Hivi kiranga ukirudigi bongo huwa inakuaje ma trafiki wakikustopisha?
Unapiga slang au kibongo.
Hebu tupe experience, ukitoa licence ya us, Matrafiki wana react aje
Shukurani kwa kutaka experience yangu. I am in the mood for a biographical account today.
Sijarudi Bongo miaka 14 sasa.
Nikirudi Bongo siendeshi gari, naweza kujisahau na kuendesha upande wa kulia wa barabara kwa sababu nimezoea kuendesha Marekani.
Wadogo zangu huwa wananipa dereva ananiendesha.
Huwa naongea Kiswahili, lakini nikichanganya Kiingereza watu wanasema naongea kama Mmarekani, wakati mimi nimejitahidi sana niongee Kiingereza cha kimataifa zaidi kisicho cha Kimarekani, lakini nafikiri kukaa na Wamarekani miaka mingi kunafanya matamshi yabadilike hata bila mtu kujua.
Kuhusu vitambulisho miaka ya nyuma sana nilikuwa Zanzibar nataka kuingia Prison Island, just off Forodhani, sasa pale watu wasio Watanzania wanalipa zaidi. Mimi sikuwa na kitambulisho cha Tanzania (kwa sababu nilikuja likizo kutoka New York City na sikuwa natembea na passport ya Tanzania nikiwa Tanzania). Ila nilikuwa na Permanent Resident Card (Green Card) ya Marekani inayoonesha kuwa mimi ni Mtanzania.
Nikawaonesha wale Wazanzibari kama ushahidi kuwa mimi ni Mtanzania.
Waliikubali ile green card kuwa kitambulisho kwamba mimi ni Mtanzania, ingawa ni document ya serikali ya Marekani.
Nilishangaa sana.
That was in 2012. Sijarudi tena Tanzania mpaka leo. Wazazi wangu kuwa wanakuja sana huku, na ndugu zangu wengine kuwapo huku, inachangia kunifanya nione nishawaona watu muhimu bila kuja Tanzania.
Nilisubiri sana kizalendo niwe na green card tu bila kuchukua uraia wa Marekani, hususan kwa kutumaini habari za uraia pacha.
Ila nikawa napanda ngazi kazini na kazi nyingine za juu zinazotaka security clearance huwezi kupata bila kuwa raia wa Marekani. Benki Kuu ya Marekani (Federal Reserve) walitaka niende kufanya kazi nao, ila tatizo ikawa sina uraia wa Marekani.
Nikasema hapa uzalendo umenishinda, nina mambo ya kuyakamilisha na kukosa uraia wa Marekani kutani cost.
Kufikia 2016 nikachujua uraia huku US so next time nikija itabidi nilipe kama mtalii wa nje.
Ila kuhusu Kiswahili nakioenda sana, mara nyingi huwa natumia msamiati wa Kiswahili ambao hata watu wanaokaa Tanzania wengine hawaijui.