Mitaji inatukwamisha vijana

iSirius

New Member
Jun 8, 2023
2
2
Mimi ni kajana niliye fanikiwa kusoma na kumaliza Bachelor ya Business Administration.

Tangu kumaliza chuo (2022) hadi leo, nimebahatika kufanya kazi katika kampuni 4 zinazojihusisha na usafirishaji wa mizigo kutoka Nje.

Kutokana na changamoto za kazi, ndo zilinifanya kuhama hama na hatimaye kuacha kazi na kujiajiri baada ya kuona fursa, na kutambua jinsi kazi inavyofanyika.

Nikizingumza kwa niaba pia ya vijana wenzangu wenye changamoto kama yangu, nimegundua kuwa Vijana wengi tuna mawazo, uwezo, nguvu na hali ya kutaka kufanya biashara lakini tunakwama kutokana na kukosa mitaji.

Na tunapojaribu kutafuta njia ya kutatua changamoto hii hata kwa kukopa, pia inakuwa ngumu kutokana na vigezo vilivyopo ili kupata mikopo hiyo, ila kubwa ikiwa ni dhamana ya kuweka ili kupata mkopo.

Ombi langu kwa idara/ ofisi mbalimbali zinazojihusisha na kuwawezesha vijana (kutoa mikopo), kuweka vigezo ambavyo vitatuwezesha vijana kama mimi kumudu vigezo hivyo, ili kutuwezesha na kufikia malengo.
 
Kama una maarifa ya hiyo taaluma huwezi kukosa mtaji! Mitaji hipo ya kumwaga! Vijana mnapokuwa vyuoni mnajichanganya katika mambo ambayo hayatawasaidia pindi mmalizapo! Mnapokuwa vyuoni mnaambiwa acheni mambo ya kukariri! Jitambue unataka nini katika hiyo field unayosomea! Unaishia kupewa karatasi lililoondikwa CHETI ambalo haliwezi kukusaidia kitaa! Ona sasa unavyoanza kulia kisa eti mitaji! Hata ukipewa mtaji leo baada ya meizi mitatu huna kitu zaidi ya madeni!
 
Wacha Kesho tukawasemee, don't worry! Jitahidi usikilize professional speeches kutoka kwa watu wanaowaza kwa kutumia vichwa vya juu.
 
Mimi ni kajana niliye fanikiwa kusoma na kumaliza Bachelor ya Business Administration.

Tangu kumaliza chuo (2022) hadi leo, nimebahatika kufanya kazi katika kampuni 4 zinazojihusisha na usafirishaji wa mizigo kutoka Nje.

Kutokana na changamoto za kazi, ndo zilinifanya kuhama hama na hatimaye kuacha kazi na kujiajiri baada ya kuona fursa, na kutambua jinsi kazi inavyofanyika.

Nikizingumza kwa niaba pia ya vijana wenzangu wenye changamoto kama yangu, nimegundua kuwa Vijana wengi tuna mawazo, uwezo, nguvu na hali ya kutaka kufanya biashara lakini tunakwama kutokana na kukosa mitaji.

Na tunapojaribu kutafuta njia ya kutatua changamoto hii hata kwa kukopa, pia inakuwa ngumu kutokana na vigezo vilivyopo ili kupata mikopo hiyo, ila kubwa ikiwa ni dhamana ya kuweka ili kupata mkopo.

Ombi langu kwa idara/ ofisi mbalimbali zinazojihusisha na kuwawezesha vijana (kutoa mikopo), kuweka vigezo ambavyo vitatuwezesha vijana kama mimi kumudu vigezo hivyo, ili kutuwezesha na kufikia malengo.
Million 50 zinatolewa Halmashauri
Kigezo ujuane na mtu aliyepo Ofisi kubwa huko Serekalini ndio unapewa kinyume na hapo sahau
 
Kama una maarifa ya hiyo taaluma huwezi kukosa mtaji! Mitaji hipo ya kumwaga! Vijana mnapokuwa vyuoni mnajichanganya katika mambo ambayo hayatawasaidia pindi mmalizapo! Mnapokuwa vyuoni mnaambiwa acheni mambo ya kukariri! Jitambue unataka nini katika hiyo field unayosomea! Unaishia kupewa karatasi lililoondikwa CHETI ambalo haliwezi kukusaidia kitaa! Ona sasa unavyoanza kulia kisa eti mitaji! Hata ukipewa mtaji leo baada ya meizi mitatu huna kitu zaidi ya madeni!
Ahsante kwa ushauri Mkuu 😁.
 
Inakuaje mkuu unakurupuka tu.. Hujala au bange? Mbona unaongea ushangingi? Ni vijana wangap uliwahi wapa mitaj wakafeli?
 
Back
Top Bottom