Msiba wa Daudi Mwamgosi: Kinachojili Itete, Tukuyu katika mazishi yake

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
======================

Tokana na wingi wa picha Update zote zimewekwa mwanzo wa habari ili kuhakikisha ujumbe unasomeka kwa wote
wenye niya ya kutambua nini kinaendelea katika msiba wa Marehemu D. Mwambosi

========================

Wakiongea kwenye mazishi ya mwandishi wa habari aliyeuwawa na polisi.kwa nyakati tofauti Mbunge wa Rungwe Profesa MARK MWANDOSYA na Katibu mkuu wa Chadema Dk W.P.SLAA wameahidi kuwasomesha watoto wa marehemu Daud Mwangosi.

Akianza Prof Mark Mwandosya amesema anajitolea kumsomesha mtoto wa kwanza alie kidato cha nne mpaka chuo kikuu.

Naye katibu mkuu wa Chadema amesema kwa kuanzia wameshatoa kiasi cha fedha na vile vile wameahidi kumsomesha mtoto wa pili ambaye sasa yuko darasa la saba.

Source.Eborn Fm


IMG-20120904-WA009.jpg


Wawakilishi Mbalimbali wakitoa salam za Pole kwa ndugu wa Marehemu


Mwakilishi wa Chanel Ten Hamis akitoa pole katika msiba huu muda huu






Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akitoa pole zake kwa wafiwa


Mwanaharakati Francis Godwin akielezea Jinsi Mauti yalivyo mkuta Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi






Rais wa UTPC Kenny Simbaya ambaye pia ni kiongozi wa msafala wa kuleta Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi akiwa anatoa salam za Pole kwa wafiwa.


Dr Slaa akitoa pole kwa wafiwa wote Muda huu










Wakina mama wakiwa wenye majonzi makubwa sana na huzuni muda huu

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu

Maelfu ya watu wakiongezeka kuja katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi Muda huu

Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali

Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu

Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliye jishika, akiwa na uchungu muda huu




Ibada ikiwa inakaribia kuanza

Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa

Waandishi wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .


Endelea kufuatilia Moja kwa moja hapa


PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

Updates; Forever Bold, RIP D. M, Tuonane Mtoni Mkuu!!



Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makabirini

Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko

Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele

Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa Tayari katika Kaburi

Shughuri za kuzika zimeanza

Mazishi yanaendelea

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu

Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe

Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa

Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa

Dr Slaa akiweka Shada la Mauwa

Dr Slaa Baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho

Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake

Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua

Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua


Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katiaka Kaburi

Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi

Waandishi wa Habari wakichukua Tukio Live `

Na huu Ndio Mwisho wa tukio zima la Mazishi ya Ndugu yetu, Mwanaharakati, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.


 
ni kweli pr mwandosya kajitolea kusomesha familia?
 
Inanitoa machozi mwanaume mzima mimi! Nani atasimamia mke na watoto wa marehemu kufikia malengo ambayo baba yao alikua anawapigania wayafikie? Huu ni udhalimu usiovumilika hata kidogo,wamemuua Daud kwa kosa gani kubwa alilofanya? au kosa lake ni kuzaliwa Mtanzania na kupigania ukweli?

Head of the state yuko wapi huku watu na maswaiba wake wanatumaliza Watanzania yeye amekaa kimya akitabasamu tu?wananchi kulalamika haitatusaidia,shime tuungane kuondoa udhalimu huu,wanaharakati,viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa tunasubiri matamko yenu haraka iwezekanavyo!

Leo kwa familia ya Daud kesho kwa familia ya mmoja wetu,Watanzania hatupo salama tena ndani ya nchi yetu wenyewe,na walioamua kutuua ni watu tuliowachagua kutuongoza! Eeh Mungu wasimamie na uwaangazie mwanga wenye matumaini watoto wa Daud Mwangosi, R.I.P soldier
 
Tangulia Mwangosi Mungu akunyoshee mapito yako umekufa ukitetea haki ya mwananchi kupata habari na kukataa udhalili wa kunyanyasa wanahabari ukienda huko waambie waliotangulie watoe laana zao kwa KIkwete Mwema na Kamhanda
 
Nimepata taarifa kuwa Mhe. Mwandosya amejtolea kuwasomesha watoto wa marehemu.
Mwandosya mnafiki mkubwa itasaidia nini wakati watoto kinda kabisa hakukuwa na sababu ya baba yao kunyang'anywa uhai wake,watoto wanamuhitaji baba yao
 
pole sawa wanafamilia na wanahabari
wamesemaje hao waliozungumza kumsaidia mjane na kusomesha hao watoto aliowaacha?
 
cku yaja. Maadam hawa police na viongozi wao tunao huku mtaani itajulikana cku hiyo. R.I.P daudi
 
Ahsante Mkuu kwa kutuletea matukio haya kwenye picha RIP mpambanaji mwenzetu Mwangosi, inasikitisha saana!!!

 
Back
Top Bottom