SoC01 Tuanzishe Benki ya vijana kupunguza tatizo la ajira kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 15, 2021
15
45
Ajira kwa vijana Tanzania imekuwa changamoto endelevu inayohitaji mbinu mbalimbali za utatuaji. Jitihada kutoka kwa serikali na sekta binafsi zinahitajika ili kuweza kutatua changamoto hii ya arija kwa vijana. Mara nyingi wataalamu mbalimbali wametoa angalizo juu ya ongezoko la vijana wasio na ajira na tatizo hili kuonekana kama ni bomu la masaa linalosubiri kulipuka tu.

Idadi ya vijana nchini Tanzania inaongezeka kwa kasi kama inavyoonyeshwa na takwimu za Umoja wa Mataifa za mwaka 2020 ya kuwa vijana walio chini ya miaka 24 wako asilimia 64 na wale wenye umri wa miaka 15-34 wako asilimia 34. Takwimu hizo zinaenda mbali na kufafanua ya kuwa, vijana wa umri wa kati ya miaka 15-35 wasio na ajira ni asilimia 3.6.

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana walio na elimu na wasio na elimu ni kubwa kwa pande zote na jitihada mbalimbali zinahitajika kuweza kutafuta suluhisho la kudumu. Natambua fika kumekuwa na mikakati mingi iliyowekwa na serikali pamoja na sekta binafsi kupunguza tatizo hili nami ningependa kujenga hoja mbadala itakayoweza kusukuma jitihada zingine zilizopo.

Changamoto nyingi zinazowakumba vijana ni pamoja na ujuzi na mitaji. Kutokana na hili, vijana wamekuwa wakihimizwa kujiajiri bila kuona wapi watafanikiwa kupata ujuzi, mitaji na mafunzo stahiki yatakayoweza kukuza mawazo yao. Kumekuwepo na vyombo mbalimbali vya kuwasaidia vijana kunoa vipaji na kuwapatia ujuzi mbalimbali ila bado mitaji inaendelea kuwa changamoto.

Kuanzishwa kwa benki ya vijana kutakuwa sehemu ya suluhisho la ajira kwa vijana kwa kuwapatia mitaji itakayoweza kuwasaidia kuanzisha biashara ama kuendeleza mawazo yao ya ubunifu. Benki hii ya vijana italenga kuwasaidia vijana wasio na mtaji, wenye mitaji wa kati na wale vijana wenye mitaji mikubwa. Benki hii inapaswa kuwa mali ya vijana itakayoendeshwa na kuratibiwa na vijana wanaojua changamoto mbalimbali zinazowapata vijana wetu.

Wazo hili za uanzishwaji wa benki ya vijana, linapaswa kuwashirikisha vijana wenyewe kuona uhalali wake, kupata maoni ya namna bora ya kuiendesha benki hii pamoja na kuona taratibu imara zitakazoweka vigezo vya wakopaji na mengine mengi. Mwaka 2007 Benki ya Wanawake ilianzishwa kwa madhumuni kama haya na mpaka sasa benki hiyo inaendelea ikikadiriwa kuwa na mtaji wa thamani ya bilioni 8.5.

Je, tunaweza kujifunza kutoka kwenye uendeshwaji wa Benki ya Wanawake na kuona ni kwa namna gani benki ya vijana inaweza kuwa bora zaidi?

Tukumbuke kuwa, asilimia 64 ya watu nchini kwetu ni vijana ambayo ni zaidi ya nusu ya watu wote. Kutokana na wingi huu, ni kweli kuwa benki hii ya vijana itakuwa na mtaji mkubwa sana kama vijana wote tutaona haja ya kuwa na benki hii na kuwekeza pesa zetu humo. Benki hii inaweza kumilikiwa na serikali kwa 50% na 50% zangine zikamilikiwa na vijana kwa kununua hisa ama kwa namna itakayofa.

Manufa ya kuanzisha benki ya vijana ni kutoa fursa kwa vijana wote wenye mawazo ya biashara, sayansi ya ubunifu, kilimo na mengineyo kupata ujuzi kwa kutumia wataalamu watakaowekwa na benki ili kuwafunda vilivyo na kuweza kuwapa mikopo midogo midogo kukuza mawazo yao. Hii ikiwa na maana ya kuwa, vijana watapata fursa kuleta maombi ya bunifu zao za sekta yoyote watakayopenda kisha bunifu hizo zitafundwa vilivyo na zile chache zitakazokidhi vigezo zitapewa mikopo midogo ya kuikuza wakati huo bunifu hizo zikibaki mali ya benki ya vijana mpaka pale zitakaposimama na kuweza kuzalisha faida.

Uwepo wa benki ya vijana itawapatia uhakika vijana kuwa kuna mahali watakwenda na kusikilizwa na kuwachochea zaidi kuja na mawazo yenye ubunifu mwingi shindani. Changamoto iliyopo sasa ni kwamba, vijana wengi wamekuwa na bunifu nzuri sana ila hawana pa kwenda kupata mafunzo zaidi na mitaji. Uwepo wa benki hii utawahakikishia uwepo wa mlezi wa ujuzi na fedha.

Benki ya vijana itaweza kuvutia wawekezaji wenye lengo la kuwasaidia vijana kwa kuweka fedha zao ambazo zinaweza kuzalisha faidia kutokana na mikopo watakayopewa vijana kuzalisha. Kuna taasisi zingi zisizo za serikali zinazofanya kazi kulenga kuwasaidia vijana ambazo huwapatia ujuzi na mitaji midogo midogo ili waweze kuboresha maisha yao, ila miradi mingi inakosa muendelezo hususani pesa zinapoisha kutoka kwa wafadhili. Uwepo wa benki hii ya vijana utasaidia taasisi mbalimbali kuwekeza pesa ambazo zitazunguka kusaidia vijana wengi na hatimaye pesa hiyo kurejea na kusaidia vijana wengine.

Benki ya vijana inapaswa kuwa na riba ndogo kabisa itakayoruhusu vijana kupata mikopo kwa unafuu mwingi na kuweza kurudisha bila maumivu wakati wa kuanzishwa biashara zao. Sambamba na hili, swali linaweza kuwa je, nini itakuwa dhamana ya mikopo ya vijana hawa?

Dhamana inapaswa kuwa miradi anzishwa na vijana, miradi hiyo itakuwa mali ya benki kwa kipindi fulani ambayo itakuwa chini ya uangalizi mpaka pale miradi hiyo itakapokomaa ndio vijana hao wataachiwa huru.

Nadhani kuna haja ya dhati kabisa kutafuta mbinu zote za msingi kutatua changamoto ya mitaji kwa vijana kwani imekuwa pingamizi kwa muda mrefu sasa. Uwepo wa benki ya vijana itakuwa ni chombo mahususi kwa vijana kitakachoweza kutatua changamoto zao. Uanzishwaji wa benki hii haujachelewa, tathimini ya kutosha ifanyike, ushiriki wa vijana katika hili ni muhimu na kuufanya mjadala wa kitaifa utakaotoa mwanga wa namna benki ya vijana itakavyoweza kuanzishwa.

Mwalimu Nyerenyere aliwahi kusema “Uvivu wa kutumia akili unaweza kutufanya tutumie dawa kuondoa matatizo ambayo si ya dawa hata kidogo. Daktari asipojua ugonjwa wangu na sababu zake hawezi kujua dawa yake. Akinipa dawa nikapona, atakuwa kaniponya kwa bahati tu, kwa desturi daktari wa namna hiyo hawezi kumponya mgonjwa, na ni daktari wa hatari sana.” Nukuu hii iko wazi kutukumbusha ya kuwa, matatizo ya vijana ni jukumu letu kutafuta suluhisho kwa kutumia akili zetu ili kupata suluhisho. Je, uanzishwaji wa benki ya vijana Tanzania itakuwa suluhisho kwa ajira? Tutafakiri kutoka hapa.
 
Benki nyingi zilianzishwa na kufa. Benki zilizopo zina uwezo wa kuwakopesha watu kufanya miradi. Wenye uzoefu na uwezo wa kuanzisha miradi ni wastaafu, lakini ndio hupewa mikataba na teuzi pindi wanapo staafu, na kuhimiza vijana wajiajiri. Vijana hawana uzoefu wa kutosha kuanzisha miradi mikubwa hata kama wakikopeshwa. Matokeo wanakwama wakithubutu, na jamii kuwalaumu na kuulaumu mfumo wa elimu kuwa haukuwaanda vijana kujiajiri.
 
Itakuwa benki ya hao hao wa huko juu.

Na vijana hamtakopeshwa mtaambiwa hamna mali isiyohamishika ili muweke dhamana ya mkopo.
 
Wazee wa nchi hii unawajua unawasikia,Wataongeza umri wa Ujana na Kuitela hiyo Bank....Huoni sasa hivi kuna Vijana wa 40+ Unafikiri tulipenda
 
Una wazo,zuri na umefikilia mbali sana LAKINI VIJANA WENYEWE UNAWAJUWA VIZURI KWELI MKUU,

UKIMPA BODABODA TU HLF USIMSIMAMIE MIEZI 3 CKU IKIIONA UTAHIS LABDA IMEBADILISHWA.

Sasa leo umpe 3M hlf hana mali isihamishika, hiyo pesa itarudije mkuu.

Siyo rahic
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom