TPA: Upanuzi wa bandari ya Tanga ukikamilika itakuwa na uwezo zaidi ya bandari ya Mombasa, itapokea tani milioni 2 za mizigo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,923
141,889
Mkurugenzi mkuu wa bandari bwana Erick amesema upanuzi wa bandari ya Tanga ukikamilika itakuwa na uwezo wa kupokea tani milioni mbili za mizigo na wataipiku bandari ya Mombasa Kenya.

Erick amesema upanuzi huo umelenga kuhimili ushindani na kuzishawishi nchi nyingi zaidi kutumia bandari zetu.

Chanzo: ITV habari.

Kazi Iendelee!
 
issue sio kutanua bandari, issue unayo capacity ya kuifeed hiyo bandari kufikia hizo tani 2milioni za mizigo?..

Shida kuu ya tanzania ni uzarishaji mdogo, tutafute akili tuweze kuzarisha sana...low production ndio issue ya Tanzania..
 
unapofanya upanuzi wa bandari usifikirie kubeba mizigo ya watu wengi nje ya nchi yako, fikiri kwanza uzarishaji wa ndani na huku nje iwe ziada sasa....production capacity yetu ni ndogo sana hata kuweza kuifanya Dar port kuwa busy.

wasomi wetu wakae chini wafikiri cha kufanya nchi iwe busy kwa production capacity kuwa juu..
 
issue sio kutanua bandari, issue unayo capacity ya kuifeed hiyo bandari kufikia hizo tani 2milioni za mizigo?..

Shida kuu ya tanzania ni uzarishaji mdogo, tutafute akili tuweze kuzarisha sana...low production ndio issue ya Tanzania..
Uzarishaji=uzalishaji
 
Porojo tu hakuna kinachofanyika
Unajua uwezo wa bandari ya Mombasa wewe, au unaandika tu ? Mwaka jana Mombasa ilipokea tani milioni 35. Bandari yetu ya dar kubwa kuliko zote nchini ilipokea tani milioni 17 tu. Kwa hiyo hata iwe imekamilkia ya Tanga , bandari ya dar na Tanga hazikaribii mizigo inayopokewa na Mombasa. Uzalendo maana yake sio kutuandikia uongo ndugu yangu. Nenda google upata ukweli. Na Kenya wakijenga bandari ya Malindi , ni basi tena hatuwapati
tena kea capacity ya kupokea mizigo.
 
Kumbuka Mombasa ni kisiwa,Tanga sio kisiwa.Usilinganishe Kisiwa na nchi kavu,iliyozungukwa na bahari.
Siongelewi habari za kisiwa au nchi kavu, nazungumzia miundo mbinu iliyopo Mombasa kamwe haitakuja kupatikana Tanga port.
 
Ni ndoto ya mchana kweupe kuilinganisha bandari ya Tanga na Bandari ya Mombasa.

Mombasa wapo mbali sana na Bandari ya Tanga na hautatokea Tanga kuipata Mombasa port.
Lugha za kufurahisha...tunaweza kuipita Bandari ya Mombasa, tena sana..Ila baada ya miaka 20 au zaidi
 
Back
Top Bottom