondoke pamoja.Ikambidi Bernard Membe amsitishe dereva wake kwenda Airport na badala yake akamwambia watakutana Tunduru ili baada ya mazishi waende katika ziara ya kikazi aliyopaswa kuifanya mkoani Shinyanga katika mgodi wa Wiliamson.

Safari ya kuelekea Tunduru ikafanyika.Lakini kama mjuavyo Bernard Membe ni Kachero aliyebobea ikampasa kuchunguza kama ni ukweli ile ndege aliyoondoka nayo Waziri Mkuu ilikuwa imejaa au la!?Taarifa za uhakika zikamthibitishia kuwa ndege haikujaa na nafasi yake ilikuwepo ila tu Waziri Mkuu hakutaka kuona uwepo wake."Episodes" zijazo nitaelezea kwanini Edward Lowassa na Bernard Membe walitofautiana baada tu ya serikali ya awamu ya nne kushika hatamu.

Msafara ule ulifika salama Tunduru na kushiriki mazishi ya Mzee Akukweti salama.Na ndio wakati ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipokea taarifa ya uteuzi wa Mama Migiro.Rais Kikwete kwa kutambua kuwa karibia nusu ya serikali yake ipo naye Tunduru akaamua kuwaita viongozi wote waliokuwepo Tunduru(mawaziri na manaibu mawaziri)na kuwajulisha juu ya uteuzi wa Mama Migiro.Kisha akamwambia Waziri Mkuu wake kuwa kesho yake wakutane Dar es salaam(Ikulu)saa nne asubuhi ili wajadiliane juu ya uteuzi wa waziri mpya wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.Akamwambia watakuwa pamoja na Makamu wa Rais.Wakati huo ni Mzee Mohamed Shein.

Baada ya mazishi ya Mzee Akukweti na kupokea taarifa ya uteuzi wa Mama Migiro,Bernard Membe aliaga kisha kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.Wala hakujua ni nani atateuliwa.Na wala hakuhisi kama uteuzi ule ungemhusu yeye.Na hii ni kwasababu tayari kulikuwa na "beef" baina yake na Waziri Mkuu hivyo mashauriano yoyote juu ya uteuzi wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa basi Waziri Mkuu asingeweza kupendekeza jina lake au hata kuunga mkono pendekezo la Rais kama lingemhusu yeye.

Hapa ndipo mikakati ya Edward Lowassa ilipoanza kutekelezwa.Kwakuwa hawakulala Tunduru baada ya mazishi,walipofika tu Dar es salaam kulifanyika kikao baina ya Lowassa na Rostam Aziz.Kikao kilikuwa juu ya majina ambayo waliona yanafaa kumrithi Mama Migiro.Na hii yote ilikuwa ni katika mipango ya 2010.Msisahau mpango wao wa OP yaani ONE TERM PRESIDENT waliousuka ili Rais Kikwete aongoze kwa muhula mmoja tu yaani 2005-2010 kisha Edward Lowassa achukue kuanzia 2010-2020.Mkakati ambao Rostam Aziz katika moja ya mahojiano yake na gazeti la Mwananchi na Mwananchi Digital mwaka huu(2019)anakiri ni Bernard Membe ndiye aliyeuzuia na alitoa sababu za kuuzuia na wao wakakwama.

Tuendelee..

Katika kikao chao Edward Lowassa na Rostam Aziz walipendekeza majina ya Balozi Dk.Batilda Burhan na Mzee Abdulrahman Kinana.Na walikuwa na sababu zao mahsusi juu ya mapendekezo haya.Tutaanza na sababu za wao kumpendekeza Balozi Dk.Batilda Burhan,walisema ni mwanamke alafu muislamu.Hivyobasi kwa mpango wao wa 2010 asingeweza kuchukua fomu na kuwania urais kwasababu kwa wakati ule bado Tanzania ilihitaji kuwa na kiongozi mwanaume kwahiyo kwa mwanamke kupatiwa ofisi kubwa kama Ikulu isingewezekana na pia wajumbe wa Nec na Mkutano Mkuu wasingeweza kumchagua.Sababu yao nyingine ilikuwa ni dini.Waliamini kuwa kama utamaduni ulivyo basi isingekuwa rahisi kwa muislamu kutoka kisha muislamu mwingine kuingia.Kwahiyo hili pekee lilitosha kuwafanya waratibu mipango yao vizuri bila kujulikana.

Kwa Mzee Kinana napo walikuwa wajanja sana.Wakawa na sababu mbili kama ilivyokuwa kwa Balozi Dk.Batilda Burhan.Kwanza walikuwa na hoja ya uraia wake.Wakajua fika ikitokea anachukua fomu 2010 basi hatofika mbali kwa maana ya kwamba tayari alikuwa na doa la uraia wake.Kwamba watafufua hoja ya "usomali" iliyowahi kumsumbua huko nyuma alipokuwa Mbunge na Waziri.Lakini pia sababu yao ya pili ni dini.Kwahiyo hapa walijua lazima wangemzuia.

Lakini kubwa zaidi walijua fika njia nyingine nzuri ya kuwamudu Dk.Batilda Burhan na Mzee Kinana ni kuwajulisha kabla(usiku ule ule)kuwa majina yao yanapendekezwa kwa Rais Kikwete ili wamrithi Mama Migiro.Na kwamba wao(Lowassa na Rostam)ndio Kingmakers wakuu wa suala lile.Kwa wasiojua huu ndio ulikuwa mtindo wa Lowassa na Rostam kwa wateule wengi wa Rais Kikwete kuwahadaa kwamba wao ndio waliokuwa wakiwapigania katika teuzi wanazopata kwahiyo wasiwaangushe katika matakwa yao.Na wengi walioteuliwa waliamini hivyo na bila kujua wakajikuta wapo loyal sana kwa Lowassa na Rostam kumbe haikuwa ukweli.Wajanja walijua na wakapuuzia uzushi huu na kuna wakati Rais Kikwete alijua akawa hamshirikishi Lowassa katika teuzi anazofanya ili kuzuia taarifa kuvuja.

Kweli baada ya kikao cha Lowassa na Rostam kumalizika kesho yake saa moja asubuhi Lowassa aliwahi Ikulu akiwa na mapendekezo yake.Nia ya kuwahi ilikuwa kufunga maneno na Rais Kikwete kabla ya Makamu wa Rais kujua.Rais Kikwete hakuweza kuonana na Lowassa kwa muda ule kwahiyo wasaidizi wake(Rais Kikwete)wakamjulisha Lowassa kuwa muda wa kikao chao ni uleule uliopangwa wakiwa Tunduru katika mazishi na haujabadilika kwahiyo ni vyema akarudi muda uliopangwa maana kwa wakati ule Rais alikuwa na ratiba nyingine.

Rais Kikwete alikuwa "smart" kuliko Waziri Mkuu wake katika hili.Inasemekana muda ule Lowassa kaenda Ikulu kuonana naye kumbe yeye alikuwa na kikao kizito na Makamu wa Rais juu ya uteuzi wa mrithi wa Mama Migiro.Na jina alilokuwa nalo ni la Bernard Membe.Lowassa hakuliwaza kabisa.Na hakutegemea kama Membe angekuwa ni chaguo la Rais Kikwete.

Lowassa aliondoka Ikulu na kuahidi kurudi tena baadaye wakati wa muda wa kikao kama walivyokubaliana jana yake wakiwa katika mazishi Tunduru.Kweli muda ulipowadia Lowassa alirejea Ikulu na kukaa kikao na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dk.Shein.Lowassa alitoa mapendekezo yake na sababu zake(sio zile za kimkakati kuelekea 2010).Kuhusu Dk.Batilda Burhan alitoa sababu kwamba kwanza ni mwanamke na ingekuwa vyema akamrithi mwanamke mwenzake yaani Mama Migiro lakini pia ana elimu nzuri na uzoefu wa kutosha serikalini na katika chama.

Kuhusu Mzee Kinana alitoa sababu kwamba ni kada mzoefu wa chama,amewahi kuwa waziri na mbunge wa jimbo,amewahi kuwa mbunge wa EALA na Spika wa EALA.Ana uzoefu wa nafasi ya juu jeshini.Hivi vyote vinatosha kumteua kurithi mikoba ya Mama Migiro na kama suala ni ubunge basi ateuliwe ubunge na kupatiwa uwaziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Rais Kikwete na Makamu wake Dk.Shein walipingana na mapendekezo yale.Sio kwasababu hawakufaa la hasha bali tayari Rais Kikwete alikuwa na sababu muhimu za kumteua Bernard Membe kutokana na uzoefu wake serikalini,kwenye chama na siasa kwa ujumla kama mbunge wa jimbo.Na kwa wakati ule katika serikali yake ni Bernard Membe ndiye aliyekuwa na elimu kuhusu masuala ya diplomasia ya uchumi na alikuwa na uzoefu wa utendaji katika nyanja za diplomasia tangu akiwa katika "ofisi nyeti",wizara ya mambo ya nje pia ubalozini nchini Canada.

Huku akiwa hajui kinachoendelea Dar es salaam Dk.Batilda Burhan alimpigia simu Bernard Membe na kumpongeza juu ya uteuzi aliopata.Lowassa aliwajulisha wenzake kuwa mpango wao umefeli kwani Rais Kikwete kaamua kumteua Bernard Membe kama mrithi wa Mama Migiro.Kwake lilikuwa ni pigo kubwa sana.Hakutaka historia ya nchi kuwa na Rais mwenye uzoefu wa wizara ya mambo ya nje ijrudie baada ya Rais Kikwete.Ndio maana majina ya Mzee Kinana na Dk.Batilda Burhan yalikuwa ni sehemu ya mkakati wake.

Baadaye Rais Kikwete kupitia Katibu Mkuu wake Kiongozi Mzee Luhanjo alimtangaza Bernard Membe kama waziri wake mpya wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Naye Bernard Membe alijulishwa kuwa anapaswa kurudi haraka Dar es salaam ili aapishwe kwani siku inayofuata inabidi asafiri nje ya nchi kikazi na Rais Kikwete katika mkutano AU.Bernard Membe alirejea Dar es salaam siku hiyohiyo baada ya kutangazwa kuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na siku hiyohiyo aliapishwa kisha kesho yake wakasafiri katika mkutano AU.

Hata AU hawakujua kama Rais Kikwete anaenda na waziri mpya wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.Aliwashtukiza katika mkutano.

Hivi ndivyo uteuzi wa Membe ulivyotokea.Hivi ndivyo mikakati ya Lowassa ilivyofeli.Hivi ndivyo Kikwete alivyozichanga karata zake.

Je wajua namna Membe alivyotumia Ujasusi kuikwepa RICHMOND!?

Tukutane kesho muda kama huu......
=====
1. Mzee Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere
2. Rais Kikwete alimtuma Membe kwa Mwalimu Nyerere, Sehemu ya Pili (2)
3. Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl. Nyerere, Sehemu ya tatu (3)
4. Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere, Sehemu ya nne (4)
5. Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere, Sehemu ya tano 5
 
Hii inaitwa ni delusion, delusion ni ugonjwa wa akili ambapo mgonjwa huamini mambo ambayo kiuhalisia hayapo, mfano anaweza kuwa anaamini kabisa kichwani kwake kwamba yeye ni muhimu na nchi nzima inamuona hivyo, wakati siyo kweli.
 
Unataka tuamini kwamba Membe hakuwa mrithi wa Migiro ?
 
Kweli siasa ngumu sana, wanavyocheka na kupongezana mbele ya camera, kumbe nyuma ya pazia na mioyoni mwao kumejaa vitaaa.
 
Mkuu samahani naomba ukipost inayofuata unitagi pia naomba kama hautajali nisaidie namna ya kupata episoda 1-5 maana nimepata hiyo 6 tu.

Natanguliza shukurani 🤲
 
Andika kitabu, kitakuingizia hela kuliko hizi episode. Hizi ni utangulizi tosha. Hingera kwa kuyajua yote hayo.
 
Pitieni hapa.....
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom